Dudubaya Atema Cheche Baada ya Kusikia Ugomvi wa Ali Kiba na Diamond

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dudubaya anajulikana kama mmoja wa Wasanii wa siku nyingi bongoflevani ambae pamoja na headlines zake binafsi huwa anasikika mara chache akizungumzia au kutoa ushauri kwa ishu kadhaa za Wasanii wenzake.
Baada ya kusikia yanayoendelea kati ya mastaa wa bongofleva Diamond na Ally Kiba kwamba wako kwenye beef, Dudubaya alikutana na AyoTV Dar es salaam na kuyasema yafuatayo >> ‘Wasanii wa Tanzania tuna wapambe na sio marafiki kwa sababu mpambe unaweza kuwa umelewa yeye ndio anakoleza ugomvi lakini rafiki ni yule anaekuonya au kukushauri’

Ali Kiba alifanya ngoma na R.Kelly nikafurahia na nikapenda kinoma kupiga salute kwa mdogo wangu anakwenda next level, Diamond kaja kufanya vizuri na ninafurahia… muziki huu unakosa nguvu kwa sababu ya roho mbaya, wivu na chuki na kutokuwa makini na wanaotuzunguka, anakwenda kwa Diamond anasema hivi kisha anakwenda kwa Ally Kiba anasema hivi’ – Dudubaya
‘Ninachowashauri hawa wadogo zangu watulie chini wajitambue ni Wasanii na usanii wao ni wa kutengeneza pesa, tena watengeneze hata Tour ya Amani wazunguke nchi nzima.. wazunguke hata Afrika Mashariki na sio hizi beef’
‘Siku moja nilikua na Dully Sykes na Christian Bella alafu watu wakawa wanasema Diamond ooohhh sijui kashindaje tuzo saba, nikawaambia hivi ukiwa na akili timamu wimbo kama ‘my number one’ kila kona unayopita, video mpaka TV za kimataifa zinapiga alafu leo unaweza video yako ya kijingajinga unategemea kuishinda ‘my number one’ …….Diamond alistahili kushinda hizo tuzo saba, mimi sikuona cha ajabu’
Kwenye sentensi nyingine Dudubaya amesema ‘kuna gazeti moja liliandika eti Diamond alihonga hela kuchukua hizo tuzo, ni vitu vya kipumbavu kabisa… hujui kusoma lakini picha lazima uione, Ali Kiba na Diamond kila mmoja ana mama yake, wakae chini kama binadamu wajitambue, waachane na mambo ya watoto wa hapa mjini hawa ni wapambe tu mwisho wa siku hawana msaada’
Unaweza kumsikiliza Dudubaya zaidi hapa kwa kubonyeza play kwenye rangi ya orange hapa chini.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. da kweli dudubaya nimeamini ukubwa dawa, umeshauri kisomi kabisa hapa

    ReplyDelete
  2. Safi sana dudubaya misanii mengine imekaa kinafki sanabna wanapenda kuchochea ugomvi. Kwanza huyu Dully sina imani nae kabisaaa ukiangalia kiundani anajikomba sana kwa dimond halafu anajitia anamsuport sanaaa kumbe mnafki akikaa pembeni anamdis tu haya why aanze kumuongelea vibaya domo pembeni kama hakustahiki tunzo zote zile wakati kwa insta yake shobo nyingiiii na caption zake za vijembe kwa alikiba daaah namshangaaga sana. Minina ushauri kwa dully awaache madogo wafanye kazi asiingize machuki yasiokuwa nafaida ameshakuwa sasa misifa yake akamuonyeshee mnyama waunyamani TID yule ndo saiz yake atuachie hawa watu wetu.

    ReplyDelete
  3. Dudubaya kweli mkubwa anaona mbali nakubali ushauri wako daiomond na kiba wamezungukwa na madui wanachotakiwa tu wayamalize alafu hawa viongozi wao nao niwanafiki sana pia daimond anatabia ya kusikiliza maneno ya watu mimi naimani kabisa kiba hana tabia hiyo kwayo sisi mashabiki tunataka amani kutoka kwenu

    ReplyDelete
  4. yaaan kwa kweli mm nimempenda sanaaa DUDUBAYA kuliko yule mfirwaji LE MUTUZ kazi kuchochea ugomvi usio na maana eti yeye anasema Diamond ni mlima Alikiba ni kichuguu hawezi mfikia Diamond..huu ni usenge hapa sisi tunataka wapatane na sio kuendeleza ugomvi,asante sanaaa dudubaya mungu akujaalie kwa mawazo yako mazuriii,..ubarikiwe sana kakaa!!!

    ReplyDelete
  5. safiii sanaaaa duku bayaaa,asanteee!!!! mawazo yako ni mazuriii sanaa ubarikiweee...ninaimani watasikiliza ushauri wakooo...

    ReplyDelete
  6. kweli Mziki wa bongo umebeba watu tofauti.. dudu baya ni mtu wa mbali kwa domo na kiba kaongea ya maana kwa moyo safi na ya kiume kuliko huyo mtu wao wa karibu ommy dimpoz... salute dudu!!!

    ReplyDelete
  7. Dudubaya sasa umekua kwa kweli,ushauri mzuri sana. Ulichosema ni sahihi kabisa madogo waache mambo ya wapambe cjui matakataka gani ya marafiki uchwara hawa mara nyingi wanapotosha na wako kishabiki zaidi,ukifulia hao wanakimbia. Cha mcngi cc fans tunataka muzuki wa amani na wasanii wetu waishi kwa amani sio mabifu ya kipumbavu. Ally K na Diamond wote ni wanamuziki wazuri nawapenda elewaneni acheni ushamba.

    ReplyDelete

Top Post Ad