Mtoto mwenye umri wa miezi saba amelawitiwa na baba yake mzazi.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtoto huyo alifikishwa Hospitali ya Amana katikati ya wiki iliyopita kwa maelezo kuwa ana maradhi ya kuharisha, lakini baada ya madaktari kumfanyia uchunguzi walibaini kuwa mtoto hakuwa na ugonjwa wa kuhara, bali alikuwa amelawitiwa.

Muuguzi wa hospitali hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe, alisema walimpokea mtoto huyo kwa maelezo kuwa anaharisha. Lakini walipoona tatizo lake ni kubwa, waliwasiliana na daktari wa magonjwa ya watoto, Dk Omar Maiza ili kumfanyia uchunguzi zaidi.

Alisema baada ya daktari huyo kumchunguza kwa mara ya kwanza, ilionekana kuwa mtoto huyo alikuwa amelawitiwa zaidi ya mara moja. “Ilitushtua kuona mtoto akiingiziwa vidole sehemu ya haja kubwa na vikiingia bila shida. Huu ni ukatili mkubwa kwa watoto,” alibainisha muuguzi huyo.

Dk Maiza alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo hospitalini kwake, lakini akasema taarifa zaidi atazitoa leo.

Mama wa mtoto huyo alifariki dunia mwezi mmoja tu baada ya kujifungua watoto pacha.

Hata hivyo, pacha mmoja wa kiume naye alifariki muda mfupi baadaye kwa maradhi kama hayo ya kuharisha.

Baada ya mama wa pacha hao kufariki, ilibidi baba wa watoto hao kutafuta mfanyakazi wa kushinda nao wakati yeye akiwa kazini.

Akizungumza na Mwandishi jana, mlezi wa mtoto aliyefanyiwa ukatili huo, Saada Ismail alisema waliamua kumpeleka mtoto huyo hospitali baada ya kuona anaharisha kuliko kawaida.
Alisema siku zilizopita alikuwa vizuri na yeye ndiye aliyekuwa akimbadilisha nguo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema hakuwa na taarifa za tukio hilo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyo baba alawitiwe pia

    ReplyDelete
  2. Inabidi watu kama hawa washuhulikiwe maana wanaboa wanaharibu maisha ya watu.

    ReplyDelete
  3. Looooo! huyu baba ni baba kweli au maana huo ni uuwaji tenaniukatili sinamengi selikali liangalieni hili maana.

    ReplyDelete

Top Post Ad