Sakata la Flora Mbasha kunasa Mimba Gwajima Akimbia Nchi…Waumini Sasa kugawana Mpaka Mbao za Kanisa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kufuatia  sakata  la  Flora  Mbasha  na  mumewe  likumuhusisha  moja  moja  kiongozi  wa  kiroho  Mchungaji  Gwajima, habari  tulizozipata  ni  kwamba  mchungaji  huyo  amekimbia  nchi….

Habari  toka  chanzo  cha  kuaminika  kilichopo  ndani  ya  kanisa  la  mchungaji  huyo  ni  kuwa  Gwajima  hivi  sasa  ameshauza  karibia  robo  tatu  ya  mali  zake  na  kwamba  moja  kati  ya  magari  yake  ya  kifahari  huenda  likanunuliwa  na  mwanamuziki  Diamond.

Jamaa  hivi  tunavyoongea  anaweza  akawa  ameshatoroka  tayari, maana  hili  sakata  limeanza  kumwendea  hovyo  na  wiki  iliyopita  kuna  madalali  walikuja  hapa  wakiitaka  gari  yake  aina  ya  Hammer, wakidai  kuwa  inataka  kununuliwa  na  mwanamuziki  Diamond,”  kilisema  chanzo  cha  habari  hii.

Kikaendelea  kumwaga  data  kuwa  karibu  wiki  zima  lililopita  mchungaji  huyo  alikuwa  kwenye  mipango ya  kuuza  baadhi  ya  nyumba  zake  na  kwamba  hata  familia  yake  hivi  sasa  haiko  kwenye   makazi  yake  anayoishi  siku  zote…

Hata  familia  yake  sijaiona  karibu  wiki  mbili  hapa  kanisani  na  taarifa  tulizonazo  karibu  waumini  wengi  tu ni  kwamba  jamaa  anataka  kuhama  nchi  lakini  hatujui  ni nchi gani  anayotaka  kwenda  kufanya  makazi  yake  tena  ya  kudumu,” alisema.

Habari  hizo  zinadai  kuwa  baadhi  ya  waumini  wamepanga  kugawana  mali  kadhaa  za  kanisa  pamoja  na  za  Gwajima  mwenyewe  endapo  itagundukia  kuwa  ametoroka  kweli….

Kuna  baadhi  ya  waumini  wamekerwa  sana  na  hii  skendo ya  Flora  Mbasha, wamekuwa  wakijiapiza  kwamba  hata  zile  mali  zake  ni  halali  yao  kwani  zinatokana  na  sadaka  wanazotoa  kila  siku, inasikitisha  sana  kwa  kweli.” alisema  mtoa  habai  hii.

Inasemekana  kuwa  mchungaji  Gwajima amepanga  kuwaaga  waumini  wake  kama  vile  anakwenda  kueneza  neno  katika mataifa  mengine, lakini  ukweli  ni  kwamba  anataka  kuondoka  ili  kukwepa  aibu  kutokana  na  mambo  yanayoendelea…

Jamaa  yupo  kwenye  hali  ngumu, hii  ishu  ya  Flora  Mbasha imemuweka  katika  wakati  mgumu  sana  kwa  sababu  amekuwa  akinyooshewa  vidole  sana, na  kuna  baadhi  ya  wazee  wamekuwa  wakimtaka  atoe  tamko  rasmi  ili  kukwepa  hiki  kikombe  cha  aibu,” kilisema  chanzo  hicho.

Mwandishi  alimpigia  simu  Gwajima  lakini  simu  yake  haikupatikana, na  hata  Diamond  naye  alipopigiwa  simu  ili  kujua  kama  kweli  anataka kununua  gari  la  Gwajima, simu  yake  iliita  bila  kupokelewa  na  hata  alipotumiwa  ujumbe mfupi  hakujibu  kitu
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

27 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kiukweli ni kwamba Gwaj ametutapeli.na lutotezae muda wetu mwingi sisi waumini wake,amevunja baadhi ya ndoa zetu acha yamkute.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata mchumb huna unatangaza kavunja ndoa yako. Unaiua ndoa wewe au unadhani ndoa mkojo kila mtu anayo? Acha kuchafua watu wewe. Uliku wapi kusema siku zote? Mwandishi habari ya mimba iko wapi?

      Delete
    2. We gwajima nn? Mbona ukekua mkali

      Delete
  2. Huna lolote hata ndoa huna wewe,kuna mtu alishikiwa kiboko kwenda kusali kwa Ngwajima si viherehere vyenu,ulikuwa wapi siku zote usiseme ndio unasema leo.

    ReplyDelete
  3. Limbwata la mauzauza ya hapo kanisani yamekukolea,haya Mchungaji wenu ndo anatimua,kimenuka!!!!

    ReplyDelete
  4. MUNGU adhiakiwi, olewenu nyote wachungaji, manabii, na wengine nyote mlitajao jina la YESU nawakati nafsi zenu zinamtumikia shetani. Acheni MUNGU ajidhihirishe hapa hapa mkiwa bado mpo na pumzi yake. Bado tuna nafac ya kutubu, kuteleza c kuanguka, mungu wetu Ni mwema, mwingi wa huruma, na mwenye kusamehe!

    ReplyDelete
  5. Aibu sana kujiita mtumishi wa Mungu halafu unafanya mambo ya kishetani, huku unajifanya kuhubiri injili watu waokoke. kweli Dini Imeingiliwa. ila maandako yamesema nyakati za mwisho watatokea manabii wa uongo, watawadanganya wengi, ila tutawatambua wa matunda yao. sasa tunajionea.

    ReplyDelete
  6. Halafu wewe mwandishi hiyo habari ya flora upata mimba umeitoa wapi?? tujurishe isijekuwa nawewe ni mbeya unataka kuwachafua watu buree.. tujurishe umejuaje kuwa Flora mbasha ana mimba ya Gwajima? toa habari zilizokamilika. Acha ubabaishaji. ukishindwa kuthibitisha basi nawewe utakuwa ni walewale wachafuzi na unahitaji kukamatwa na kutiwa nguvuni. huwezi kuandika kichwa habari kuwa flora anamimba ya Gwajima halafu content haielezi nani kathibitisha hiyo mimba.

    ReplyDelete
  7. Wote ndio wale wale tuu wa kung'ata na kupuliza.

    ReplyDelete
  8. mungu ni mwaminifu na ahadi zake nizakweli tutulie mengi sana yatajidhihirisha bongo na ukweli ni km maji na mafuta hujitenga na outcome tumeanza kuziona!!

    ReplyDelete
  9. hihiiiiiihihiiiiiiiiiiiiiii hahahahahahahahahahahhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa majinga hayo kumpelekea gwajima mihela sasa mnalia nini hata alama za nyakati hamzioni khaaa wajinga ndio waliwaooooooooooooooooooooo

    ReplyDelete
  10. Efata + Gwa + Jima=Wajinga ndio waliwao!
    Bwana ameamuru kila atangazae injili apate riziki kwa injili hiyihiyo,sasa mnalalama kitu gani?Kila mtu hula kilicho karibu yake,sasa Gwajima kula Flora imekuwa nongwa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kukimbiwa na Mchungaji, hili ni funzo kwa watanzania, waislam na wakristu ambao kila kukicha wao ni kuyaacha madhebu yao ya zamani na kuingia/kuvamia madhehebu mapya.

      Delete
    2. Wewe hujijui ni mtu wa dini ambacho hujui unachokiabudu sasa. Njoo jumapili kanisani kama unafikiri gwajima ni mtoto mdogo eti akimbie . Hayo madhehebu yenu kaeni nay9 muendelee kuabudu msivyovijua mnafata mkumbo dini ya baba dini ya bibi hujui ulifanyalo. Mnaamini waandishi wa udaku maana ni wa kuzimu. Njoo jumapili kama Gwajima kakimbia kwa taarifa za upuuzi kama hizi. Na bado mtasubiri sana. Mazuri yanakuja sijui mtasemaje na bado. Hamna akili nyie kuandika msokijua

      Delete
  11. Kuna siku nilikwenda kanisani kwa gwajima roho yangu ikawa nzitooooooo sikuingia kanisani nikatudi home,hawa wachungaji sidhani Kama wako ok,there is something wrong,wanatumiakia ms freemason.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndo una mapepo hujijui sasa. Unamashetani kabisa yanaogopa nguvu ya Mungu

      Delete
  12. Hahahahaaaaa 1:45 pm unamapepo kaombewe eti rohonzito kuingia kanisani ila guest roho siyonzito

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe ndo mwenye mapepo,na makanisa yenu fake fake ya ulokole,mnaibiwa hakuna Mungu umo ni mapepo tu yanawaongoza.Mungu wa kweli akai kwa wachungaji wazinzi.

      Delete
    2. Mzinzi baba yako na mama yako. Kamtongoza mama yako ? Haman kipya badala ya kufata matendo makuu ya Mungu mnadanganywa na mashetani wenye haya magazeti yanayoongozwa na mapepo. Huna hata haya we kanisa lako lipi lisokuwa na wazinzi ? Kwenda zako huko unamsindikiza kutongoza waawake ? Pondwa kabisa

      Delete
    3. Wew ni bwege na utakuwa kuni cku ya mwisho wewe kwanza nyie ndio mnao tudhalilisha wakristo ina maana muwe wa. Frola anamuongopea mkewe? Iko cku atamuhitaj mkeo chz wew wanamazingaombo mnawaabudu nyiny ni motoni tu

      Delete
  13. mbona habari ya mimba haipo,au kakubebesha ww hebu kua mkweli.

    ReplyDelete
  14. Makubwa haya. MUNGU TUSAIDIE

    ReplyDelete
  15. Acha uzushi shetwani wewe! Huoni Haya jpili Gwajima alikua church sasa wewe unasema Gwajima wa udaku ndiye kakimbia nchi au yupi?

    ReplyDelete
  16. Huyo yapaswa apigwe mawe hadi afe kua fundisho kwa mmbwa wengine

    ReplyDelete
  17. Mtasubiri sana kuanguka kwa Gwajima nyie andikeni kufurahisha nafsi zenu nyie mko mwilini ye rohoni. Andikeni hadi mchoke hamna hara aibu kuandika taarifa za uong0 mkubwa hata hazipo eti waumini wagawana mbao njoo kila jumatatu jumatano na ijumaa na jumapili Gwajima atasimama wala page ya kipepo moja kama hii haimuondoi Gwajima nchini . Uongo mtupu na mnajua mnaadika uongo. Nyie andikeni mlipwe mshahara na mlipe kodi. Mungu tunaemtumikia atajibu kwa Moto. Mtasubiri sana eti mimba ulimsindikiza guest wewe badala ya kufatilia shughuli za kimaendeleo kufundisha jamii unapotosha ti uongo mtupu na unajua ni uongo ulichoandika utalipwa kwa matendo yako

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umerogw hujijui wew mchungaji ana gar la kifahar hummer mil 500 we unakula dagaa unamchangia kweli kawaroga vzur huyo ni mwananazingaombo nyie ni machiz shitukeni!!!!

      Delete

Top Post Ad