google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html VANESSA MDEE azungumzia nia yake ya kushiriki BIG BROTHER | UDAKU SPECIAL

VANESSA MDEE azungumzia nia yake ya kushiriki BIG BROTHER

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

LEO July 11  ndo siku ambayo usaili wa kuwatafuta washiriki watakaoiwakilisha Tanzania katika reality show ya Big Brother nchini Afrika Kusini utaanza kufanyika.

Mara nyingi zinapokaribia siku za usaili mashabiki mbalimbali huweka ubashiri wao wa mastaa ambao wanadhani wanafaa kwenda kutuwakilisha.

Vanessa Mdee ni miongoni mwa mastaa mabao walitajwa na baadhi ya watu kuwa anaweza kufaa kama atawania nafasi hiyo mwaka huu.

Hiki ndicho alichojibu Vanessa kama yuko tayari kuwaridhisha mashabiki wanaotamani achukue fomu na kushiriki kwenye usaili wa kupata nafasi hiyo.

“Nasikitika kuwaambia wale wote ambao wangependa kuniona katika nyumba ya Big Brother kwamba haitakaa itokee” Amesema Vee Money na kutaja sababu, “character yangu haiendani na kukaa kwenye nyumba na watu wengi hivyo, yaani I will be so defeated yaani ntatoka siku ya tatu afu ntawa disappoint wale waliokuwa wanapenda niwe pale”.

Licha ya yeye kutokuwa na wazo la kushiriki ila amemtaja mtu anayedhani anaweza kufaa kwa nafasi hiyo.

“I think Rahim should Try, Rahim da Prince. Rahim I think he understands a lot about the world halafu pia ana personality he is very outgoing so nadhani angeweza kufanya vizuri pale”.

Lakini pia amemtaja mtu ambaye hastahili na asiyetakiwa hata kujaribu kuchukua fomu:

“Nadhani mpoki asiende”.LOL!

Usaili wa kuwatafuta wawakilishi wa Tanzania kwenye Big Brother utafanyika kwa siku mbili kuanzia leo July 11 na July 12 katika hotel ya New Afrika jijini Dar.

Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad