Wavuta Bangi na Watumia Unga Waiwinda Roho ya RAY C

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wiki  za  hivi  karibuni  mwanamuziki  wa  bongo  fleva  ambaye  pia  ni  mwanaharakati  wa  kupinga  matumizi  ya  dawa  za  kulevya  Rehema  Chamila  ‘Ray C’   amepatwa  na  misukosuko  mingi  ambayo  haikuwa    mbali  sana  na  mahusiano  na  dawa  za  kulevya….
Ni  wiki  mbili  zilizopita  tangu  mwanadada  huyo  achezee  kichapo  toka  kwa  mwanamuziki  wa  bongo  fleva  Rashid  Makwilo  maarufu  kama  Chid  Benz  akimtuhumu  kumpotosha  mkewe….
Ikumbukwe  kuwa  kabla  ya  tukio  hilo  la  Chid, Ray  C alikwaruzana  na  Legend  wa  bongo  fleva  TID  baada  ya  kuposti  kwenye  mtandao  wake  ujumbe  wa  kumuomba  waongee….
TID  alimuijia  juu  mrembo  huyo  kwa  matusi  kibao  na  kumtaka  akae  mbali  nae  na  asimfuatefuate….
Ni  hivi  karibuni  Ray  C  ameanza  harakati za  kuokoa  wasanii  na  watu  ambao  wanahisiwa  kutumia  madawa  ya  kulevya, hali  ambayo  imemfanya  ajijengee  maadaui  wengi  kwenye  jamii  ya  watumiaji  wa  madawa  ya  kulevya  ambao  wameapa    kumsambaratisha….

“Ray  C anajisumbua  bure  tu, anashindana  na  sisi, sisi  kama  anaona  tumepotea  atuache,kwanini  asihangaike  na  mabwana  zake  kwanza?  huyu  demu  vipi?,”   alisikika  teja  mmoja  maarufu  kwa  jina  la Lima  wa  Tandika.

Lima  aliyekuwa  akipewa  sapoti  na  wenzake  waliokuwa  pembeni  yake  aliendelea  kufunguka  kuwa  Ray  C asiendelee  kuumiza  kichwa  kudili  nao, kama  yeye  ni  mwanaharakati  wa  kweli  basi  adili  na  wanaowafikishia  hayo  madawa….
“Mi  nashangaa  kumuona  akihangaika  na  sisi  wakati  kuna  watu  ambao  anapaswa  adili  nao. Awatafute  wale  kama kweli  yeye  ni  shujaa,” aliongeza  kijana  mmoja  aliyeonekana  kuzidiwa  na  kilevi.
Kijana  huyo  alimuonya  mwanadada  huyo  asiwafuatilie, lasivyo  atahatarisha  maisha  yake  kwani  wakubwa  wakijua  watakasirika  sana  na  wanaweza  kumfanyia  chochote.
“Mngemshauri  tu  aachane  na  sisi, wakubwa  wetu  wakijua  ni  kesi  kubwa  mno, sijui  kama  anaweza  kupambana  nao,” aliongeza  kijana  huyo.
 Teja  huyo  alienda  mbali  zaidi  na  kudai  kuwa  alichofanyiwa  na  TID  na  Chid  Benz  ni trela  tu, akitaka  picha  kamili  aendelee  kuwafuatilia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad