Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu yaahidi Kulipa Fedha za Mafunzo kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB), imesema mwishoni mwa wiki hii, itakuwa imelipa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ambao hawajapata fedha hizo kwa mwaka 2013/14.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/15.

Alisema bodi hiyo ilikwama kuwalipa baadhi ya wanafunzi walioanza mafunzo kwa vitendo Julai mwaka huu kutokana na uhaba wa fedha.

Aliongeza kuwa, hadi sasa vyuo vitano ndivyo ambavyo wanafunzi wake hawajapatiwa fedha hizo, lakini hadi mwishoni mwa wiki hii, fedha hizo zitakuwa zimeingizwa kwenye akaunti zao.

Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo cha Tumaini Makumira Arusha (TUMA), Chuo cha Mtakatifu Stefano Moshi (SMMUCO), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mtakatifu Agustine Mwanza na Chuo cha Theophil Kisanji (TEKU), ambapo jumla yao wapo wanafunzi 9,946.

Katika hatua nyingine, Mwaisobwa alisema hadi wanafunga maombi ya mikopo Julai 31 mwaka huu, wamepokea maombi ya mikopo 58,037 kati ya hiyo, wavulana 37,689 na wanawake 19,592,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwel jitahid muwape khaki zao kwan vjan wanateseka zaid wafanyao mafunzo kwa vitendo maeneo yasiyo kwao ila nawapa pole xn kwa kpnd kgum mluchoptia hatimaye muda mchache ujao yaweza kuwa faraja kwen,amin!

    ReplyDelete
  2. Kwel jitahid muwape khaki zao kwan vjan wanateseka zaid wafanyao mafunzo kwa vitendo maeneo yasiyo kwao ila nawapa pole xn kwa kpnd kgum mluchoptia hatimaye muda mchache ujao yaweza kuwa faraja kwen,amin!

    ReplyDelete
  3. hawa jamaa wa bodi ya mikopo ni wezi tu, hizi hela zinatolewaga mapema lakini wao wanazifanyiaga shughuli zao kwanza kuzizungusha wakishapata faida ndiyo wanawalipa wanafunzi, inabidi hiki kitu kiwekwe sawa, sbabu yanawapa wanafunzi matatizo mengi.

    ReplyDelete

Top Post Ad