Jakaya Aishi Kwa Matumaini Upatikanaji wa Katiba Mpya, Asema Yupo Tayari Kukutana na Ukawa Kunusuru

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

RAIS Jakaya Kikwete amesema yupo tayari kukutana na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ili kunusuru mchakato wa Katiba mpya.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja siku chache baada ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kupinga hatua ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumtuma Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, kusaka suluhu na viongozi wa Ukawa.

Akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro juzi, mara baada ya kusoma risala yao na kuunga mkono Bunge la Katiba, Rais Kikwete alisema hana 

sababu ya kutokutana na viongozi waliosusia vikao vya Bunge.

Alisema kutokana na hali hiyo, yupo tayari kukutana nao, na kwamba wanajua namna ya kukutana naye ili waweze kufanya mazungumzo yatakayoliwezesha taifa kupata Katiba mpya.

“Mimi sina tatizo la kukutana nao. Wanajua jinsi ya kukutana nami ili tuweze kutafuta namna ya kumaliza tofauti hizi.

“Mimi naishi kwa matumaini. Naamini kuwa tutafika mwisho vizuri. Mchakato ni mgumu, lakini barabara ndefu haikosi kona. Tukidhamiria kweli kweli tutafika tuendako vizuri,” alisema Rais Kikwete.

Alisema anasikitishwa na tofauti za viongozi wa siasa na kuleta mfarakano kwa taifa, hali ya kuwa tangu awali aliwaambia kuwa wakijiruhusu kushindana na kuviziana ni wazi mchakato wa Katiba utakwama.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mkundu huyoo kikwete hajitambuii anakula pesa za wananchi anatembea na magar zaid ya 20 for what.....????????????????ulinzi kwan hatakufaa mungu ndo anapanga kifoo ..

    ReplyDelete
  2. sms bila tusi haifiki? tuweni na hekima jaman ka hatuna malez ya wazazi dah

    ReplyDelete
  3. Its too late my dears.hata akikutana na ukawa leo haina maana kwa sababu mabilioni kibao ya masikini watanzania yalishateketea kwa kutumiwa na wezi wa CCM.na yeye mwenyewe alishazidiwa nguvu na majambazi wa ccm tangu mapema so ni mchezo wa kuigiza tu anacheza hapo.huyu Kikwete alikuwa anataka aache historia ya kuwatengenezea watanzania katiba bora ila kile kikao cha ccm kilichokaa dodoma kipindi flani hivi nyuma ndio kilimtisha na kikaharibu kila kitu na akina mzee mkapa na mwinyi ndio wakamtisha zaidi kwamba hiyo katiba itamgeuka na yeye.....sasa kwa udhaifu na uoga wake wa kufanya maamuzi na kusimamia msimamo wake kama amiri jeshi mkuu ndio ametufikisha hapa.na yeye hajajitambua tu kwamba sasa badala ya kuacha historia ya kuachia watanzania katiba mpya sasa ataandika historia ya chama kikongwe cha CCM kumfia mikononi mwake........

    ReplyDelete
  4. ht ukawa nao wezi walewale

    ReplyDelete
  5. Ndugu wananchi hebu muache matusi huwezi kumtukana mh.Rais hadharan hivo kama huyo mjinga aliecomment hapo juu naomba police/ maafisa usalama wamkamate achukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wengne mnaotukana kwan inawezekana kumpata.By Jackson

    ReplyDelete
  6. Ndugu wananchi hebu muache matusi huwezi kumtukana mh.Rais hadharan hivo kama huyo mjinga aliecomment hapo juu naomba police/ maafisa usalama wamkamate achukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wengne mnaotukana kwan inawezekana kumpata.By Jackson

    ReplyDelete
  7. matusi siyo mazuri kwa mtu yeyote haswa haswa aliyekupita umri na hata kuweza kukuzaa, tatizo ni elimu duni wanayopata hawa vijana wasiku hizi ndo zinawafanya wakose adabu, kama mtu waweza tukana hivyo hadharani basi hapo mbeleni itakuwa shida!!

    ReplyDelete

Top Post Ad