Kassim Mganga Amwagia Sifa Ali Kiba, 'My Favorite Artist'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwimbaji kutoka Tanga, ‘Tajiri wa Mahaba’ Kassim Mganga amemtaja Ali Kiba kuwa ndiye msanii  wa bongo flava anaemkubali zaidi Tanzania.

Ali Kiba amefunguka katika mahojiano maalum aliyofanya na tovuti ya Times Fm na kueleza kuwa mbali na kuwa ni mwimbaji mwenye uwezo mkubwa, hata kitabia yuko vizuri.

“Ali Kiba (ndiye my favorite artist in TZ), mimi binafsi nampokea vizuri sana. Nafikiri anachokifanya mimi kinanivutia sana. Napenda uandishi wake, napenda melodies zake na napenda utulivu wake. Ana hekima kama zangu, yuko kimyaa (anacheka).” Kassim ameiambia tovuti ya Times Fm.

Kassim Mganga ameeleza kuwa mwaka jana kabla hajatoa wimbo wake ‘I Love You’ uliokuwa hit, alikuwa na mpango wa kufanya wimbo na Ali Kiba na walikuwa tayari wamekubaliana lakini mambo yaliingiliana na kazi haikukamilika.

Katika hatua nyingine, Kassim Mganga ameeleza kuwa watanzania hatupaswi kuendekeza majigambo na uadui kati ya wasanii badala yake kufanya kazi na kuwasapoti wale ambao wanaiwakilisha nchi yetu katika mataifa mbalimbali kama vile Diamond badala ya kuwajengea uadui.

“Diamond ni mtu ambaye ameweza kutufungulia sana soko letu kiukweli, tunashukuru. Tunatakiwa kuwa nyuma yake tumsapoti tuendelee kumsukuma na sisi huku tunaendelea kujongea. Kwa hivyo, vinapokuwa vinajengwa vitu kama hivyo (uadui/majigambo) sio jambo zuri kwa sababu vinajenga uadui na mwisho wa siku muziki tunakuwa tunaufanya kimajigambo tu lakini sio kwa ajili ya kuutangaza muziki wetu…”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. cna nongwa na diamond naheshimu kazi zake, lakini Kiba is ma number one dude!! jamaa ni mkali.

    ReplyDelete
  2. Ali kibazaidi kiukweli bilaupendeleo

    ReplyDelete
  3. "Sio uadui / majigambo"Nimependa hiyooooooooooooooooooooooooo,
    Kiba hajigambi,nampenda

    ReplyDelete
  4. umenena kaka mkubwa Mimi nimekuelewa kila mtu anaaina ya muziki anoupenda mimi pia mziki wa kiba unanikonga sana moyo

    ReplyDelete

Top Post Ad