Waziri wa Mkuu Mizengo Pinda Avunja Ukimya na Kutangaza Kugombea Uraisi 2015

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Mkuu Mizengo Pinda, amevunja ukimya na kuamua kutangaza nia yake ya kutaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.

Pinda alitangaza nia hiyo juzi usiku Ikulu ndogo ya Mwanza jijini Mwanza, mara baada ya kuwaalika wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) toka mikoa sita ya Kanda ya Ziwa.

Habari kutoka vyanzo vyetu vya kuaminika zilieleza kuwa Waziri mkuu aliwaalika wajumbe tisa kutoka katika wilaya zote za mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera.

Pinda aliyekuwapo jijini Mwanza kwa ajili ya kuendesha harambee ya Mfuko wa Taasisi ya Benjamin Mkapa iliyofanyika jana usiku, alikutana kwa ‘mafungu’ na wajumbe zaidi ya 50 kutoka Mara, baadhi toka Mwanza, Geita na Kagera.

“Wajumbe wengine wa Shinyanga, Simiyu na wale Mwanza na Geita alikutana nao jana (juzi) jioni ili kuwashawishi wamuunge mkono  baada ya jina lake kupitishwa na NEC,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kilisema wajumbe toka wilaya hizo za Kanda ya Ziwa, walianza kuwasili Ijumaa mchana jijini Mwanza kwa lengo la kuitikia wito wa Waziri Mkuu kabla ya hawajatangaziwa nia yake.

SABABU ZA KUTANGAZA NIA
Waziri Pinda aliwaeleza wajumbe hao sababu kubwa zilizomfanya aguswe kutangaza kuwania nafasi ya Rais 2015, ni kutokana na ushawishi mkubwa toka kwa maaskofu, masheikh, baadhi ya wabunge, watu maarufu pamoja na mke wake.

Sikuwa na nia hiyo kwa vipindi vyote vitatu vya ubunge wangu, lakini watu hao akiwamo mke wangu, nimeshawishika kutaka nafasi hiyo,” alisema Pinda.

Alisema ameona hana sababu ya ‘kuzembea’ kutangaza nia ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao.

SIFA
“Ninazo sifa za kunitosheleza kuwania nafasi hii, ikiwamo kutokuwa fisadi, pia nimekuwa ndani ya viongozi wa nchi wa awamu zote nne tangu 1974 enzi za Nyerere (Julius), Ali Hassan Mwinyi, Mkapa (Benjamin) na sasa Kikwete,” alidai.

Aidha, alisema kutokana sifa hizo hataweza kuchangishiwa pesa za kuingia madarakani kama wengine (hakuwataja), bali atawapa kiasi alichonacho ili kuwawezesha kumsaidia.

Pinda maarufu kama “mtoto wa mkulima”, alidai anaamini viongozi wakuu waliopita madarakani na kuongoza nchi, wanamuunga mkono.

VIKAO VYA CHAMA
Kutokana na nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya Maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ana uhakika jina lake halitaweza kukatwa na litafikishwa katika mkutano mkuu wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama.

“Kama wajumbe wa mkutano mkuu, mjiandae ‘kunibeba’ kwani kati ya majina matano yatakayotajwa na kamati kuu, nitakuwamo na pia na kati ya matatu pia nimo…nguvu zenu ni katika mkutano mkuu.”

Ilielezwa kati ya majina matano ambayo yatapelekwa Kamati Kuu, moja ni la Pinda, mwanamke, kijana, mgombea toka Visiwani na waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

Hata hivyo, hofu ya Pinda ilielezwa ni baadhi ya wajumbe walioalikwa kuwa miongoni mwa wapiga debe wa baadhi ya walionyesha nia ya kugombea nafasi hiyo akiwamo Lowassa.

Aidha, habari toka ndani ya kikao hicho zilidai, wajumbe walioalikwa kuhudhuria mkutano huo waligoma kupokea mgawo wa Sh. 50,000 zilizotolewa baada ya kumalizika kwa kikao.

NAPE
Uamuzi huo wa Waziri Mkuu kutangaza nia unaenda kinyume na chama chake ambacho hivi karibuni kiliwafunga ‘midomo’ wanachama wake kutangaza nia hiyo kabla ya muda akiwamo Lowassa, Bernad Membe na Frederick Sumaye.

Juhudi za NIPASHE kumpata Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, kuzungumzia ‘nia’ hiyo ya Pinda, zilishindikana kutokana na simu yake ya mkononi kutopatikana.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. na nyuki atamuachia nani.

    ReplyDelete
  2. Mpaka leo hajui kazi ya wm imemshinda .

    ReplyDelete
  3. kila mtu anautaka huu uraisi, nadhani uraisi huu wa Tz unalipa kishenzi, ngojea na mimi nijitangaze!!

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa Pinda kalime kijijini ndiyo inayokufaa sasa naona ni bora hata tukapata raisi fisadi lakini akaiendeleza nchi na wananchi wake, sifa yaku Raisi siyo uaminifu peke yake. Hawa maraisi ambao wanashindwa kumkalipia hata mkuu wa wa wilaya hatuwataki. Tunataka mtu kama Raisi wa Ruanda ameiendeleza nchi na wananch wake, Tanzania ipo kama Somalia baada ya miaka zaidi ya 50 kupata, vijana hawana ajira, mji mchafu, usalama ukiweka pesa benki taabu, ukienda zichukua mtu na boda boda anakusubiri njiani akuue achukue, kuziweka nyumbani unaogopa, wananchi wanashindwa kuishi kwa kupata mlo mmoja kwa siku, vijana wanakimbilia mjini kuwa machinga na wezi, mwananchi anaogopa kuwa na simu nzuri, kwakweli bora raisi fisadi atuibie lakini atuletee maendeleo.

    ReplyDelete
  5. Ni bora ukafungue kanisa mzee wetu,maaana hata sijui tukuite mpole sana au
    unaogopa lawama kukemea maovu sijui.kwa ujumla kazi za mshikemshike wewe huziwezi.
    Asante hata hapo ulipotufikisha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata kanisani hawezi,maana kanisani hakuna kufumbia maovu.

      Delete
    2. Akaendeleze ufugaji wa nyuki.

      Delete
  6. Akikua ataachakua mpole

    ReplyDelete
  7. Lakini kwakua yeye ni mkatoliki atakua Rais kwasababu waatoliki ndio wenyehaki yakua marais kwa upande wa wakristo niwaotu,

    ReplyDelete
  8. Mpole sana hafai, tanzania inaitaji raisi mwenye amri aina fulani ya udikteta.

    ReplyDelete

Top Post Ad