Baada ya Kimya Kirefu Director wa Video Nick Dizzo Nae Aongelea Suala la Wasanii Kufanya Video Nje ya Nchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Toka Kina Diamond na Ommy Dimpoz Waanze Kufanya Video zao nje ya nchi Kumekuwa na Mijadala Mingi Kwenye Social Media Kuhusu Suala Hilo wengine Wakisema ni Bongo hakuna Madirector Wazuri , Wengine Wakisema Bongo Hakuna Vyombo Vizuri kwa Kazi Hiyo ..

Leo Director Mkali wa Video za Bongo Nick Dizzo Nae Amevunja Ukimya na kuongea na Udaku Specially Kuhusu Suala Hilo Kama Ifuatavyo:

"Mimi kama mimi sidhani kama ni tatizo kwa.mtu yeyote kufanya kazi na makampuni ya nje ,sababu hiyo yote ni katika kuboresha na kuleta utofauti katika kazi zao, ila kamwe siyo kwamba hapa Tanzania hakuna vifaa ama directors wanaoweza kufanya kazi bora na nzuri kuliko hizo.Hapa Tanzania kuna kila aina ya vifaa kuanzia cameras,taa,directors na vitu vyote muhimu kwa ajili ya kazi yoyote ni hela tu inahitajika kwenye budget maana hata hizo wanazofanya nje pia zinatofautiana ubora sababu mwisho wa siku ni budgetK
kwa muda mrefu vyombo vya habari vimekua vikilazimisha hii topic kua kubwa ila sidhan kama ina nguvu yoyote.
Kwa takwimu ya haraka haraka ,kwa mwaka video za muziki zinazotengenezwa hapa hapa na makampuni ya hapa Tanzania ni nyingi sana kulinganisha na zinazotengenezwa njee,pia hata ukichunguza kazi zilizofanyika nje na makampuni ya njee siyo zote bora kuliko zinazofanyika na makampuni ya hapa...hivyo sidhani kama kwa sasa hilo ni tishio kwetu...ila cha msingi ni sisi wenyewe kufanya kazi bora zaidi ili hata hao wachache wasiende kabisa nje na ikiwezekana na wale wa nje pia waanze
kufanya kazi na makampuni ya hapa Tanzania So bado naamini kua tuna nafasi kubwa sana" Nick Dizzo

Follow Nick Dizzo :
Instagram: @Nickdizzorusule
Twitter: @Nickdizzo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad