Diamond Azidi Kujiharibia Yamkuta Tena Huko London Usiku wa Kuamkia Leo Jumamosi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Haya promota VICTOR aliye Andaa Show ya Diamond London kashikiliwa na polisi, walionunua ticket kuona show yake wamegoma kuondoka hadi warudishiwe pesa na wamerudishiwa.

Diamond hakuonekana ukumbi wa La Face huko London ambapo alitangaza kutumbuiza, na kesho alidai usiku wa tar 20 atatumbuiza ujerumani bure. na hadi mida ile hakujulikana alipo au imekuwaje...tusubirie

Sasa huyu kijana amekuwa anapata bahati mbaya hivi..... Maana inakuwaje juzi iwe ujerumani leo london michezo ya ajabu inamtokea?

HAYA UKWELI TUUSUBIRIE KUUSIKIA AS NDIO BADO HAKUJAKUCHA SASA.... ukweli/uongo utakuja

ila mie nimechoka kumsikia eti show show inabidi management yake ijifunze kitu wasiburuzweeeeeee...tutasikia. inasikitisha sie tunaependa miziki yake na jitihada zake

*******
SIJUI NINI KINAENDELEA JAMANI ILA NAANZA KUMUONEA HURUMA AS EARLIER KWA FB PAGE YAKE ALIANDIKA HIVI

"Tafadhali, nikikuomba unipangie list ya nyimbo ambazo ungependa niziimbe usiku wa leo pale #LAFACE_CLUB London utanipangiaje???...
(if i ask you to arrange a playlist for my Performance tonight at #LAFACE_CLUB #LONDON how would it be.....?)"

ALIKUWA TAYARI KABISAKUTUMBUIZA...... HAYA TUTASIKIA

********
SASA CHA KUSHANGAZA ZAIDI NI KUWA

Masaa kama 7 yaliyopita niseme kama saa 5 usiku mida ya London, alirusha kideo kikionyesha ukumbi huko Ujerumani atakapo piga ile show yake siku ya jumamosi tar 20 Sept (BURE) kufidia yaliyotokea siku ambayo akufanya show. the huku iko hivi ameacha tena sohooo huko London la kutofanya show

Itabidi ajibu kuwa alikuwa wapi mida aliyotakiwa kuwa ukumbini London, nimeona ameanza kuitwa tapeli...

WEWE DIAMOND KAMA ULIKUWA UNAJUA UTAKUWA UJERUMANI KWANINI HAUKURUSHA UJUMBE KUOMBA MSAMAHA FANS WAKO WASISUMBUKE KWENDA?????

TUSUBIRIE STORY ZA KAPUNI....VIDEO TENA MNASIKIKA MNAONGEA KISWAHILI...HOW COME? TUFAFANULIE TUJUE MAANA IKIWA ULISAFIRI KWENDA KWA MWEST KUMFURAHISHA MMMHHHH...SEMA MAANA LAZIMA UTASEMA WA UK HAWAKUKUPA PESA MLIZOAHIDIANA AU???

****
OK DIAMOND KWA INSTA KAMRUSHA MKAKA PICHA NA KUANDIKA HAYA

Tafadhari ndugu zangu wa UK!!!....kuweni makini sana na promoter huyu (Victor - Dj rule) mnaposikia kaandaa show, party au Hafla yoyote...ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwasababu ni tapeli.... si unajua aisifiae mvua imemnyeshea... basi mie nimeloa kabisa!"

HIII NI KAMA SAA MOJA ILIYOPITA YAANI SAA 11:40 ASUBUHI MIDA YA LONDON


MAJIBU NAYO MOJAWAPO NI

"embu jieleze vizuri sasa maana wengi tukisikia show zako hatutakuja hata kwa kunusa mlango. kwanini unamuita tapeli? juzi ujerumani ulisema hivyohivyo yule kaka tapeli embu sema acha uswahili na kutapeli jina ni lako kamahaujifunzi shauri yako. sema elezea nini sio kukmchafua mwenzio bila proof"

"A piece of advice naomba uwe na mwanasheria wakuangalia hiyo mikataba sasa kuna vitu vimejificha nyuma ya kutaka kukuharibiaa kazi shemu letu kuwa makini na jitahidi uwe na mwanasheriaa binadamu sisi wabaya walaaahi nakuambia kuna kitu tuu hapa c bure"

"Kwanza kama wasemvyo wadau, hizo ni njama, shtukia chezo na ujipange kimataifa na kimaarifa zaidi. Set new terms and hire a professional lawyer kwa ajili ya kuingia mikataba ya kazi zako na kusimamia. Haya yasikuyumbishe wala kukurudisha nyuma bali yawe ngazi ya kufikia kule wasikotaka ufike. @diamondplatnumz"
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. asipojipanga atapoteza washabiki wa kuenda kwenye shows zake, kama anaona sifa kutwa ziarani kufanya shows na hana uhakika na mikataba anayoingia nayo ajipange ile ya german ilitosha kuwa funzo na isijuridie iyo sasa ni usumbufu watu wameshajijengea show ya dai haina uhakika tena waeza show up kwa place na kusikue na kitu kinaendelea is about time kaa chini upumzike na ujipange upya or else utasahulika dogo!! hakuna mtu atataka kununua ticket feki pound 20 or 50 atafanyia mengine

    ReplyDelete
  2. Anadai fee kubwa sana. Waandaji weyewe wanangoja kiingilio ndio wamlipe naye anataka kulipwa kabla!! Ingia mkataba mzuri lipwa kianzio halafu piga shoo ondoka wakulipe inayobaki ktk account. Wasipofanya hivyo washitaki. Utaset utaratibu wa kistaarabu. La sivyo tulis myumbani labda hujafikia level ya kimataifa!

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana kabisa na wewe mdau hapo juuu. Haka kapiga mchiriku kanajifanya kako so expensive. Hawa mapromota hizo hela anazozidai watazipata wapi??? Kwa nini asiweke madau ya kawaida kama wanamuziki wengine wa level yake?????? Sasa hapo kalipo kanajifanya kamekuwa Jay Z wapi bwana nenda mdogo mdogo hiyo level ya kudai hayo mahela unayoyataka bado hujaifikia. Kajidanganya na hizo video zake mbili tatu ambazo ni feki vile vile. Na pia anajiona na hizo awards zake ambazo ni scrap. Hovyo kabisa huyo aende kule na mchiriku wake akawadanganye hao Watanzania ambao hawajafunguka. Mtu mwenyewe hata akienda ulaya waingiaji wa show zake ni waswahili wenzake hukuti hata mzungu mmoja wala waafrika kutoka mataifa mengine. Pale New Jersey wa Kenya hawataki hata kumsikia kwa jinsi alivyowatapeli kwa kupiga show ya masaa mawili wakati waliishailipia $20.00 huyo ni mtu wa hovyo kabisa. Na mapromota iwe fundisho kuwapeleka Ulaya wanamuziki uchwara kama huyo Domo.

    ReplyDelete
  4. Au kuna masharti ya dini yake ajatimiza?

    ReplyDelete
    Replies
    1. duh we kiboko ha ha ha h ah ah

      Delete
  5. Weee diamond kwani hunafanya kazi bila mkataba? au ndo lugha gongana? miye nakuwshauri tafuta mwanasheria mzuri awe anasoma mikataba yako kwanza kabla hujaanza kutangaza kupiga show !! Lazima uwe na MWANASHERIA WAKO.

    ReplyDelete
  6. tatizo la huyu jamaa anaendekeza njaa, wewe kama msanii mkubwa huwezi ukawa unakurukupikia tu madili na maproduza wa hovyo hovyo tu, yani unapiga madili yasiyo kuwa na uhakika, anajishusha taratibu huyu.

    ReplyDelete

Top Post Ad