Maelfu Wajitokeza Kumsindikiza Freeman Mbowe Polisi Alipoitwa Kuhojiwa Kuhusu Kauli yake ya Maandamano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAMIA ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), asubuhi hii wamejitokeza kumsindikiza Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kuelekea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yaliyopo Posta jijini Dar es Salaam.

Mbowe amefika makao makuu hayo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli yake aliyoitoa Jumapili iliyopita ya kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.

Katika tukio hilo, baadhi ya waandishi wa habari wamekimbizwa na polisi waliokuwa na mbwa wakitakiwa kukaa umbali wa mita 200 kutoka katika makao makuu hayo ya polisi.

Follow us:
Instagram:@udakuspecially
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu jamaa simuelewi,sijui,nadhani kuna kitu anataka,na ni nini hasa kwa hii nchi?URAIS?
    Sio mtu wa msaada kabisa hata kwa hicho alicho nacho,ana roho mbaya sijaona,si mfano wa kuwa kiongozi kabisa.Akiongea utadhani ni mtu mwenye uchungu na nchi hii pamoja na watu wake.Ni mchochezi sijaona mfano,sasa maandamano ya nini?Kama tumepata uhuru bila kumwaga damu basi tafuta haki bila kumwaga damu,unachochea yakitokea ya kutokea hapa utakimbia nchi na Helkopta yako halafu sisi walala hoi ndio tutaumia.Kwa msiomjua najua mtachonga sana.

    ReplyDelete
  2. Acha uzushi hujuic. Kitu wewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. mdau kasema msiomjua mtachonga sana,mmojawapo wewe.
      eti kweli nini hasa alichofanya kinishawishi kumpa kura yangu?
      Bora yake Zito wa watu!

      Delete
  3. Kweli,mie bora angekuwa Halima Mdee kwenye kinyang'anyiro cha urais angenishawishi kumpa kura yangu,lakini kama wanamsimamisha huyu hapana.

    ReplyDelete
  4. KAVURUGAVURUGA CHADEMA WEEEEEEEEEEEE.! CHADEMA IKO CHALI KAMA MENDE
    ANAPOTAKA KUFA.

    ReplyDelete
  5. yaani sijaona km wewe wasio jua watachonga sanaaaaaaaaaaaaaa ana lolote uchu wa madaraka tu na kuendeleza biashara zao warudi kwao uchagani wakauwane watuache na amani yetu

    ReplyDelete
  6. Ukweli ni huu hakuna Mtu kiongozi wa kiafrika ambaye ataweza kusema hana ubinafsi, je katiba ya chadema juu ya kuongoza inasema nini? Je ungovi wa chadema ni kuhusu nini? je si ungozi kama kuna ungovi juu ya pesa za wanachama ikiwa ni pesa za inchi itakuaje?

    Angalia Zambia Chiluba alitupa madongo juu ya Kaunda nini kilitokea aliposhinda uchanguzi alitaka kugagania hadi kifo kumutenganishe, Mja jirani yetu hataki kuondoka amekuwa wa milele? Kama ktk chadema mnataka kuwa wa milele je mkishika inchi itakuwa Je?

    Angalia Sudani ya kusini Vita hatakuja kuisha hata siku mmoja maana inchi anaza kujegwa ju ya ukabila, mbunduki, nk.

    ReplyDelete
  7. Nyie wachangiaji mnaomshambulia Mbowe ndio hamna akili kabisa au kama mnaxo basi mnashindwa kuzitumia kwa sababu ya kuhongwa vijisenti na watawala ili mje kubwabwaja mitandaoni humu.kwanza sielewi kwa nini mnasema sema sana machafuko?kwani mnamtisha nani na kwanini?sioni sababu yoyote ya machafuko kutokea tanzania.watu waendeshe siasa kwa haki.watu waache kuiba mali za umma.watu waache kutumia polisi kwa manufaa yao wakati polisi hao wanalipwa mishahara kwa kodi zetu....watu waandae mazingira ya haki na wawaache watanzania waamue wanataka kuongozwa na nani na sio kulazimisha kuendelea kutawala milele.....hii nchi ni ya watu wote na hakuna mpuuzi yeyote awaye mwenye hati miliki ya tz.....hakuna sababu ya machafuko tz zaidi ya ccm kutaka kutulazimisha tuingie kwenye machafuko kwa manufaa yao na vizazi vyao......watz tusikubali propaganda chafu hizi za ccm kuendelea kutuona watanzania milioni 50 ni wapumvavu na wao kijikundi kidogo cha watu ndio wenye akili ya kuendelea kutuibia na kutuacha sisi tunakufa kwa umasikini kwa kutupa wakati Mwenyezi Mungu katujalia kila kitu......huuu ni upuuzi wa hali ya juu

    ReplyDelete
  8. Anonymous hapo juu waache waibiwe wameshazoe viongozi wezi na wavivu, mi nashukuru niko zangu mamtoni mawachungulia kwa darubini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na shangazi yako unae huko mamtoni?

      Delete
  9. Shangazi yangu si ni wewe unaesaga rhumba hapo bongo na kuendelea kushabikia chama kilichokaa madarakani zaidi ya umri wako na watoto wako watakaa chini darasani mpaka matako yaote kutu.

    ReplyDelete

Top Post Ad