Picha za Kilichotokea Baada ya Diamond Kupelekwa Kwenye Show Saa Kumi Alfajiri Ujerumani.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mmiliki wa hit single ya ‘mdogo mdogo’ Diamond Platnumz anahusika tena kwenye zile habari zinazoongelewa sana ambapo time hii imetokea Stuttgart Ujerumani.
Alitakiwa kufanya show weekend iliyoisha sehemu inaitwa Stuttgart lakini ikashindikana baada ya kudai kucheleweshwa na Promota na badala yake akampeleka kwenye ukumbi saa kumi alfajiri.
Inasemekana mashabiki wenye hasira waliosubiri kuanzia saa nne usiku walianza kufanya fujo kwa kurusha chupa na kuvunja vyombo vya muziki vilivyokua vimefungwa hapo kwa madai pia kwamba vilikua vibovu ambapo inataarifiwa kwamba Ma Dj wawili walijeruhiwa kwa kiasi kikubwa pamoja na vyombo vyao kuharibiwa.




Diamond alipowasili saa kumi alfajiri tayari mashabiki walikua wametoka nje kama hivi ambapo mmoja wa mashabiki waliokuwemo kwenye tukio hilo amesema Polisi walilazimika kuingilia kati na Diamond hakudhurika.
Platnumz ambae ameahidi kuongea na Amplifaya ya CloudsFM aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii muda mfupi baada ya hilo tukio >>>> ‘kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany, Promoter anatupeleka kwenye show saa kumi alfajiri‘
‘Naomba mtambue halikua kosa langu, mimi ni mgeni tu na ninafata maelekezo ya Promoter hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaotaka mimi‘ – Diamond
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad