Diamond Platnumz’ Asalimisha Nguo Zake za Kijeshi Kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Mwanamuziki Nassib Abdul, ‘Diamond Platnumz’ amesalimisha nguo zake za kijeshi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Diamond alisema kuwa juzi alipokea wito uliomtaka afike kituoni hapo (Oysterbay) akiwa na madansa wake pamoja na nguo hizo. Alisema haikuwa rahisi kwake kutii amri ya vyombo vya dola kwani alikuwa na woga kutokana na kutokuwa na rekodi ya yoyote ya matukio ya uhalifu.

“Nisingeweza kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana na ya jeshi na hayakuwa sare rasmi za jeshi hilo, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo,” alisema nyota huyo aliyetajwa kuwania tuzo za MTV EMA zinazotarajiwa kufanyika Novemba 9 mjini Glasgow, Scotland.

Diamond alisema si kweli kwamba alichukuliwa dhamana na Chifu Kiumbe, ila ukweli ni kwamba alisindikizwa na mdau huyo wa sanaa nchini kama kaka yake kutokana na woga aliokuwa nao, lakini hakushikiliwa na kutakiwa dhamana yoyote.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi mbona niliona nap kina Nay na chege walivaa mbona sijasikia kama wamekamatwa?

    ReplyDelete
  2. walipewa onyo, wakatii !

    ReplyDelete

Top Post Ad