Jinsi Bilionea Wa Madawa ya Kulevya Bongo 'Chonji' Alivyokamatwa Huko Magomeni..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
HII kali! Kukamatwa na polisi kwa mfanyabiashara bilionea jijini Dar, Mharami Mohamed Abadallah ‘Chonji’ (44) (aliyezungushiwa duara) hivi karibuni akidaiwa kukutwa na madawa ya kulevya ‘unga’ aina ya heroin yenye thamani ya shilingi 300,000,000 kumelitikisa Jiji la Dar, Uwazi limefuatalia hatua kwa hatua.


Mtikisiko huo umekuja kufuatia maeneo mbalimbali ya jiji kumzungumzia kwa namna mbili, wengine wakifurahia wengine wakisikitika, hasa wanawake wanaoishi maeneo ya Magomeni Kondoa, Dar  ambako mfanyabiashara huyo ndiko kwenye makazi yake.

AKUTWA NA SARE ZA JESHI
Tukio lingine liliwatikisa polisi wenyewe kufuatia upekuzi wa kina nyumbani kwake ambapo walimkuta pia na sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zinazofanana kwa sehemu kubwa na zile zilizomwingiza Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwenye mzozo na jeshi hilo.

AKUTWA NA BUTI
Mbali na sare kwa maana ya mavazi, pia mtuhumiwa huyo alikutwa na viatu vya jeshi hilo maarufu kwa jina la buti nazo zikiwa mpya!

BASTOLA NAYO
Katika hali iliyowatia shaka zaidi askari ni pale Mharami alipopekuliwa zaidi na kukutwa na bastola ambayo jeshi la polisi halijaitolea ufafanuzi inaitwaje na ilitengenezwa nchi gani!

VITU VINGINE
Vitu vingine vilivyokutwa kwa mtuhumiwa huyo ni jiko dogo la gesi na gundi ya plastiki, vyote vinaaminiwa kutumika wakati wa kutengeneza kete za unga tayari kwa kusafirisha.
Mharami, mbali na ishu zote hizo, anadaiwa kumiliki maghorofa mawili, Tandale na Magomeni Kondoa jijini Dar, mabasi na magari manne ya kutembelea mwenyewe.

ALIKAMATWA KAMA KWENYE SINEMA
Mharami alikamatwa Oktoba 21, saa saba usiku nyumbani kwake, Magomeni Kondoa lakini kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo linasemekana kufananishwa na inavyokuwa kwenye sinema za Kimarekani.

Inadaiwa kuwa, awali askari zaidi ya 20 kutoka Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania walifika kwenye nyumba hiyo kufuatia kutonywa kuwepo kwa unga na kumbana mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake wanne ndani.Ikadaiwa kuwa, mtuhumiwa na wenzake walijaribu kutoroka  walipogongewa mlango na kukataa kufungua.

Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba baada ya Mharami kugoma kufungua mlango polisi walilipua mabomu ya machozi na kupiga risasi hewani ndipo alipokubali kufungua huku wenzake wakiwa wametawanyika kwa kupanda juu ya paa la nyumba ndogo kisha kupanda kwenye jumba  la ghorofa tano ambalo analimiliki mtuhumiwa huyo.

WATU WATOKA NA NGUO ZA KULALIA
Ikazidi kudaiwa kuwa, kufuatia milio ya mabomu na risasi, baadhi ya wakazi wa eneo hilo walitoka kushuhudia wengine wakiwa na nguo za kulalia tu.

ALICHOSEMA MJUMBE, MTENDAJI
Mjumbe wa Nyumba Kumi Shina Na. 2, Mwanamtama Sasamalo alipohojiwa na Uwazi alikiri kutokea kwa tukio hilo la kamatakamata ya askari kwa Mharami na wenzake.

“Ilikuwa kama saa saba usiku, polisi walinigongea nyumbani kwangu wakasema wanataka kumkamata mhalifu, tukafuatana hadi nyumbani kwa Mharami. Niliwakuta polisi wengine wakiwa na silaha wameizingira nyumba yake, nilichokishuhudia ni ungaunga ukiwa umesambaa chini, wahusika walikamatwa na kufuatana na askari,” alisema mjumbe huyo.

Naye Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Makanya, Kata ya Ndugubi, Alex Mwisongo alipoulizwa alisema tukio hilo lipo, akaongeza kuwa vijana wengi wamekuwa mateja katika mtaa wake na wameathiriwa na unga ambao hajajua unakotoka.

KAMANDA NZOWA SASA
Naye Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alipoulizwa na waandishi wetu ofisini kwake alisema Mharami alishawahi kukamatwa mwaka 2009 kwa kuhusishwa na madawa ya kulevya ambapo alikuwa chini ya uangalizi wa polisi na mahakama.

Aliwataja waliokamatwa naye safari hii kuwa ni Rehani Mursal (45), mkazi wa Mburahati (Dar), Abdul Abdallah (37), mkazi wa Mbezi Shamba (Dar), Tanaka Mwakasaburi (35), mkazi wa Magomeni- Makanya (Dar) na Maliki Zuberi (29), mkazi wa Magomeni Mwembechai (Dar).

Watuhumiwa hao wote walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar, wiki iliyopita chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi na askari magereza mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda na walipelekwa mahabusu ya Gereza la Keko, wanatarajiwa kurudi mahakamani Novemba 6, mwaka huu.
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HUYU CHONJI NA NSEMBO NI MARAFIKI SANA NA WOTE NDIO BIASHARA YAO YA UNGA, SHAMIMU MAMA WA BLOG 8020 FASHION NA YEYE KAANZA HIYO BIASHARA, BISHA KAMA NAKUSINGIZIA NZOWA FANYA KAZI YAKO BABU

    ReplyDelete
  2. CHONJI NDIO ALIYEMPA DIAMOND ZILE NGUO ZA JESHI WANAZO NYINGI SANA. DIAMOND NDIO WANAMTUMIA KUPELEKA MADAWA YA KULEVYA NJE YA NCHI, SIO KUIMBA TU DIAMOND AWE NA HELA ZOTE HIZO, KAMA NI KUIMBA KUPATA HELA ANGEPATA DOKTA REMMY MAANA ALIKUWA NA MKE MZUNGU

    ReplyDelete
  3. KWELI DIAMOND SAFARI ZAKE NYINGI NI MIPANGO YA UNGA, MZIKI NI KAMA MWAVULI TU. YEYE NI CHAMBO TULISHAMJUA

    ReplyDelete
  4. Mbona Rummyshael Shoo akamatwi?ni muuza madawa pia,ebu mfuatilieni @rummy255 insta mumuone anavyojishaua Kama DEMU hela yenyewe ni ya kuumiza watoto Wa watu,nzowa kamata mwiziiiiii ,

    ReplyDelete
  5. Okayyyy sasa napata pichaaa rummy Na mume Wa shamimu ni marafikiiiiii,nawaonaga pamoja,rummy anabadilisha magari Kama nguo nasikia akikutia tu sahau daladala anakununulia Gari

    ReplyDelete
  6. IDDY AZANI MBUNGE NA YEYE MBONA WANAMUACHA AU KWA VILE MWANA CCM MWENZAO? WAKINA AUNT EZEKIEL, WEMA SEPETU,JACKLINE WOLPER, MASOGANGE NA WENGINE WENGI TUNAWAJUA MNAWAACHA? KWANZA HATA TUKIWATAJA HAMUWAFANYI KITU MAZAFANTAZIIIIIIIIIIIII

    ReplyDelete
  7. SINTA NA YEYE KASHAFUNDISHWA HIYO BIASHARA NA MRS SEMBE SHAMIMU 8020 FASHION

    ReplyDelete

Top Post Ad