google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Kizimbani Kwa Kucheza Ngoma ya Kigodoro Wakiwa Uchi | UDAKU SPECIAL

Kizimbani Kwa Kucheza Ngoma ya Kigodoro Wakiwa Uchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAKAZI wa eneo la Masasi Mbovu katika Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara wamefikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani kujibu shitaka linalowakabili la kucheza wakiwa watupu kwa staili ya vigodoro kwenye sherehe ya ndoa.

Jemima Jordan (22), Aziza Chukachuka (20), Anna Yohana (25) pamoja na mtoto mwenye umri wa miaka 17 (Jina linahifadhiwa) walifikishwa mahakamani hapo juzi mbele ya Hakimu Halfani Ulaya na kusomewa shitaka na mwendesha mashtaka Iddi Athumani.

Athumani alidai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Septemba 30 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika eneo la Masasi Mbovu huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa linalokwenda kinyume na maadili ya kitanzania.

Alidai kwa kuwa shauri hilo linamshirikisha mtoto aliye chini ya miaka 18, ni vyema Mahakama ikaahirisha kesi hiyo ili kupisha upelelezi wa kina kuhusu shitaka hilo linalowakabili washtakiwa hao.

Hakimu Ulaya alikubaliana na ombi la mwendesha mashtaka na aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 30 mwaka huu itakapotajwa tena. Watuhumiwa hao walio nje kwa dhamana hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi kuna sheria ya maadili ya kitanzania? Iwapo sheria hiyo ipo, nadhani itakuwa ni vizuri itumike kwa mafisadi kwani siamnini kuwa ufisadi ni sehemu y maadili y kitanzania.

    Halafu maadali ya Kitanzania yameandikwa katika kitabu gani cha sheria?

    ReplyDelete

Top Post Ad