Taarifa Kuhusu Madaktari Watanzania Waliokwenda Kukabiliana na Ebola Afrika Magharibi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Unaposikia ugonjwa wa ebola, ni sawa na kusikia sauti ya mauti. Ugonjwa huu ambao unaliandama eneo la Afrika Magharibi umesababisha vifo vya maelfu ya watu na hata kuuingiza ulimwengu kwenye wasiwasi mkubwa.

Ugonjwa huu huweza kuambukizwa kwa kugusana tu, kwa kuwa virusi vinavyoeneza maradhi haya huishi katika majimaji ya mwilini yakiwamo mate, damu na hata jasho.

Pamoja na hatari ya ebola, lakini Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa maagizo ya Rais Jakaya Kikwete, ilituma timu ya madaktari bingwa watano kwenda katika nchi zilizoathirika na ebola ili kusaidia.

Madaktari hao ni Justin Maeda ambaye ni mganga mkuu wa Hospitali ya Mvomero, mkoani Morogoro, Theopili Malibicha kutoka Hospitali ya Mkoa wa Lindi, Godbles Lucas, wizarani, Erild Temba kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na Saasita Ramadhan kutoka Chunya, Mbeya.

Madaktari wote hawatakwenda eneo moja. Dk Maeda, Malibicha na Lucas wataenda Liberia, wakati Temba na Ramadhan wakienda Sierra Leone.

Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja anasema madaktari hao wamekwenda katika nchi hizo ili kusaidia kutoa huduma za afya na kupata ujuzi.

“Kitendo cha madaktari hawa kwenda katika nchi zenye ebola si cha kutisha kama wengi wanavyodhani kwani ni sawa na askari anayekwenda vitani,” anasema.

Anasema mwanajeshi hupata mafunzo akijua siku yeyote anaweza kupata wajibu wa kwenda kupigana kwenye vita ambako kuna kufa au kupona.
Credits:Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tuwaombee,Mungu wetu ni mwema awaepushe na madhara.

    ReplyDelete
  2. tunawapongeza kwa ujasiri wao lakini chondechonde tunaomba wakirudi wachunguzwe kwa umakini, isije kuwa kama wale wamarekani waliongia kwao bila kuchunguzwa mfano new york hivi karibuni na kujichanganya na watu, kule marekani wanatiba bora na utaratibu mzuri wa kumcontain mgonjwa wa ebola, ikitokea hapa kwetu, itakuwa ni majanga tu!! eeh Mungu tuepushe na hilo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli kabisa,ni kuomba Mungu atuepushe na hilo
      na hivi tumezoea kubanana kwenye madaladala,makanisani/misikitini shart kwa salamu za kushikana mikono.Mungu wetu tuangalie kwa jicho lako la huruma.

      Delete
  3. Hivi hao madaktari watasaidia nini ikiwa ugonjwa wenyewe hauna tiba? MAJANGA

    ReplyDelete
  4. ni ujasir kwenda kwenye izo nchi zilizoathiriwa sana na ebola,, ila sizani kama ni jambo zuri kuwapeleka madaktari wetu sehemu za hatari ivyo kwani ni sawa na kutaka kuwapoteza,,




    ReplyDelete
  5. jamani hakuna short course ya udaktari? posho

    ReplyDelete

Top Post Ad