Vita Nzito Mbili Kubwa Hapa Mjini: Ali Kiba Vs Diamond na Clouds FM na Times FM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Erick Evarist, Musa Mateja na Chande Abdallah
MTIFUANO! Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 limepita lakini nyuma yake limeacha vita nzito iliyowahusisha mafahari wawili, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba huku waandaaji wa tamasha hilo, Clouds FM wakisigana na Times FM kumgombea msanii wa Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’, Risasi Mchanganyiko linakupa mchongo kamili.


TIFU LILIVYOKUWA
Kwenye shoo hiyo iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Ali Kiba (Team Kiba), walipiga kelele za ‘buuu’ pale alipopanda Diamond kutumbuiza ili kumharibia.

CHANZO CHANENA
Chanzo makini kimedai kuwa, vurugu hizo hazikutokea kwa bahati mbaya bali zilipangwa na wafuasi wa Kiba ambapo inasemekana ziliandaliwa gari aina ya Toyota-Costa zipatazo 25 zilizokuwa zimejaa watu na kwenda kuwamwaga viwanjani hapo kwa shughuli mbili muhimu; kuzomea na kuhamasisha wengine wazomee pindi Diamond atakapopanda jukwaani.

“Ishu ilipangwa, Team Kiba waliibuka na Costa kama 25 hivi, wakajipanga katika maeneo tofauti ya uwanja huo lakini zaidi walikaa karibu na jukwaa ili kuweza kutimiza vizuri azma yao ya kuharibu pindi Diamond atakapokuwa akitumbuiza,” kilidai chanzo hicho.

WALIFANIKIWA?
Kwa namna moja mashabiki hao walionekana kufanikiwa kwani waliweza kuwashawishi watu wengi wazomee kiasi cha kumfanya Diamond ashtukie  na kuamua kutamka hadharani: “Jamani kuna uhuni unaendelea hapa.”


TEAM DIAMOND WACHARUKA
Madai yanasema mara baada ya Team Kiba kufanya vurugu hizo na kufanikiwa, baadhi ya mashabiki ambao waliaminika ni wa Diamond (Team Diamond), walicharuka na kusema hawakubaliani na uhuni huo ambao umefanywa hivyo watahakikisha wanapambana kulipiza kisasi kwa namna yoyote ile.
“Hatukubali, wao si walijipanga hapa kumharibia Diamond, sasa na sisi tutahakikisha tunalipiza kisasi kwa namna yoyote,” walisikika wakisema mashabiki wa Diamond.

TALE AKIRI KUSIKIA
Paparazi wetu aliwatafuta Diamond na Kiba ili kujua wanazungumziaje vurugu hizo. Baada ya kumtafuta Diamond bila mafanikio, alipatikana meneja wake, Hamis Taletale ‘Bab Tale’ ambaye alikiri kuwepo kwa maandalizi ya zomeazomea ambayo yalikuwa na lengo ya kumharibia msanii wake.

“Hizi kwetu tumezichukulia kama changamoto, tulisikia kwamba kuna watu wamelipwa kwa ajili ya kufanya fujo lakini hatukujali sana kwani lengo letu si kugombana na mtu, sisi tunafanya muziki mzuri ambao ndoto zetu ni kuufikisha katika levo za Kimataifa,” alisema Bab Tale.

KIBA ANAHUSIKA?
Alipotafutwa Kiba kuzungumzia suala hilo alikataa kuhusika nalo na kudai halina ukweli wowote kwani si rahisi kuwalipa pesa mashabiki wengi kiasi kile waliojitokeza uwanjani.
“Hiyo si kweli ni uzushi tu, sasa mimi nitawalipa nini hao mashabiki wote waweze kumzomea huyo Diamond? Siyo rahisi. Kwanza mimi nifanye hivyo ili iweje? Mimi si mtu wa kushindana na Diamond hata siku moja, nafanya muziki wangu, mashabiki wanauelewa, nashukuru Mungu kwa hilo,” alisema Kiba.

CLOUDS FM VS TIMES FM
Kwa upande mwingine, vita nzito ilizidi kutokota kupitia tamasha hilo baada ya msanii Davido kupanda jukwaani na kutumbuiza ilhali akiwa amewekewa pingamizi la kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) sambamba na zuio la Mahakama ya Kisutu lililowekwa na Redio Times FM waliodai kuwa na mkataba wa kufanya shoo na msanii huyo Novemba, mwaka huu Bongo.

TIMES WANASEMAJE?
Mkurugenzi wa Redio Times FM, Rehure Nyaulawa alipotafutwa kwa simu kuhusiana na suala hilo alisema mahakama ilishaweka pingamizi, anashangaa kuona msanii huyo alipanda jukwaani lakini akasema hawezi kukaa kimya, atakwenda mbele zaidi ili haki itendeke.

CLOUDS JE?
Kwa upande wao, Clouds walipotafutwa hawakupatikana hewani lakini kimsingi na wao wana hoja zao ambazo zitabainika pindi kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.

Hata hivyo, kuna madai kwamba, zuio la Davido kutopanda jukwaani Leaders Club lilipelekwa na mahakama kwa Clouds Media Group wakati Tamasha la Fiesta linaandaliwa na Kampuni ya Primetime Promotion, kwa hiyo barua hiyo ilikuwa ‘missing in action’.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad