Wema Sepetu Sasa Ajuta Kuwa Maarufu, Asema Umaarufu Unamtesa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

‘BEAUTIFUL Onyinye’, WEMA Isaack Sepetu ‘Madame’ ametoa ya moyoni na kufichua kwamba maisha yake ya umaarufu anayoishi yanamtesa kwa asilimia 40.

Pamoja na mateso hayo, staa huyo wa filamu alisema anafurahia maisha yake kama mtu maarufu ikiwamo na kuandikwa na vyombo vya habari mara kwa mara.

“Kuna wakati najutia kuwa maarufu kwa asilimia kama 40 hivi lakini nashukuru kwani kwa asilimia 60 nayafurahia maisha yangu.

“Ukiwa nyota kuna changamoto nyingi sana, kuna wakati mtu anaweza kukuandika habari inayokufanya ushindwe hata kutoka nje na kubaki ndani tu,”alisema.

Wema alisema kuna wakati huwa anatamani asingekuwa maarufu kwani akifanya kitu kidogo hata kama ni cha kawaida lakini hupokelewa kama habari kubwa na kuongelewa sana.

“Lakini katika maisha kama haya sina cha kufanya japo kuna mambo ambayo huniumiza na najitahidi sana kuvumilia,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmh,asilimia 60 kwa 40?sijui ni mwandishi unajichanganya au vipi,sio kwamba haunyimwi usingizi kwa kuwa wanaoandika wanatumia simu za
    Huawei na Tecno?

    ReplyDelete

Top Post Ad