Hatimaye Diamond Aongelea Kuhusu Kuachana na Wema na Mahusiano yake na Zari Boss Lady

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jana Nov 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.
Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:

Adam Mchomvu :”…Nataka kujua ile vibe ya Fiesta that day, story zilikuja ooh Diamond kazomewa.. kazomewa kazomewa..na vitu kama vile, sijapata chance ya kukusikia wewe una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na that situation..?“

Diamond :- “… Siku zile kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki ushakuwa kama sio fani tena, ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie hivyo wewe mwenyewe kama msanii ujue una control vipi kwa sababu sio mara ya kwanza vitu kama hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa mpaka na mayai viza kabisa.. Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni kawaida…“

B 12  :-“…Kwa hiyo ukweli uko wapi kati yako wewe na Wema Sepetu?...”

Diamond  :- “…Kuna vitu vitu fulani nadhani kuvizungumza sio vizuri… Lakini ikifikia kuvizungumzia vinazungumziwa… Uzuri wa mahusiano yetu ni kwamba kila mtu anafahamu… Haijafikia kuweka wazi ndio maana ninapoulizwa inakuwa ni swali gumu kulijibu.. “

B 12 :- “.. Ni gumu kwa upande wako lakini yeye yuko tayari kuzungumza kwamba it’s over kati yangu mi’ na Diamond…“

Diamond  :- “… Sijui…“

B 12  :- “...Hii ngoma kama umemzungumzia yeye direct hivi… watu wamekuza akili zao zikaenda mbali zaidi kimawazo lakini, kwamba inawezekana ile singo umemwimbia yeye hivi kwamba bado unamzimia japokuwa bado kama kakutosa hivi…“

Diamond  : “.. Waswahili wanasema ‘A’ na ‘B’ yote majibu, halafu ukisikiliza ile nyimbo kama kweli mtu mwenye ufahamu wako, kweli kabisa hauwezi kuwa na maswali mengi …“
Kuhusiana na mahusiano yake na Zari the Boss Lady, Diamond amejibu hivi:

Diamond  :- “.. Zari ni rafiki yangu tu, alipokuja hapa mimi ndio nilikuwa mwenyeji wake Tanzania na kama mimi ndiyo mwenyeji sikutaka kuleta roho za kibaguzi, unajua hata alipokuja Davido pia ilibidi awe na mimi karibu ili hata kesho na kesho kutwa  mimi nikiwa Nigeria basi Davido anipokee hivyo hivyo…“

Iko hapa full Interview ya Diamond kwenye XXL, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad