Jibu la Diamond la Kwanini Ametumia Tena Wazungu Kwenye Video Mpya ‘Ntampata Wapi’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya Diamond kuachia video ya ‘Ntampata wapi’ iliyofanyika Afrika Kusini, amekutana tena na maswali aliyokutana nayo kipindi alipoachia video ya ‘Mdogo mdogo’, ya kwanini amewatumia zaidi wazungu kwenye video ya wimbo wake wenye ladha ya Kiafrika. 

Hili ndio jibu la Platnumz baada ya kuulizwa swali hilo kwenye kipindi cha Power Jamz kupitia East Africa Radio:

Kuna kitu kimoja, waache ubaguzi inategemea na script ya nyimbo inavyozungumza, script inataka kitu gani, script yangu ya mdogo mdogo ilikuwa inazungumza kwamba mapenzi hayachagui, ndio maana kulikuwa na familia ya kizungu mimi familia ya kiafrika, mimi namtaka demu wa kizungu lakini wazazi wake hawataki, kwahiyo ndo maana mwisho tukaandika mapenzi hayachagui”.

Na naamini hicho kitu ndo kilisababisha kufanya hata Marekani ikashinda tuzo, video ya Aye haikushinda ikashinda video ya Mdogo mdogo kama video ya Afrika kwasbaabu concept yenyewe ilikuwa inazungumza vizuri, wazungu wenyewe wameona kama aah hii kweli lakini tuache maswala ya kibaguzi”.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad