Charles Mihayo,Mtanzania aliyewauwa watoto wake wawili Australia ahukumiwa kifungo cha maisha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Charles Mihayo, (36) mzaliwa wa Tanzania ambaye mwezi April, 20, 2014 aliwauwa watoto wake wawili wadogo wa kike nyumbani kwake huko Melbourne, Australia (Ingia hapa) amehukumiwa kifungo cha maisha.

Inadaiwa kuwa baada ya kuachwa na mke wake, hasira zilimfanya bwana Mihayo kuamua kufanya ukatili wa kukatisha uhai wa watoto wake mwenyewe Savannah (4) na Indianna (3), ili tu kumuumiza mke wake kama njia ya kumlipizia kisasi. Inadaiwa kuwa aliwauwa kwa kuwakandamiza na mto baada ya kucheza nao.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa siku mauaji hayo yalipofanyika, mama wa watoto hao aliwapeleka kwa baba yao bwana Mihayo. Baada ya kuwafikisha baba yao aliwafanyia shopping ya nguo na viatu vipya.

Kabla ya kutenda ukatili huo kwa damu yake mwenyewe, Mihayo aliwarekodi video wakicheza muziki huku akicheza nao. Na katika video ambayo polisi baadae waliiona, alisikika akiwaambia binti zake wamuoneshe mama yao nguo mpya alizowanunulia, na walifanya hivyo na kisha mwanaume huyo akakaa mbele ya camera na kusema “tutamuonesha mama kitu kingine dakika kumi zijazo”, na kuendelea kucheza nao hadi alipowakandamiza na mto (pillow) hadi kufa.

Baada ya kufanya mauaji Mihayo mwenyewe aliwapigia simu polisi ambao baada ya kufika nyumbani kwake wakiwa mlangoni aliwaambia , “Tayari, nimewaua. Nimewaua watoto wangu. Inabidi mumuulize huyu [mama yao] sababu.”

Polisi waliwakuta watoto hao wakiwa tayari wamefariki huku wakiwa wamevalishwa nguo na viatu vipya ambavyo walinunuliwa na baba yao siku hiyo.

Licha ya kuhukumiwa kifungu cha maisha, Charles Mihayo anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 31 kabla ya kupata haki ya kupewa msamaha.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inasikitisha Sana, watanzania tuwe na hofu ya Mungu, shetani hatatushinda.

    ReplyDelete
  2. hizi ndio tabia za wanaume wengi wanapoachana na mwanamke huwa wanataka kumkomesha.
    mtu kaishaachana na wewe kakuacha huru ufanye utakacho unamtafutia sababu za kumkomesha ili?
    haya sasa kajikomesha mwenyewe.

    ReplyDelete
  3. MJINGA SANA WEWE SASA UMEPATA FAIDA GANI!! UMEMUUMIZA MAMA YAO??? UNAJIDANGANYA BINADAMU TUMEUMBWA KUSAHAU ATAZAA WENGINE WATAMLIWAZA JEE WEWE???

    ReplyDelete

Top Post Ad