URAIS:January Makamba awaita wasanii wa Bongo Movie Serena Hotel leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katika hali ya kushangaza, naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba amewaandalia chakula cha jioni wasanii wa Bongo Movie leo jumatatu usiku Serena Hotel, imefahamika. Mualiko huo unaoratibiwa kwa karibu na msanii JB, unatarajiwa kuambatana na maombi ya bwana Makamba kwa wasanii wamuunge mkono katika ndoto yake ya Urais 2015. Kila msanii atakayeshiriki ameandaliwa bahasha maalum ya pesa za Xmas na Mwaka Mpya 2015. 

Baadhi ya wasanii wanatajwa kutumika kuvuta pesa kutoka kwa wagombea zaidi ya mmoja, wakitumia mchakato wa Urais kama mwanya wa kujipatia pesa za bila jasho. JB anatajwa pia kuwa mtu wa karibu wa Edward Lowassa, hivyo kuzua sintofahamu juu ya ushiriki wake katika kuwashawishi wasanii wenzie wa Bongo Movie kukutana na kumuunga mkono January Makamba. 
Hongereni wasanii kwa kutumia vema fursa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukipata kitumie, ukikosa kijutie, wakipata uongozi hawatawajua tena, bora mchukue chenu mapema kwa yeyote atakaye jipendekeza.........

    ReplyDelete

Top Post Ad