Uzuri na Mapungufu yaliyopo kwenye Video Mpya ya Ally kiba (Mwana Dsm)

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii mwenye jina kubwa hapa bongo ally kibba Jana 19.12.2014 ameachia video iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wake ya Mwana dsm nimeona tujadili Uzuri na mapungufu yake ili aweze kujirekebisha kwenye video zinazofuata.

Uzuri :
Video ina Quality moja Poa sana na pili Nimependa jinsi Walivyokuwa Wanacheza Ali Kiba na Wacheza Show wake.

Mapungufu
Video hii itatamba sana hapa nchini Tz labda na east Africa tu ila itapata shida sana kutamba katika nchi zisizojua kiswahili kwa sababu video ya wimbo haielezei uhalisia wa maudhui wa nyimbo husika.

Kiufupi mtu asiyejua kiswahili hawezi kujua wimbo unazungumzia nini.

Kwa wale ambao hamjanielewa,wewe mtanzania unayejua kiswahili jaribu kuangalia video wakati sound ipo silent kama utaelewa video inazungumzia nini.

Halafu angalia video ya diamond ya NITAMPATA WAPI bila sauti.

Wewe mwenzangu umeona mapungufu gani?

Angalia Video Hapa:


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli kabisa. Nimejaribu kuiangalia hii video mara tano sijaelewa lolote kwanza watu wengi mno, ukiona video inalundo la watu vile kuwa nzuri ni nadra sana, video nzuri inapendeza watu wawastani na classic. Sipo team Diamond wala team Kiba ila bado kwakweli, huwezi kuipambanisha hii video ya mwanadar salaam na ntampata wapi, ni vitu viwili tofauti. Ni hayo tu, kiba bado anatakiwa ajipange sana, amekurupuka inshort.

    ReplyDelete
  2. kachemka..................=))

    ReplyDelete
  3. Kiba pa1 na management yake kwa kweli hawapo makini hata kdogo yani kwa mwendo huu hawezi hata kdogo kumsogelea Diamond

    ReplyDelete

Top Post Ad