Aibu Kubwa: Mtumishi wa Mungu Afumaniwa live na Mke wa Mtu Wakibanjuka Nyumbani Kwa Mwanamke

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Risasi Mchanganyiko
Ohoo, ama kweli dunia imekwisha! Mtumishi wa Mungu (Muinjilisti) ambaye kipindi chake cha dini kinarushwa katika kituo kimoja maarufu cha televisheni Bongo (Jina tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la Fredrick Kishindo ‘Badoo’ hivi karibuni alipata aibu ya kufungulia mwaka 2015 baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani, Risasi lina mkanda nzima.

Mtumishi Fredrick Kishindo ‘Badoo’ Akijitete 

Ilikuwaje?
Awali chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Januari 11, mwaka huu Muinjilisti huyo anayesifika kwa kuhubiri watu waache dhambi alionekana akinyata kuingia kwenye nyumba ya mke wa mtu huyo iliyopo Sinza jijini Dar huku kukiwa na taarifa kuwa, mume wa mwanamke huyo alikuwa safarini.

Wifi mtu atonywa
Ikaelezwa kuwa, kufuatia mazingira hayo wifi wa mwanamke huyo alitonywa juu ya taarifa za Badoo kuingia kwenye nyumba ya kaka yake, maelezo yaliyomshitua hivyo kulazimika kuelekea eneo la tukio.
Baada ya wifi mtu huyo kufika nyumbani kwa kaka yake na kuhakikishiwa kuwa Badoo yuko ndani, aliuliza namna ya kuwapata makamanda wa Operesheni Fichua Maovu ya Global Publishers ‘OFM’ ambapo mmoja wa majirani alimpatia namba ya simu, akawapigia.

Polisi washirikishwa
Katika kuhakikisha usalama katika eneo hilo, wifi huyo pia aliwasimamisha polisi waliokuwa doria na kuwatonya juu ya uzinzi unaofanyika nyumbani kwa kaka yake na kwa kuwa kazi ya askari ni kulinda raia na mali zao, walitoa ushirikiano.

OFM watinga eneo la tukio
Baada ya makamanda wa OFM kupigiwa simu na kunyetishiwa juu ya uwepo wa Muinjilisti huyo chumbani na mke wa mtu, kwa kutumia pikipiki zao ziendazo kasi walianza safari na baada ya dakika chache walikuwa wamefika kwenye nyumba hiyo na kuwakuta polisi.

Muinjilisti, mke wa mtu live
Polisi wakiwa na OFM waliongozwa na wifi mtu huyo hadi kwenye chumba ambacho madhambi yalikuwa yakitendeka, walipoingia walikuta mke wa mtu na mtumishi huyo wa Mungu wakiwa kama walivyozaliwa.

Aibu iliyoje!
Baada ya kuona ‘picha imeungua’, mtumishi huyo alisikika akisema kuwa amepata aibu ambayo hakuitarajia huku akiomba asipigwe picha wala kufanyiwa kitendo kibaya bali apewe nafasi ya kujitetea.
Aidha mke wa mtu aliyenaswa akimsaliti mumewe alionekana kutahayari na aliishiwa nguvu zaidi alipomuona wifi yake aliyekuwa amefura ile mbaya.


Utetezi wa mtumishi wa Mungu
Kufuatia kunaswa huko, Badoo alijitetea kwa kujichanganya, awali alisema aliitwa na mwanamke huyo kwa ajili ya kuongea mambo ya biashara na kwamba eti walivua nguo kutokana na hali ya joto iliyokwemo chumbani humo.

Kana kwamba alihisi kajichanganya, Muinjilisti huyo aligeuza utetezi na kusema aliingia majaribuni baada ya kushawishiwa na ibilisi kisha mwanamke huyo hakumwambia kuwa ana mume.

Bofya hapa usikie utetezi wake
“Jamani naomba mnisamehe, si kosa langu bali ibilisi ndiye aliyenishawishi na huyu mwanamke hakuniambia kama ana mume. Hapa aliniita kwa ajili ya biashara flani.
“OFM nawajueni lakini niko chini ya miguu yenu, naomba msiitoe habari hii gazetini kesho n’tawaletea chochote pale ofisini kwenu, si ni pale Bamaga ee, napajua sana pale”.


OFM ni mwiko kupokea rushwa
Licha ya utetezi wake huo, makamanda wa OFM walisimamia weledi wa kazi yao na kumweleza kuwa, rushwa kwao ni mwiko hivyo kama atafika ofisini kwao iwe ni kwa ajili ya maelezo zaidi ya kwa nini amevunja moja ya amri kumi za Mungu.

Mpaka OFM wanaondoka eneo la tukio, mke wa mtu huyo alikuwa akiendelea kumuomba msamaha wifi yake huku Muinjilisti naye akijaribu kutuliza mambo yasifike mbali akidai kuwa, mke wake, ndugu na marafiki wakijua ataaibika.

Chanzo:Global Publishers
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mmmmmmmmmmm jamani dunia hadaa ulimwengu shujaa

    ReplyDelete
  2. Mh kwakweli mmefanya vibaya sana sababu mmedhulumu nafsi ya mtu. Ila mimi sidhani kama ni busara kufumania mke wa kaka yako na kuanza kuita mitandao au magazeti unafanya ivyo ili iweje? nasema hivyo sababu aibu ya mke wa kaka yako ni aibu ya kaka yako pia na pia huyo mama anawatoto huoni kama unaumiza akili za watoto maana watasoma wataona upuuzi wa mama yao lakini haita isha hapo tu itawaathiri kisaikologia. Halafu huyo kaka yako anajisikiaje maana sisi wasomaji tusio mfahamu inaishia hapo lakini wale wanao mfahamu je? usifikiri watamuonea huruma aslilimia kubwa watamcheka maana binadamu tulivyo wataanza mh huyu itakuwa anakasoro mbona mke wake anatoka nje ya ndoa. Hao ni mwili mmoja aibu ya mmoja ni aibu ya wote, haya wewe umepata faida gani maana hata Mungu hapendi fumanizi la aina hiyo unavizia ili iweje, sawa kaka yako ataoa mke mwingine unawaweka watoto wao upande gani ndo mwanzo wa panya road wakati dunia inahangaika kunusuru ndoa wewe ndo wakwanza kuvunja ndoa maana alichokiunganisha Mungu mwanadamu na asikitenganishe wewe ni nani ulimkanya? Na sasa mipicha ya kazi gani fumanianeni yamalizeni kiutu uzima . haya mara bado kaka yako anmsamehe mtaita tena hao wanaojiita OFM kupiga picha za kusamehe. Acha ujinga na ufikirie kwanza mimi binafsi naona ni ushamba fikiri kwa makini wenzako wanapata hela wewe unapata aibu na haitoki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. yy ni kioo cha jamii,ndo maana yuko published....mbn diamond akitolewa kweny magazeti haulalamiki?

      Delete
  3. kiukweli mmefanya kosa sana maana umedhulumu nafsi ya mtu.
    Ila wifi mtu naelewa kabisa unauchungu sana na kaka yako lakini sidhani kama ni busara kumfumania mke wa kaka yako na kupiga picha hadharani kiasi hiki kwasababu kuu zifuatazo: 1. huyu mama ni mke wa kaka yako aibu yake ni aibu ya kaka yako usifikiri umemkomoa wifi yako hata kaka yako maana wao ni mwili mmoja.
    2. Ana watoto usifikiri hawatakuja kuona upuuzi huu maana tabu ya mitandao hadi picha wataona, unawanyong'onyeza watoto unawaharibu kisaikologia hawapaswi kuona haya mambo.

    Mimi binafsi sipendi tabia ya kufumaniana na kuwekana mitandaoni hata kidogo ni ushamba uliopitiliza halafu unapata nini, je wakiendelea au wewe uliyefunania ukasamehe unafikiri watu watamcheka mkeo tu hata wewe wataanza kujiuliza maswali kwanini atoke nje unakasoro gani. sidhani kama ni sawa, mfumanie yamalizeni kiutuuzima na watoto wafanyaje ambao akili hazijakomaa, unamkomoa nani? unaumiza ambao hawana hatia watoto hata huyo kaka yako bado ni aibu kwake. fikiri sana ndo maana fumanizi la kuvizia hata Mungu hapendi sababu wakiachana unapata nini utalea wewe watoto ndo mwanzo wa kuwa na panya road mitaani, kaka ataoa mke mwingine watoto wanaachwa njia panda. Ni ujinga sana ninaweza nisieleweke lakini hakuna faida ya kutuwekea mafumanizi yenu mitandaoni zaidi ya hasara. UJINGA TU. Fumania maliza kimnyakinya hata kama unaona ndo mwisho wenu.

    ReplyDelete
  4. acheni ubwege mlitaka aendelee na tabia zake za kishenzi, mm naona poa tu

    ReplyDelete
  5. wifi amefanya vizuri sana amemuokoa kaka yake sana cos uyo mtumishi agendelea na tabia yake chafu. utanedaje nyumba ya mtu ameolewa mume wake ayupo unasema unaeda kuogea mambo ya biashara na biashara hiyo mpaka chumbani.aibu sana

    ReplyDelete
  6. Kwanza kabisa mambo ya ndoa wanayajua watu wawili ndani. Ni kweli huyo dada kafumaniwa, lakini je ni nini kilichopelekea mpaka akaamua kuisaliti ndoa yake? Je huyo Mume yeye ni mtulivu kwa kiasi gani. Mimi nina mashaka na hiyo ndoa kama ina amani. Nahisi moto unawaka katika nyumba yao. Hata huyo wifi hana upendo na kaka yake wala na huyo wifi yake.

    Binafsi naona angemuonya huyo wifi yake na kama angerudia tena hapo ndiyo lingekuwa suala lingine. Hivi kwa mfano huyo kaka mtu angempiga huyo mkewe na kumuua huyo wifi angepata faida gani? Huyo wifi yeye ni msafi hata awe wa kwanza kuhukumu?

    Mtumishi naye ni mwanadamu na Mungu alijua hiyo ndiyo maana kuna mistari isemayo kesheni mkiomba maana roho i radhi lakini mwili udhaifu. Na pia ee Mungu wangu yale ninayotaka kuyafanya siyafanyi bali nafanya yale nisiyoyapenda.

    Sitetei uovu uliotendeka ila sikubaliani na hatua zilizochukuliwa na huyo wifi mtu. Haya sasa endapo watarudiana, maana unaweza kuta kaka yake ndiye hajiwezi kwa mkewe wifi utakuwa katika hali gani.

    ACHENI KUVUNJA NDOA ZA WATU.

    ReplyDelete
  7. Bongo bwana ni shidaaa. wabongo waliowengi wanawaza ushirikina,kukata viungo vya albino,ndoa za wake wengi,ndoa za utototoni,kukeketa watoto wa kike,fumanizi na ujinga mwingine mwingi wakati nchi zingine watu wanawaza maendeleo kama ujenzi wa reli,kuboresha miundombinu na kadhalika.alafu bongo tunalalamika hakuna dawati,dawa,maji,miji isiopangwa na kutembeza bakuli la omba omba duniani kote

    ReplyDelete
  8. Watu wa namna hii ni wabaya sana kwa sababu huwa wanatumia neno la Mungu kudangaya watu atawambia mtumishi anakuja tunakuja kufanya maombi kumbe nyuma ni hawara yake.

    ReplyDelete
  9. Siku hizi watu wanaremba sana uovu.Zamani watu kama hawa walikuwa wanapigwa mawe mpaka wafe. Sasa wewe umeolewa halafu unakwenda kuzini halafu uliapa kwamba utakuwa mwaminifu mpaka kufa. kwani hapo amesha kufa? Halafu pia huyu anasema ni mtumishi inakuwaje wewe uwe mnafiki hivyo leo uje useme unaonewa? wapingwe mawe ili iwe fundisho kwa wengine.

    ReplyDelete

Top Post Ad