Mfahamu kwa undani Zarinah, mwanamke anayezima Nyota ya Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

JINA la Zari hivi sasa limekuwa jina maarufu katika masikio ya Watanzania, Afrika Mashariki na kwingineko hasa baada ya mwanadada huyo mfanyabiashara na mwanamuziki wa Uganda kuwa na urafiki na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassib Abdul maarufu kwa jina la usanii Diamond Platnum.
Zari The Lady Boss
Kwenye mitandao ya kijamii kama Tweeter, Facebook,Instagram na hata Whatsapp lazima utakutana na jina Zari akiunganishwa na Diamond na wengine wataunganisha na Wema Sepetu aliyewahi kuwa mpenzi wa Diamond.

Uhusiano kati ya Zari na Diamond umezua gumzo kila eneo Tanzania na Afrika Mashariki huku wakifananishwa na mastaa wa nje kama vile Kanye West na Kim Kardashian kwa namna wanavyofuatana wakati wote huku Diamond akionesha kila aina ya mbwembwe za kumjali mrembo huyo kutoka Kampala, Uganda.

Uhusiano wa Zari na Diamond umewafanya kuandamana kila sehemu hivi sasa. Wawili hao walianza kuonekana kuwa na ukaribu wa mahusiano tangu Diamond alipokwenda Afrika Kusini kwenye Tuzo za Channel O ambapo Diamond aliibuka na ushindi wa Tuzo tatu.

Baada ya Tuzo hizo, Zari alimualika Diamond kushiriki katika ‘pati’ maarufu ambayo mwanadada huyo huandaa kila mwaka nchini Uganda ambapo mwaka huu ilijulikana kama All White Ciroc Party.

Wawili hao baada ya sherehe hiyo, walifuatana ambapo Zari alimsindikiza Diamond nchini Rwanda na Burundi alipokwenda kutoa burudani nchini humo, na picha kusambazwa katika mitandao ya kijamii na kuwafanya wawili hao kuwa gumzo hivi sasa katika mitandao Tanzania na Afrika Mashariki.

Je, Zari ni nani hasa? Zarina Hassan Tlale.Maarufu kama Zari ni Mganda anayeishi Afrika Kusini.

Mrembo huyo ni mwanamuziki na mfanyabiashara. Ni mwanamke aliyefanikiwa na anayependa kuishi maisha ya kifahari. Anamiliki magari ya kifahari na yenye gharama kubwa kama Lamborghini Gallardo, BMW- 2006,Chrysler-2008, Audi Q7-2010 na Ranger Rover Sports .

Mwanadada huyo ni binti wa Halima Sultan Hassan na Nasur Hassan akiwa na asili ya damu mchanganyiko ikiwa ni pamoja na ya Kihindi , Toro, Somalia na Burundi kutoka mji wa Jinja, Uganda. Babu mzaa mama yake anatoka India na bibi yake ni kutoka Uganda. Babu yake mzaa baba ni kutoka Somalia na bibi yake mzaa baba anatoka Burundi.

Zari maarufu kama The Bosslady aliwahi kuolewa na mwanamume anayejulikana kwa jina la Ivan na kubarikiwa watoto watatu wa kiume Pinto, Didy na Quincy na anamiliki kampuni tatu.

Mwanadada huyu alizaliwa Septemba 23,1980. Zari amekulia katika mji wa Jinja katika nchi ya Afrika Mashariki inayojulikana kama Uganda.

Zari alisoma shule ya msingi, kisha kwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jinja ambapo alisoma kwa bidii kutimiza ndoto zake. Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, mwanadada huyo alihamia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala ambapo alikuwa akitoa burudani ya muziki katika maeneo ya starehe kabla ya kuhamia mjini London, Uingereza na kusomea Stashahada ya masuala ya urembo (cosmetology).

Historia yake kimuziki inaonesha Zari alianza kuimba akiwa na umri mdogo wakati akisoma shule ya msingi ambapo alikuwa akitoa burudani katika matamasha ya muziki yaliyokuwa yanaandaliwa na wafanyakazi wa shule,wakati wa hafla za mwishoni mwa mwaka na katika mashindano mengine ya jumuiya akiwakilisha shule yake.

Ingawa amekulia katika familia ya Kiislamu yenye wasichana sita na wavulana wawili, Zari hakuacha mapenzi yake kwenye muziki. Alianza muziki akiwa na umri mdogo na albamu yake ina nyimbo kali kama ‘Toloba’ na ‘Hotter Than Them’. Watu waliomvutia katika muziki ni Wasanii wa Marekani Arethal Franklin na Whitney Houston wakati akiwa sekondari.

Afrika waliomvutia akapenda muziki ni wanamuziki wa Afrika Kusini Brenda Fassie, Miriam Makeba, Lucky Dube na Malkia wa Muziki Afrika Kusini, Yvone Chaka Chaka. Alipojiunga na sekondari alijiunga na makundi ya dansi,drama na muziki jambo ambalo lilimsaidia kuchaguliwa kwa miaka miwili mfululizo la Muigizaji Bora.

Baada ya miaka miwili ya kufanya vizuri katika majukwaa na matamasha ya shule, alipumzika na kuhama kutoka Uganda kwenda London, Uingereza na kuendelea na masomo yake lakini bado mapenzi yake kwa muziki yakiwa mawazoni mwake. Zari kwa msaada wa familia, mashabiki na marafiki wa- naopenda mtindo wa muziki wake na kuamini anaweza aliamua kuchukua hatua mwaka 2007 wa kurekodi singo yake ya kwanza inayoitwa Oliwange (ikiwa na maana wewe ni wangu) .

Mwaka 2008 Zari alishinda Tuzo ya Channel O ya Video Bora ya Muziki ya Msanii Bora Afrika Mshariki. Hafla ya tuzo hizo ilifanyika Johannesburg, Afrika Kusini. Tangu hapo Zari ameendelea kutoa nyimbo zaidi za kuvutia, huku akitiwa moyo na mashabiki wake wakati huo.

Mwaka 2009 alipata Tuzo inayojulikana kama Diva ya mwaka katika kipengele cha Diaspora tangu hapo aliendelea kutengeneza muziki. Zari hivi sasa anaishi Afrika Kusini ambapo anamiliki maduka makubwa ya vipodozi na shule ya elimu ya juu mjini Pretoria wakati akiendelea kujijenga kimuziki.

Inaelezwa kuwa Zari na aliyekuwa mumewe Ivan wanamiliki Shule ya Brooklyn City ambayo ina kampasi sita Afrika Kusini, huku kila moja ikiwa na wanafunzi kati ya 800 hadi 2,100. Wanafunzi hao hupewa vyeti vya taifa wanapomaliza mwaka. Vile vile Zari amejenga hosteli iliyopo barabara ya Sir Apollo Kaggwa, Kampala na anamiliki nyumba kadhaa katika mji huo hasa eneo la Munyonyo, pamoja na duka kubwa la nguo Afrika Kusini.

Ingawa muziki wake haujafanya vizuri kama wanamuziki wengine wa Uganda akiwemo Jose Chameleone, Bebe Cool, Bobi Wine na Ragga Dee, Zari amekuwa akifurahia kwa mafanikio zaidi kwenye biashara na kutokana na hilo anasema lazima arudishe kwa jamii na hivyo kuamua kusaidia vituo na taasisi kadhaa zinazohitaji misaada kama Katalemwa Cheshire Home, Sanyu Babies’ Home pamoja na Gereza la Luzira.

Mfano mwaka 2013 kutokana na moyo wake wa kusaidia,kwa kutimiza hilo baada ya sherehe zake anazozifanya kila mwisho wa mwaka aliamua kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha M-Lisada kilichopo Nsambya siku moja kabla ya Sikukuu ya Krismasi, akifuatana na watoto wake Pinto, Didy na Quincy.

Alitoa zawadi maalum kwa watoto hao, ambapo Zari alishiriki kuandaa chakula cha Krismasi na kisha baadaye wanawake, sukari, biskuti, mchele na matoke. Mbali na masuala mengine yote, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali,watu wengi nchini Uganda wanakubaliana kuwa Zari ndio Mwanamke Mrembo zaidi nchini humo.

“Sitafuti umaarufu, wenyewe umaarufu ndio hunifuata,”aliwahi Zari kusema kupitia mtandao wa Red Pepper akikanusha habari za baadhi ya watu wanaodai kuwa anatafuta umaarufu kwa nguvu.

Habari zake kuandikwa katika mitandao ya kijamii pamoja na shughuli zake za uhisani zimesababisha wengi kudai kuwa anataka tu umaarufu, kujulikana na kuzungumziwa kila wakati.Hata hivyo akijibu madai hayo, Zari alisema umaarufu unamtafuta yeye na sio kwamba yeye anautafuta.

Quote of The Day:
'You've gotta dance like there's nobody watching,
Love like you'll never be hurt,
Sing like there's nobody listening,
And live like it's heaven on earth.'
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

21 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nakubaliana na Zari,na ni Kweli kabisa umaarufu ndio unamfuata.
    Ona hata wewe mwandishi umetafuta cha kupost kuhusu Zari ili mradi tu
    siku isiishe bila kumuandika Zari mara 3,4,5..Lol!

    ReplyDelete
    Replies
    1. NDIO NI KWELI KABISA UMAARUFU NDIO INAMFUATA ZARI!!!!

      Delete
  2. Mimi binafsi sijali sana umaarufu wa Zari ila namuhofia sana kijana wetu Diamond kama atakuwa na mwisho mzuri na huyu binti hasa ukiangalia upande wa Zari, huyu dada tayari kamaliza maisha kwa kuwa tayari alikwisha olewa na amezaa watoto watatu na Diamond bado yupo freshhata mtoto wa kusingiziwa hana je mwisho wao unakuwaje?
    Diamond hafanani tena kumuoa Zari, na je Zari atakubali kuachwa njia panda wakati kaingia na miguu yote kwa Diamond? Mhh, naona kama ipo shida inakuja muda si mrefu hasa ukizingatia wadau wa Zari wameanza kumtafutia kashfa Diamond eti ni Shoga ilimradi wamuharibie tu ili awe na dosari. Atahitaji kuwa na mwanasaikolojia au ataharibikiwa.

    ReplyDelete
  3. Umeenda kwenye website ya Zari umecopy na kupaste halafu unakuja kudanganya watu kuwa hivyo ndio kumfahamu kwa UNDANI Zari. Hivi hujui kuwa dunia siku hizi imekuwa kijiji? Ngoja nikudonolee tu ukweli kuhusu Zari. Kwanza hamiliki hayo magari unayosema anamiliki, pili hata hayo maisha unayoyaita ya juu hata huko kwao Uganda wanasema alivyoanza kutoka na Diamond ndio ameanza kuishi kama Superstar. Tatu hakuwahi kuolewa alizaa tu na Ivan kwa sababu ndugu za Ivan walimkataa.

    Mwisho jina lake halisi alilozaliwa na kupewa akakuwa nalo ni ZAITUNI KIRIJWAKO, ukigoogle kwa hilo jina la Zaituni Kirijwako ndio utaufahamu undani wa Zari the Bosslady asie na mkwanja wake mwenyewe.

    Na hizo biashara za mumewe mnazomsifia nazo ni biashara za unga kwa sababu Uganga wa kienyeji haumewezeshi mtu kununua magari ya kifahari.

    ReplyDelete
  4. anomymous 8.34. pole sana hater. utake ustake zari yupo juu siyo hiyo wema wenu

    ReplyDelete
  5. Zarinah Zaituni ambaye tunamjua kama Zari namfahamu sana. Familia yake ilikuwa ya kuhangaika sana ila ilikuwa na wasichana watatu ambapo wawili wao walikuwa wazuri sana ambao walikuwa wanamvuitia sana wanaume. Kati ya mwaka 1996 na 2000 wasichana hawa walikuwa maarufu sana kwenye baa mbalimbali sana pale Jinja na karibu kila mwanamme mwenye hela aliwatembea nao wote, ndipo Zarinah aliweza kuzaa mtoto mmoja wa kiume na jamaa ambaye hakuweza kujulikana vizuri wakati huo. Mwaka 1999 Zarinah alitoroshwa na jamaa mwingine anayejulikana kama Ivan ambaye alikuwa amepata hela nyingi sana kutokana na kufanya biashara ya madawa ya kienyeji huko Afrika ya kusini; akahamishiwa huko bondeni. Ivan akampenda sana Zarinah na kuamua kumsomesha elimu ya juu ambapo alimpeleka London kusomea urembo. Baada ya kupata cheti cha urembo Zarinah alitaka awe mwanamuziki, hivo mwaka 2007 akaaza mambo ya muziki. Hakufanya vizuri katika mziki hivyo akaamua kuuacha na kuanza kusimamia biashara mbalimbali za Ivan ambazo alizitangza kwa jina la mrembo Zari. Utajiri wa Zari ni wa mme wake Ivan; ndiyo maana leo hii Zari ndiye anayetunza ndugu zake wote.

    Baada ya kuachana na Zarinah, Ivan amekuwa kama amechanganyikiwa kidogo kwa vile aliwekeza pesa nyingi sana kumfanya Zarinah awe mwanamke staa, lakini akashangaa kuwa baada ya Zari kuwa staa akamkimbia. Diamond aliingia kwenye kurunzi ya Zari baada ya Ivan kukataa kulipia White Party, na Zari akambembeleza Diamond awe mgeni rasmi ili kuvutia watu, jambo lililofanikiwa sana nje ya matarajio ya Zari mwenyewe. Hakuna anayejua njia ya Zarinah, Diamond na Ivan katika mkabala huu itaishia wapi ngoja tuwafuatilie pole pole kwa makini. Kuna mahala nimesoama kuwa Zari ana mimba ya Diamond ya wiki tano; huenda hiyo itavunja kabisa ndoa baina ya Ivan na Zari na hivyo kufungisha ndoa mpya ya Diamond na Zari. Katika sheria ya ndoa inapotokea hali ya nama hii huwa kunaweza kuwa na tafsiri nyingi sana; tusubiri tuone.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acheni wivu wenu!!!! mtasema sana!!.Diamond mtunze na kumjali sana Zari achana na hao ni mawivu yao tu!! Wana wivu haooooooooooo!!!

      Delete
  6. woote mtajifanya mnamjua Zari ila ukweli utabaki kwa wenyewe nani kamtajirisha mwezie as longer wamezaa utajiri utabaki kuwa wao wote na ndomana Ivan hafatilii magezeti na anamtunza zari na watoto coz mali ni zao wote. ukishakaa na mwanaume miaka miwili chochote alichochuma ni cha kwenu wote so haijalishi zari masikini au anajivunia utajiri wa mwanaume. upooooo je ingekuwa zari hajitumi kusimamia hizo kampuni au maduka leo hizo mali zingejulikana? ukiona mafanikia ya mwanaume ujue nyuma yake kuna mwanamke anae mwongoza.

    ReplyDelete
  7. Dimondo mafanikio yake ni juhudi zake jumlisha mama yake anamwongoza vyema.

    Hivyo Zari anaweza kuolewa na Dimondo iwapo watakubaliana wote waislam na dini haichagui ukubwa wa mtu ni upendo wa dhati.

    ReplyDelete
    Replies
    1. WEWE UMESEMA KWELI KABISA MAPENZI HAYAJALI UMRI KAMA WANAPENDA KWA DHATI WAFUNGE NDOA TU TENA WOTE WAISLAMU HAKUNA SHIDA. CHIBU FANYA KWELI BASI!!!!!!

      Delete
    2. Zarina alikuwa muislamu lakini sasa sio muislamu ni born again christian labda asilimu sasa baada kumpata Diamond. Na alisema mwenyewe kwenye Sporah show kuwa yeye ameokoka. Kwikwikwii hata mukiandika kwa herufi kubwa haisaidii.

      Delete
    3. ALAAAA KUMBE KAOKOKA MBONA HIZO HABARI NJEMA KABISA!!! BIG UP ZARI JINA LAKO LA WOKOVU NI LIPI??? HAISUMBUHI HIYO NDOA MTAFUNGA KWA MKUU WA WILAYA MBONA POA TU

      Delete
    4. kwikwikwi za nini au ulichoandika sio za kweli???

      Delete
  8. MTASEMA SAANA NA VIJIBA VYENU VYA ROHO DIAMOND NA ZARI KAMA KAWA!!! MANENO YENU YANAONYESHA WIVU WA KIWANGO CHA JUU SAANA. POLE WEEE .DIAMOND NA ZARI KAZENI BUTI BINADAMU KAZI YAO KUSEMA MSIOGOPE !!!!

    ReplyDelete
  9. Sheria ndio itakapo fanya yake hapo baada ya kuzaa. Zari atamwambia dai zikutaki ila nataka matunzo ya mtoto. Weee mali zinahamia ya zari tena.

    ReplyDelete
    Replies
    1. WANA WIVU HAOOOO!!!! DIAMOND ULIIMBA NA SASA YANATOKEA MIYE NAKWAMBIA HIVI KUWA NA MSIMAMO USIYUMBISHWE NA MANENO YAO WATASEMA MCHANA USIKU WATALALA MTUNZE ZARI MTOTO AZALIWE SALAMA!!! AKIKISHA ZARI HAPATI STRESS CHIBU!!! MUNGU AKUPE NINI TENA!!!!

      Delete
  10. DOMO ATALIUA JIJI MALI ZITAMILIKIWA NA ZARI MAAAKE ATAJUUTA MANA HATAPATA KITU

    ReplyDelete
    Replies
    1. HELA ZA ZARI DIAMOND HAFUI DAFU!!!!

      Delete
  11. ZARI ANA HELA WEWE!!!

    ReplyDelete
  12. Kweli bongo supu.hamuna jipia nihela naumbea.TZ

    ReplyDelete
  13. maisha yao tuwaachie wao wenyewe,hata mkikesha mnabishana haitawasaidia chochote,its like agame so let us watch

    ReplyDelete

Top Post Ad