Mwanamke Kama Unataka Kumnasa Mwanaume Mwenye Sifa Fanya Hivi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kama wewe ni mwanamke ambaye umeshafikisha umri wa kuolewa lakini wanaume wenye sifa uzitakazowanakupitia kushoto basi soma hapa kwa makini

Kumpata mwanaume mwenyesifa uzitakazo na kumshawishi akuoe si jambo rahisi siku hizi, ni kama vilekumchinja kobe wallah. Baada ya kufanya kautafiti kangu kadogo nimepata majibumuafaka kwa wale wanawake wenzangu wenye kuhemkwa na ndoa.

Ngojeni niwashushieni material ya kuwanasa wanaume wenye sifa maridhawa.

1.Kuwa mtu wa Mungu yaani muumini haswa siyo wa kubabaisha, siyo wale kina vilongwa mbalivitendwa mbali, wamejisemea Wazaramo yaani unasema mengine unafanya mengine,kama ni muumini hakikisha unashiriki vume kwenye ibada na matendo yako yawe nimanyoofu. Shiriki kwenye matamasha ya kidini, vikao vya jumuiya, toa zaka nasadaka, saidia wasiojiweza siyo kifedha, hata kwa ushauri nasaha, lakini piajiunge na kamati mbalimbali katika nyumba yako ya ibada iwe ni msikitini aukanisani au jamatini. Kwa kufanyahivyo utakuwa umejiweka kwenye nafasi nzuri ya kumvutia mwanaume wa wa ndotozako.


2.Kama wewe ni mwanamke mwenye misimamo , mwenzangu jishushe. Nakusihisana ujishushe mwanamke mwenzangu, lasivyo utadoda. Wanaume wenye muafaka nidhaifu sana na wana aibu na wasiopenda kuzodolewa, kama wewe una tabia zakupenda ligi za kubishana mwenzangu humpati mwanaume mwenye muafaka, utawaonakwa mashoga zako, utaishia kuzalishwa na kuachwa au utaishia kupata gume gumelisilojia mawio au machweo, linachojali ni tendo la ndoa na kukuzasha, kwaniwenyewe husema mwanamke jeuri piga mimba jeuri yote kwisha. Ni vyema ukauweka ufeminist wako pembeni uvae umwanamke na uwe halisi, kelele zako ziwe ni zamajukwaani ukifika kwa mumeo piga kimya na uwe na heshima ya kianakike kwa mwenziwako.


3.Swala la kukutana kimwili mara baada ya kufahamiana kwa wanaume linapewa kipaumbele. Hapozamani wanaume walikuwa na uwezo wa kupigwa tarehe hata miezi sita hadi mwakawakamudu kuvumilia, lakini wanaume wa siku hizi, thubutuuu. kwa ushauri wabure, unaweza kupiga change mara mbili lakini isizidi mara tatu kama umempendahuyo mwanaume, ukijifanya unauvutia kasi kwa kuuweka usiku, atakuponyoka wallah, wanaume wa siku hizi hawajazoea mapozi. Hakikisha umezingatia vigezo vyote kumvutia akuoe ndipo ujitose mzima mzima lakini kama uko na maudhaifu yako utaishia kuchezewa.


4.Wanaume wanapenda sana kupewa nafasi, siyo kumbana na kumnyima pumzi, mwanaume anatakiwaaachwe kama mwanaume na kupewa nafasi ya kuonyesha uanaume wake siyo mambo yakufuatana fuatana nyuma kila wakati, mara mbona umechelewa kurudi kutokakazini, ulikuwa wapi, au mbona unanukia manukato ambayo siyajui, ulikuwa na nani, au kuchuguza chunguza simu yake. Kama simu yake inaita na yeye anaoga au kaisahau chumbani usiangalie display kama ni nani anapiga simu, igeuze kifudiudi na kumpelekea mwenyewe pale alipo na kama ana chati kwenye WOZAP usipige chabo kutaka kujua ana chati na nani. kwanza unatakiwa ufurahi kwamba mumeo ana mvuto na kiasi cha kuwavutiawanawake wengine, cha muhimu kwako ni kuhakikisha unamtengenezea mazingirampaka akubali mfunge ndoa, ukianza ghubu kungali mapema atakuona kimeo nakukubwaga.


5.La mwisho, nihuduma muhimu kwa mume. Mwanaume ni tendo la ndoa, chakula na usafi wa ndani nawa nguo zake, kamwe usije ukamuacha mwanaume akaondoka nyumbani na njaa, walaakaondoka na nguo chafu au zisizopigwa pasi. Kama ana mazoea ya kukutaka muwemnakula kwenye mighahawa piga marufuku hiyo tabia, tumia hizo fedha kumpikianyumbani kwake au kwako na ikibaki chenji mrudishie yote siyo unaanza kubaniabania chenji mapema atakuona huaminiki, lakini pia siku moja moja unatakiwa uchangie hela ya mtoko au shopping siyo kumuomba omba hela, ni vyema kumshagaza na vijizwadi kama vie boxer, soks za viatu au leso, waume ni wavivu kununua vitu hivyo, kama umeona shati zuri au zile fulana za ndani ni vyema pia kumnunulia. Ni muhimu sana kuhakikisha mwanaume anakuta kila kitu kiko tayari kinamsubiri na nyumba inakuwa safi wakati wote hata akija na wageni hana haja ya kushikwa na kigugumizi kwamba sijui charminglady kafanya usafi wa nyumbani au atakutana na nyumba chafu na nzi kila kona.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hayo alifanya bibi yako akafanya mama ako akakurithisha na ww tafdhali waandikie urithi wajukuu zako, itawasaidia sana, sikila mtu anaishi kwa mawazo ya mtu au alivyoiishi shangazi yako ndio kila mtu afanye kaa mbali mama dini na kutoa uchi wapi na wapi? unamtegemea Mungu au unategemea kiuno chako?

    ReplyDelete
  2. haya mada hiyo nzuri sana je akisha kuoa je ....bado umurusu mijike mingine endelee kumuandika sms ati ni heshima...?????????????????????

    ReplyDelete

Top Post Ad