NCCR-Mageuzi wataka Rugemalira, Tibaijuka, Chenge Wafikishwe Mahakamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama cha NCCR-Magezi kimesema, vigogo wote waliohusika kutoa na kupokea mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow wafikishwe mahakamani akiwamo Mkurugenzi wa VIP Engineering Ltd, James Rugemalira .

Kashfa hiyo imesababisha Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake la Mawaziri kutokana na mawaziri wawili kujiuzulu.

Mawaziri waliotajwa kwenye sakata hilo ni Profesa Anna Tibaijuka, ambaye alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na aliyeingiziwa Sh1.6 bilioni na mwanahisa wa zamani wa Kampuni ya IPTL, James Rugemarila.

Wengine waliopata mgao huo kutoka kwa Rugemarila na kiasi katika mabano ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge (Sh1.6 bilioni), Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja (Sh40.4 milioni), aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (Sh40.4 milioni), Mbunge wa zamani wa Sumbawanga (CCM), Paul Kimiti (Sh40.4 milioni) na aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk Enos Bukuku (Sh161.7 milioni).

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema waliofikishwa mahakamani hadi sasa ni vidagaa lakini na vigogo mashuhuri wakiendelea kutamba.

“Mpokeaji na mtoaji wa rushwa wote ni wahalifu na wanatakiwa  kufikishwa mbele ya mahakama ili wajibu tuhuma zinazowakabili...Rugenarila naye ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kufikishwa mahakamani.”

“NCCR tunataka kujua kwa nini baadhi waliopewa rushwa wamefikishwa mahakamani lakini watu wengine kama Profesa Tibaijuka, Chenge, Ngeleja, Yona, Kimiti na wengineo hawafikishwi mahakamani? Wote wanatakiwa kwenda kujibu tuhuma zao,” alisema Nyambabe

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah alipotafutwa kuzungumzia kauli hiyo ya NCCR alisema, “Sipo ofisini hivyo nisingependa kulizungumzia hilo.”

Waliofikishwa mahakamani hadi sasa ni Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Umeme Vijijini (Rea), Theophillo Bwakea na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma, ambao kwa pamoja wanadaiwa kupokea rushwa ya Sh485.1 milioni.

Wengine ni Meneja Misamaha ya Kodi wa TRA, Kyabukoba Leonard Mutabingwa, Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Roman Urassa na Mkurugenzi wa Fedha BoT, Julius Rutta Angello wanaokabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa ya jumla ya Sh1.923 bilioni.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad