Wizi wa KupinduWizi wa Kupindukia....Kamati ya Zitto Kabwe Yafichua namna Mabilioni ya Fedha yanavyoibiwa Serikalikia.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TAARIFA ya mwaka ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ya hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu na mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2013, imebua wizi wa kutisha wa fedha za umma uliofanywa na taasisi hizo.

Hayo yalibainika jana wakati Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, alipokuwa akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo, ambapo alisema katika ripoti za ukaguzi kwa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), imebainika kuwa ililipa mabilioni ya fedha kwa ajili ya ndege iliyoikodi kutoka Shirika la Ndege la Wallis Trading Inc la China, ndege ambayo ni hewa kwa kuwa haipo nchini.
“Hadi sasa Serikali imelipa dola za Marekani 26,115,428.75, (Sh bilioni 45.17) na sasa inadaiwa dola za Marekani 23,996,327.82 (Sh bilioni 41.51), ndege hiyo ilikuwa mbovu na ilifanya kazi nchini kwa miezi sita pekee badala ya miaka sita kama mkataba wa ubinafsishwaji ulivyotaka,” alisema Zitto katika taarifa yake.

Taarifa hiyo ya PAC, ilibainisha pia kuwa katika ujenzi wa jengo la watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja Ndege wa Kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kuna ufisadi wa takriban Sh bilioni tisa.

Ilisema pia jengo hilo lilianza kujengwa bila kibali cha Baraza la Mawaziri na kuwa thamani ya gharama za ujenzi wa jengo hilo hazijulikani kwa kuwa nyaraka muhimu hazipo.

Kwa upande wa Mamlaka ya Bandari (TPA), imebainika kutumia Sh bilioni 9.6 kwa ajili ya vikao vya wafanyakazi na mamilioni mengine kujilipa kwa ajili ya posho za safari bila kuwa na kibali kutoka serikalini.

Zitto alisema pia kamati yake imebaini kuwa misamaha ya kodi imezidi kuongezeka na kufikia Sh trilioni 1.8 mwaka 2014, huku zaidi ya Sh bilioni 80.45 za misamaha hiyo kwa mwaka zikitumika kwa njia zisizo halali.

“Mbali na hilo, pia fedha za pembejeo za kilimo zimekuwa zikitumika visivyo halali na kwa zao la korosho, zaidi ya Sh bilioni moja zilitumika kinyume cha taratibu,” alisema Zitto.

Kwa upande mwingine, ripoti hiyo imesema mifuko ya hifadhi ya jamii ipo hoi kutokana na Serikali kushindwa kulipa deni la Sh trilioni 1.87 ilizokopa.

Pamoja na hilo, taarifa ya PAC imesema pia Serikali ina hatihati katika hisa zake zilizopo katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), endapo hatua za kulipa deni la Sh bilioni 22 hazitachukuliwa hadi kufikia Machi 31.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mweeeehhhhhhhhhhhhhhhhhhhh

    ReplyDelete
  2. Tumechoka na huyu Zitto na Kamati yake ya mahesabu. Yeye kazi yake ni kuibua kashfa kila kukicha. Lakini hatuelezi ni hatua gani ambazo yeye na kamati yake wamezifanya ama wanatarajia kuzifanya ili kuzuia uhalifu na ufujaji mkubwa wa fedha za umma. Kila kukicha ni hili na lile. Hakuna mpendekezo yoyote ya maana tunayoyasikia kutoka katika Kamati yake. Na huu ufujaji wa fedha za umma haujaanza jana wala leo.Ni kitu tunachokisia kila kukicha miaka nenda miaka rudi. Mimi nadhani huyu mtu anayeitwa Zitto anatafuta tu umaarufu wa kisiasa na pengine ni mmoja ya sehemu ya hao wafujaji fedha za umma. Kama hawezi kuja na mapendekezo ya kudumu na ya kimsingi ya kuzuia hili tatizo basi sisi wananchi hatuoni sababu ya kuwepo yeye na hiyo kamati yake ya mahesabu. Hiyo kamati ivunjwe na yeye aondolewe katika hiyo nafasi ya uenyekiti. Tumechoka kuona ni jinsi gani anavyoitumia hiyo nafasi yake kutafutia umaarufu wa kisiasa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yeye kama mwenyekiti ni kazi the kutoa taarifa tu vyombo husika vitashughulika

      Delete
  3. MAYOOOOO WEEEE !!!!

    ReplyDelete
  4. Atoke na zake hapa. Atuondokee hapa na uongo wake. Badala ya kutuletea maazimio ya kudumu ili kuzuia kabisa ufujaji wa mali za umma. Anabakia hapo na kutusomea ngonjera zisizokwisha kuhusiana na huo ufujaji wa fedha za umma. Hata kama wamebaini huo wizi wa mabillioni ya shilling sasa wanataka sisi wananchi wa kawaida tufanye nini?????? Zitto achana na hizo cheap popularity tumezichoka.

    ReplyDelete
  5. Tunataka kuona faida pia sio ripoti tu peke yake zirudi hizo pesa

    ReplyDelete
  6. Ama kweli watanzania ni wagumu kuelewa.kamati hii iliundwa mahususi kuchunguza hesabu za serikali na hizi report za zito ndio matokeo yaliyopatikana baada ya uchunguzi na lazima report hizi ziwasilishwe bungeni ili bunge kupitia sheria zilizopo liwawajibishe wahusika,mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa yalishatolewa na kamati hii toka sakata la escrow sasa nyinyi huwa mnafuatilia mijadala hii au ndio kudandia train kwa mbele.na mkumbuke kamati hii haiundwi na zito peke yake.kamati inapaswa kupongezwa kwani hata wao wangeweza kuhongwa na hao wezi na kutoa report za uongo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa unachotaka kusema hiyo Nchi imeoza. Kwa sababu hakuna hata siku moja tumewahi kumsikia Zitto na kamati yake wakitoa ripoti yenye kuelezea mahesabu yaliyosawa Ndani ya Serikali. Kila kukicha ni ufujaji na ubadhirifu wa fedha. Hatuoni Sheria na wala vyombo vya kutunga hizo sheria vikichukua tahadhari yoyote ya maana ili kuzuia kabisa kuwepo kwa ufujaji huo wa fedha. Sasa hiyo maana yake nini???????? Na sio kweli wewe anonymous hapo juu wa 9:32 AM kusema kuwa huwa hatufuatilii hiyo mijadala au eti tunadandia train kwa mbele. Hiyo sio kweli. Ili kimsingi sisi wananchi wa kawaida TUMECHOKA na hiyo MIJADALA isiyoisha ya UFUJAJI WA MALI ZA UMMA. Kila siku ni ngonjera hizo hizo. Hatuoni kama kuna hatua zozote za maana na kisheria zinazochukuliwa dhidi ya wahusika. Hatuoni kama kuna dalili zozote za KULIMALIZA KABISAAA hilo tatizo la UFUJAJI WA MALI ZA UMMA. Na ndio maana tunaanza kuhoji uhalali wa kuwepo kwa hiyo KAMATI YA ZITTO NA WATU WAKE ikiwa kama ni kweli inatoa mapendekezo yoyote ya maana na ni kwa nini hayatekelezeki.

      Delete

Top Post Ad