Uchawi Wamkimbiza Zari Bongo ..Hofu ya Mimba yake Kufanyiwa Uchawi Yatawala..Amtaka Diamond Wakaishi Sauz

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

ISHU ya uchawi kwa wanawake wajawazito ndilo suala kubwa linaloingia kwenye hisia za baadhi ya watu hasa mimba inapokuwa changa, hofu hiyo sasa imemwingia mwandani wa Mbongo-Fleva anayeuza zaidi kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,  Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ ambaye anadaiwa kuikimbia Bongo kwa muda ili mimba yake isije kuchoropoka kama ilivyokuwa kwa akina Wema Sepetu na Penniel Mungilwa ‘Penny’.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa familia ya Diamond, hivi karibuni Zari aliondoka Bongo mara tu baada ya kurejea kutoka Zanzibar walikokuwa wameenda kula bata katika Msimu wa Valentine.
Chanzo hicho kilidai kwamba, wakati staa huyo mwenye maskani yake Afrika Kusini na Uganda akiwa Bongo maneno mengi yalisemwa na wengine kudiriki kuwapigia simu watu wa familia hiyo wakimtaka Zari aache tabia ya kujionesha na ujauzito wake kwani hawajui Wabongo vizuri.

NYUMBANI KWA MAMA D
Ilidaiwa kwamba mmoja wa watu waliokuwa wakiambiwa ishu hiyo alimfikishia moja kwa moja Zari aliyekuwa akipika na kupakua nyumbani kwa mama Diamond ‘D’, Sanura Kassim ‘Sandra’ maeneo ya Sinza-Mori, Dar.
Habari zilidai kwamba, Zari aliposikia maneno hayo aliamua kuondoka huku Diamond akisapoti uamuzi wa mpenzi wake kwa asilimia mia.

HOFU YATANDA
“Alipomwambia Diamond kwamba anaondoka kwa hofu ya mambo ya ushirikina, jamaa alimuunga mkono na kumsisitiza kutulia kabisa maana majanga kama hayo Bongo huwa ni ya kawaida na yalishawahi kumtokea kwa Wema na Penny ambao walishika ujauzito na ulitoka bila kujua sababu za msingi.

“Kweli Zari amekimbia Bongo, baada ya kuona watu wanamfuatafuata kila kukicha, si unajua Wabongo huwa hawaishiwi maneno? Zari amemtaka Diamond wakaishi Sauz.
“Watu wamekuwa wakisema vibaya juu ya uhusiano wake na Diamond, hasa kipindi alipokuwa Zanzibar, hivyo baada ya kurudi tu aliamua kwenda zake South (Afrika Kusini) ili akajipumzikie wasije wakampagawisha mimba yake ikatoka bure.
“Nafikiri mwenyewe unajua namna Zari alivyokuwa maarufu Bongo tangu awe na Diamond hivyo siku hizi kila anachokifanya utaona wanavyomtolea macho na wengi wao hawaishi kuudisi ujauzito wake.

YASIJE YAKAWA YA WEMA NA PENNY
“Maana wanasema eti hawezi kuzaa na Diamond, kuepuka maneno kaamua kujiondokea zake wasije wakamloga bure akashindwa kweli kuzaa na ndugu yetu kama ilivyoshindikanika kwa Wema na Penny,” kilisema chanzo chetu.

TUJIUNGE NA DIAMOND
Baada ya kujazwa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimsaka Diamond ili athibitishe kama kweli kilichochangia Zari kuondoka harakaharaka Bongo ni kwa sababu ya kuogopa ushirikina ili mimba yake isichoropoke kama inavyosemwa, jambo ambalo Diamond aliishia kuguna huku mdogomdogo akifafanua.
“Ujue Wabongo wana maneno sana na mara nyingine huwa wanalazimisha uongee hata vitu ambavyo havipo.
“Mimi sina mtoto na natamani sana siku moja niwe naye hivyo ninapokuwa na mtu naye anaonesha hali ya kunisapoti na nia moja ya kunipa mtoto, sina budi pia kumheshimu kwa uamuzi wake.
“Kweli Zari aliondoka siku chache tu baada ya kurudi kutoka Zanzibar, hayupo Bongo, si unajua Bongo mambo mengi inafikia hatua hata kumkatalia anapotaka kuondoka inakuwa ngumu maana Wabongo wanaongea sana na mara nyingine wanamfanya mtu kukosa imani na ndiyo maana inafikia wakati nashindwa kujibizana nao.
“Ninachoamini mimi ni katika Mungu tu, yote wanayosema ipo siku yatapata majibu maana Zari Kiswahili hajui vizuri hivyo tunaepuka sana watu kumtumia umbeya na kumtafsiria vitu vingi ambavyo si sahihi,” alisema Diamond.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hahahaha hajui kiswahili ila mdaku hatwariii, dogo chukua jiko ilo weka ndani acha tantariraaa vigezo vyote utakavyo katimiza unasubiri nini wee kijana mbona mnapenda uzinzi uwezo unao mnapendana msipoteze muda

    ReplyDelete
  2. Usio fira ukijaza ukifira wengine mpaka kufa kwako ndio watakukoma wabongo

    ReplyDelete
  3. chukua weka ndani kwa njia ya halal zina wacha dogo ni hatari, IF YOU LOVE HER WAT ARE YOU WAITING? chukua jumla ndio waseme sana

    ReplyDelete
  4. Usirudie kosa kurudi kwa team upupu,nakingine mungu akusaidie ombasana wasiopenda mafanikio yako ndiowanaohangaika kuchafua huku nahuko.Ila mungu tu ndio mkombozi wako mpende zari sana kwani nae anakupenda,naikibidi kama unamkubali muoe ili mtimize maandiko ya mungu msifanye zinaa,na Mungu atawasimamia nawalahutashuka kimziki

    ReplyDelete

Top Post Ad