Ushauri kwa Waislamu Wote Tanzania, Hasa Walio Mtandaoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nimefikiria muda mrefu kuhusu sakata hili la kufa na kupona la mahakama ya kadhi. Ni wazi kuwa mahakama ni muhimu katika jamii. Lakini pamoja na umuhimu wake, nadhani tukikaa chini na kutafakari, kuna mengi ya umuhimu zaidi. Jambo la kwanza .......
kwa Nchi kama Tanzania ambayo kwaajili ya uongozi mbovu wa waliokuwa madarakani kwa nyakati tofauti lingepaswa kupewa kipaumbele ni Elimu. Ona jinsi Elimu inavyochezeshwa gwaride, hadi tumefikia hatua ya kuweka div. 5, ili kuficha waliofeli.

Nirudi kwenye mada,
Nasema ushauri kwa waislamu kuwa waongeze nguvu kwenye elimu dunia. Waongeze shule zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu, zenye ubora. Waongeze vyuo vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kiislamu, wakitaka wawapokee waislamu tu haidhuru, lakini ni bora wakawapokea wote kama zifanyazo taasisi za kikristu. Elimu bora Tanzania inahitajika. Na Elimu bora Tanzania haiwezi kutolewa na Serikali tu. Ona madhehebu ya kikristo walivyoweka kipaumbele katika elimu. Hesabu tu vyuo vikuu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo. Hesabu shule za sekondari zenye ubora wa hali ya juu zinazoendeshwa na taasisi za kikristo. Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza.

Tazama kwenye afya, ona ni vituo vingapi vya afya, hospitali, hadi hospitali za rufaa zinazoendeshwa na taasisi za dini? Nafahamu walau hospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando zinaendeshwa na taasisi za kikristo. Hospitali za kawaida ni nyingi. Zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu sizifahamu, zinaweza kuwa nyingi kuliko hizo, au la. Kwenye suala la afya ndipo pa kutumia nguvu nyingi. Huko ndipo pa kuwa na hitaji la kuweka kambi Bungeni kama kutakuwa na haja.

Nadhani sio vizuri kusubiri siku zote kubebwa na serikali. Kila madhehebu wana sheria zao, sheria zao ambazo hazipaswi kwenda kinyume na sheria za Nchi. Sioni sababu ya kutumia nguvu kubwa kudai mahakama badala ya kuwekeza kwenye mambo ya maandeleo kama elimu, afya, nk. Kwanini tunadhani maisha yetu lazima kupelekana mahakamani?

Ndiyo maana nasema natoa ushauri kwa waislamu hasa waJF maana ndo watakaosoma ushauri huu, Waislamu wawekeze nguvu nyingi kwenye mambo ya maendeleo zaidi kuliko mahakama. Wawekeze kwenye elimu na afya. Achaneni mambo ya mahakama. Mahakama ya nchi inaweza kumaliza yote, ikiwa kutakuwa na haja. Lakini kwa mtu optimistic hawezi kutumia nguvu nyingi kwenye hilo.

Sio haki kwa wabunge: wawakilishi wa wananchi kupoteza muda kujadili kuwa waislamu wawe na mahakama ya kadhi au la. Ni wazi watajadili, hasa wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Ili kila mchangiaji aonekane anawajali waislamu, ataunga mkono mahakama ya kadhi, watafanya funika kombe mwanaharamu apite. Ili tu waislamu wa jimbo lake wasimtose, ili tu waislamu wasikikatae chama chake. Lakini nasema tena sio haki wabunge wapoteze muda katika jambo hili ambalo sio kipaumbele cha taifa. Sio haki lakini litajadiliwa kwaajili wa woga wa kupoteza kura.

Mniwie radhi, kama kuna moja hatapendezwa na ushauri wangu. Ukweli utabaki kuwa kuwekeza kwenye elimu, hasa elimu dunia na afya ni bora kuliko kuwekeza kwenye mahakama.

Chanzo : Jamii Forums
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

32 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ushauri mzuri ila kanisa halitawaacha waendeshe mashule,lazima litawazima tuu kama alivyofanya kambarage!na kwa kulijua hilo ndio maana wameona wakazanie mambo ya akhera na duniani watuachie sisi tutumie maxcrow yetu!Si umeona katika sakata zima la xcrow hawa jamaa hawajakula hata senti moja wakati wenzao wamebunya mabilioni,teh teh teh!

    ReplyDelete
  2. USHAURI WA MAANA SANA NDUGU TUMEKAZANIA MAHAKAMA YA KADHI KWAMBA SISI NI WAKOROFI SANA MPAKA TUNAITAJI MAHAKAMA HIYO. TUMEACHA KUPIGANIA VITU MUHIMU KWA ELIMU YA DUNIA AFYA NA MIUNDO MBINU KAMA BARABARA N.K TUMEKAZANA MAHAKAMA YA KADHI MAHAKAMA YA KADHI. HUKO MAHOSPITALINI AKINA MAMA WAJAWAZITO WANALALA WANNE KITANDA KIMOJA MADAWA HAKUNA MAJI HAKUNA VYAKULA BEI JUU HAYO HATUONI TUMEONA MAHAKAMA YA KADHI TU???????

    ReplyDelete
  3. Yes ushauri wako ni mzuri na unafaa sana. tumeacha kudai mambo muhimu tumekazania mahakama ya kadhi ili iweje kwamba sisi waislam ni watukutu saana????

    ReplyDelete
  4. Ushauri mbovu ambao sijapata kuuona ni huu . Eti umejiona una akili mno kuliko millions of Muslims . Nitakuwa sina la kukuambia kwa sasa ila endesha propaganda ujipime IQ.

    ReplyDelete
  5. USHAURI MZURI SANA!!

    ReplyDelete
  6. Hamjui maana ya mahakama ya kadhi ina umuhim mkubwa kwa waislamu mfano kunakesi nyingi za kidini za mirasi huwezi kumpa kesi hakimu asojua sheria za kiislamu hiyo hoja yako ni nzuri na waislamu ktk hilo wamelala tofauti na wakristo lkn mahakama ya miradhi ni muhim zaidi hasa kwa sisi waislam

    ReplyDelete
  7. UTAIFA WETU NI MUHIMU PIA!! FAMILIA ZETU ZOTE ZIMECHANGANYIKA SIDHANI KAMA KUNA FAMILIA AMBAYO INA DINI MOJA TU HAKUNA.

    ReplyDelete
  8. Mnataka kutuwekea sheria ya wanawake wakizini wapigwe mawe hadi kufa,sijui mara kufunika sura,yaani wanawake wa kiislamu tusiwe na sauti?Hatutaki mahakama ya khadhi wala nini,kwani si kila mtu na majibu yake siku ya kiama.

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha ujinga, mahakama ya kadhi haikufuati tu mradi ni muislam, ispokuwa kama una imani na dini yako ndio itakuhusu. we kama malaya fanya umalaya wako tu usije ukaogopa mahakama muogope utakayekutana nae siku ikifika!

      Delete
    2. haya nawe matusi ya nini tena? ndo utukutu wenyewe huu tusioutaka!! mahakama ya kadhi noooo. hili litatugawa watanzania

      Delete
  9. You are very intelligent my boy bonge la wazo , nadhani ulikuwa unatoka chooni tu wazo likakujia. Una akili sanaaaa, waambie hao.

    ReplyDelete
  10. Tatizo watu hawaendi na alama za nyakati, uelewo ndugu yako sio wote tumejaliwa uweleo, wewe angalia Dunia nzima wapi watu wako nyuma kama sio kwetu huku Africa, hityo midle- East kwenyewe kumendelea, sababu watu wanaenda shule na kusoma arama za nyakati, swala hili ni la vijana, wakiwachiwa wazee ndio hivyo tena, awaendi na alama za nyakati, wanadhani za miaka hiyo ndio za miaka hii, Binadam anaenda akibadilika, tukubali tusikatae, toka enzi hinzo za miaka kenda bara hili hili, watu wakivaa majani na hakuna hata mmja alikuwa amefika kutuletea kuzijua Imani tulizoletwa, mpaka tumeletewa, ni mabadiliko

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe umesema. wanaacha kukazania mambo ya kuteleta maendeleo wamengangania mahakama ya kadhi. fikiria mwanao apate kitabu chake shuleni mkeo apate dawa na mahali salama pa kujifungua. barabara zipitike vipindi vyote masika na kiaganzi wakulima watafutiwe masoko nk

      Delete
  11. We unayejiita mshauri wa waislam washauri kwanza viongozi wako wa dini akina ESCROW wamrudie mola wao na warudishe fedha zetu. Mahakama ni muhimu ila we hujui maana yake. Wala haikuhusu wewe. Bora ukae kimyaaaa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni muhimu kwa waislam na ndio wanapaswa kuianzisha wao wenyewe. mnataka nani awaazishie!!! Hao wanaowaita makafiri ndio waanzishie??? mnashangaza kweli.

      Delete
  12. Sisi waislam ugomvi kwetu ni kawaida, tuanataka tuweke sharia zetu wenyewe hatutaki kupangiwa na mtu. mahakama muhimu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwani kuna mtu kawakataza?????? anzisheni huko huko misikitikini kwenu !!! hakuna mtu anawazuia!!!

      Delete
  13. Kwanza elewa wewe unajiita muislam kua waislama ndio waliokua wakiongoza kua na shule ospital vyuo . Nakuhusu iyo mahakama kwetu ni suala la lazima sio kama unavyo fikilia wewe ukikataa kuwepo mahakama ya kadhi umeukana uislam wako kwanini nyinyi muhoji kuhusu mahakama yetu sisi tutaukumiana sisi tunaotaka kubaki kuwa waisla alafu nyinyi makafili ndio mnaopinga mbona nyinyi mnajeshi mbona hatuoji

    ReplyDelete
    Replies
    1. haha haha wala hakielewiki unachoogea!!!! mungu akusamehe kwani hujui husemalo!!

      Delete
  14. sasa kama mna maamuzi yenu si mngeamua huko huko kwenye ofisi za misikiti? kama ni ishu ya kiimani zaidi fanyeni kiimani na si kushirikisha au kuomba ushauri kwa watu wasio na imani yako wala hata kuijua. kwa upande wangu nilitegemea vijana wa kiislamu ambao asilimia kubwa kwa sasa ni wasomi tena kwenye sekta muhimu sana mngesaidia na wenzenu hasa wale vijana kama wazee wanaopenda mteremko wabadilike, hapa ukitazama kwa jicho la tatu wanaolilia hii mahakama wengi wao ni wale waislam wavivu wa kutafuta vyao, hivyo wanataka wanavyorithirithi hizi mali za marehemu wapate pakubwa kulingana na sheria zao, lkn kwa wale waislam wanaojitambua wenye elimu na mali huwezi kukuta analalamikia hizi vitu, msimwache elimu aende zake matokeo yake ndio haya. mbona wasabato hawajaomba mahakama ya kuwahukumu wanaokula kambare na mbuzi..... ? walitumia akili wakaona ni mambo ya kiimani hivyo wanayatatua kiimani yao, na hao wakatoliki hawajaomba msaada kwa serikali iwape ruhusa ya kuwadhibiti mapadri wanaozini, na kinyume chake wamekubali kwamba siku ya kiama kila mtu analojibu lake mbele ya Allah, sasa vipi nyie wenye imani kali mnashindwa kujiongeza lakini!!!! hebu amkeni jamani akina Dk Salum pale muhimbili wanamcha Mungu hadi wametoka alama usoni na wanafanya kazi kwa bidii na Mwenyezi Mungu kawajalia kipato tena sio mchezo, sasa nyie wengine mna mcha nani anaewakataza kuwekeza kwenye vitu vya msingi kama mlivyotufungulia Islamic bank? AMKENI BANA!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. WEWE UMESEMA KWELI KABISA. WALE WANAOWANIA MALI ZA MAREHEMU NDIO WANAKAZANIA. FANYE KAZI KWA BIDII ACHENI KUNGANGANIA MIRATHI AFTER ALL FUNGUE HUKO MISIKITINI KWENU HIZO MAHAKAMA ZA KADHI MUONE KAMA KUNA MTU AFAWAFUATA.

      Delete
  15. Acha kuongea upuuzi,unajifanya muislam wakati si muislam wewe muislam gani usiyejua misingi ya dini yako na malengo ya kuletwa ktk hii dunia? uislam umeeleza vizuri namna gani unatakiwa uishi ktk hii dunia na jinsi gani ya kukubiliana na changamoto zinazojikeza ktk maisha yako ya kidunia lakini pia unajiandaa na maisha yako ya akhera maana huko ndiko kwenye maisha ya kudumu na dunia ni mapito ya muda mfupi tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. nawe kama unayajua hayo unangangania nini mahakama ya kadhi??

      Delete
    2. umejuaje kama miye si mwislam??? kwani unadhani waslamu wote wanataka hiyo mahakama ya kadhi?? sio wote wengine hawataki hata kuisikia na ni waislamu.

      Delete
  16. Waacheni waanzishe....nzanzibar ipo na sudani na somalia....tunisia ...egypty hadi omani..hakuna jipya.cha msingi kuvumiliana.tatizo nnaloliona ni kuchanganyana dini ktk kuoana.....mkristo hatopata haki za kimsingi kwenye mahakama hiyoo.hilo halifichiki.itakuwa bias kwa maamuzi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndio maana hatuitaki iwe ya kisheria. fanyeni wenyewe na hizo nchi ulizotaja ni vita kila kukicha na mahakama hizo zipo zinafanya kazi gani? zaidi ya kuhukumu kuuwa wanawake tu waliokutwa wanazini tu.

      Delete
  17. Kwa nchi zenye uislam zaidi.....tumeona hata maamuzi yao ni ya ajabu ajabu....mwanamke anauawa kwa kupigwa mawe kwa uzinzi.....mwanaume walaaa.....sharia law ni ya uonevu.haki ni kwa wanaume tuu.escrow ni issue binafsi.waliokula ji jamaa zake wabukoba woote.sio wakristu au maaskofu woote.anzisheni vyuo na shule msome.kadhi court kwa sasa ni ziada tuu.haiitajiki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli kabisa, mashule hayana walimu wa kutosha vitabu hakuna barabara mbovu vijijini masika hakufikiki mazao yanaharibika mashambani bei za vyakula ziko juu kutoka nauli za mabasi ziko juu toka mnazi mpaka post sh 400 toka gongo la mboto mpaka mnazi 450 mpaka ufike posta 850 badala ya gongo la mboto mpaka posta 450 hayo ndio ya kuyapigia kelele mmekazana mahakama ya kazi mahakama ya kazi? inaelekea nyie waislamu ni watukutu saana ndio maana mmekazania mahakama ya kadhi.

      Delete
    2. Nafikiri hao wanawake wanazini na mapepo ndio maana wanamuua mwanamke peke yake. Maana mapepo hayaonikani kwa macho haya ya nyama. YESU AKASEMA YEYE ASIYE NA DHAMBI MIONGONI MWENU NA AWE WA KWANZA WA KUMTUPIA JIWE. (YOH. 8:7) (Mwanamke aliyeletwa kwake kwa uzinzi ili apigwe mawe)

      Delete
    3. KAMA WEWE NI MSAFI UWE KWA KWANZA KUTUPA JIWE!!!

      Delete
  18. Hii dini ya kujitawaza kila saa haina ishu, acha lowassa aingie watu waanze kupiwa sindano na risasi

    ReplyDelete

Top Post Ad