Barnaba: Diamond sio Mwanamuziki wa Kweli Anaimba Kiunjanja Tu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jana, Wakati akihojiwa na Mwanadada Shadee kwenye Kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, Msanii 'Fundi wa Muziki' kutoka nyumba ya vipaji THT, Barnaba Elias 'Barnaba', pamoja na mambo mengi aliyozungumzia, alitoa maelezo kuhusu wasanii watano anaowakubali na sifa zao Kimuziki ambapo alimtaja Msanii wa BongoFleva Diamond Platnumz kuwa sio 'Mwanamuziki' mwenye kujua kuimba muziki kiufundi.

Akifafanua kauli yake kwa mapana , Barnaba alieleza kwamba Diamond hajui kuimba kufuatana na alama zote muhimu za muziki, bali hutumia mtindo flani wa kuimba 'kiujanja', mtindo ambao kwa wanaojua kuimba muziki technically huwa wanautumia pale wanapofeli kufuata kanuni za uimbaji wakati wakiimba.

Hata hivyo, alimsifia kwa kuwa 'mjanja' na kuweza kufanya muziki wake kuvutia na kuleta ladha.

Orodha ya wasanii ambao aliwatolea maoni na kusema ni wasanii anaowakubali sana ni pamoja na, Diamond, Ally Kiba, Ditto, Amini na yeye mwenyewe.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. We barnaba na hao wanaokuunga mkono acheni ufala huo mwenzenu amechukua tuzo kibao za kimataifa yuko top ana hela ndefu halafu unasema hajui wewe unojua umeiletea nini tz hizo ni jelasi tu na roho mbaya na utabaki hapo hapo kwa mtindo huo.

    ReplyDelete
  2. Kalaga bao mwenzio anavuta mkwanja

    ReplyDelete
  3. wstu wagumu kuelewa. yy amesema tachnically diamond haimbii kiufnd tatzo liko wap?, mcmtoe diamond hali ya ubinadam kwa kumfnya hna kasoro

    ReplyDelete
  4. Barnabas kaenda shule na anajua anachokisema...kwa sisi ambao hatujui music tunaona kawaida tu bora tuburudishwe..

    ReplyDelete
  5. Barnaba kaongea kiufundi zaidi Sasa nyie midomo zege. Sijui hampigagi mswaki kwenu

    ReplyDelete
  6. We andunje unadai unaujua muziki kuliko Diamond, kwenye show uliyofanya Kyela - Mbrya, Sativa Hotel ilipata watu 17 mamae huna kitu mbigili wa mlimani

    ReplyDelete

Top Post Ad