Jela ilivyovunja Uhusiano wa Mastaa Bongo Hawa wa Bongo Movies

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katika ulimwengu wa wapendanao kuna changamoto nyingi ambazo wapenzi hukutana nazo huku wengine wakizishinda na baadhi kushindwa.

Wapo wapenzi walioshindwa kuendelea na uhusiano wao mara baada ya mmoja kuugua, kupata ulemavu na sababu nyingine nyingi, lakini wapo walioendelea kuvumiliana pamoja na sababu zote hizo na hatimaye penzi lao likazidi kuimarika na kuwa mfano katika jamii.

Hali hiyo haipo kwa watu wa kawaida peke yao bali hata kwa mastaa wetu wamejikuta wakiangukia katika mtihani huo na kushindwa kuhimili kusimamia mapenzi yao. Kifungo au jela ni moja ya sababu zinazosababisha ndoa au uhusiano wa mastaa wengi na wenza wao kuharibika.
Katika makala haya tunakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao wamekumbwa na sakata hilo:-

Jack Patrick,
Mumewe na Jux
Jack Patrick ambaye aliwahi kushiriki Shindano la Miss Tanzania 2011, alijikuta akitiwa jela mwishoni mwa mwaka 2013 huko Macao, Hong Kong, China baada ya kudaiwa kukutwa na kete 66 za heroin. Wakati Jack anatumikia kifungo chake mumewe wa ndoa, Abdulatif Fundikira alidaiwa kushindwa kuvumilia na kumuoa kisiri Miss Tanzania 2011, Salha Israel hivyo kuhitimisha rasmi uhusiano wao.

Hata hivyo, wadadavuzi wa mambo walidai kuwa hiyo ilitokana na malipizi kwa kuwa hata wakati Abdulatif aliposwekwa lupango akihusishwa na ishu hiyohiyo ya madawa ya kulevya, Jack Patrick naye aliwahi kumsaliti kwa kutoka na msanii wa Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’.

Kajala na Mumewe
Kajala ni staa wa muvi ambaye sakata lake lilianza baada ya yeye na mumewe kuswekwa ndani kwa kosa la kutakatisha fedha na mashtaka mengine. Kajala alitakiwa kutoa faini ya shilingi milioni kumi na tatu (13) au kwenda jela miaka saba (7) huku mumewe, Faraja Chambo akienda jela kutumikia kifungo cha miaka 12 baada ya kushindwa kutoa faini ya shilingi milioni 213.  Ashukuruwe Wema Sepetu ambaye alimtoa Kajala kwa kulipa kiasi hicho cha fedha.

Akiwa uraiani, Kajala alidaiwa kushindwa kuvumilia kukaa na upweke na kukwaa skendo za mapenzi ikidaiwa kutoka na wanaume tofauti lakini kubwa ni ya kutoka na Kigogo mmoja (jina tunalihifadhi) anayetanua naye sehemu mbalimbali wakati mumewe akiozea jela bila msaada wowote kutoka kwake, japokuwa mara kadhaa amekuwa akimuomba Kajala amtoe.

Binti Kiziwi na Z. Anto
Baada ya kutoka na video ya Wimbo wa Binti Kiziwi, Mbongo Fleva, Z. Anto aliamua kumuoa binti aliyetumika katika video hiyo ‘video queen’ (Sandra Khan).

Hata hivyo, misukosuko ya ndoa yao ilianza baada ya kutimiza miaka mitatu ambapo Z. Anto na Sandra walitengana kwa kudai kuwa mkewe alikuwa akishirikiana na makundi mabaya. Uhusiano wao uliisha rasmi baada ya Sandra kunaswa mwanzoni mwa mwaka 2013 huko Hong Kong, China akiwa na ‘mzigo’. Katika moja ya mahojiano, Z. Anto alidai kuwa kwa sasa anaendelea na maisha yake na anatafuta msichana mwingine wa kuoa.

Aunt Ezekiel na Sunday Demonte
Staa wa muvi, Aunt Ezekiel aliwashtusha watu baada ya kuolewa na Sunday Demonte, Mtanzania aishiye ughaibuni.

Habari zilidai kuwa mumewe huyo ameswekwa rumande jijini Abu Dhabi katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE) kwa kesi ya madawa ya kulevya. Kama mastaa wengine, Aunt Ezekiel naye alishindwa kujizuia na kuchepuka na dansa wa Mbongo Fleva, Diamond Platnumz, Mose Iyobo na hatimaye kubeba mimba ambayo siyo ya mumewe Sunday.

Chanzo: GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Life is like circle!

    ReplyDelete
  2. So most everybody has attempted to download from these free locales just to discover that it requires an excessive amount of push to watch contraband films in DVD quality. have a peek at these guys

    ReplyDelete

Top Post Ad