Meseji za Mapenzi za Kajala na Bwana Aliyekuwa na Wema Sepetu Zanaswa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BAADA ya taarifa za mwigizaji Kajala Masanja kudaiwa kumuibia bwana aliyekuwa shosti yake, Wema Sepetu kudumu kwa muda mrefu na kukosa ushahidi wa moja kwa moja, hatimaye ushahidi wa SMS za mapenzi za Kajala na bwana huyo wa Wema ambaye ni kigogo zimenaswa, Amani linakumegea mchongo kamili

Chanzo makini kilichokuwa karibu na Kajala na kigogo huyo, kilipenyeza habari kuwa kimefanikiwa kuzinasa meseji za Kajala kupitia kwenye simu ya kigogo huyo ambaye alidumu katika penzi na Wema kisha kumwagana baada ya Kajala kuingilia kati.

“Nimetumia ujanja wa hali ya juu hadi nikafanikiwa kupata SMS za Kajala na yule kigogo wa Wema, kama vipi niwatumie,” kilisema chanzo chetu.Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, SMS hizo zilionesha namna Kajala alivyokuwa akiitana baby na kigogo huyo, huku wakiwa ‘dip kimalovee’ kiasi cha kigogo huyo kuwagharamia wazazi wa Kajala mahitaji mbalimbali.

“Jamaa walikuwa wanapika na kupakua, kigogo alikuwa akigharamia kila kitu, kuanzia misosi ya nyumbani, usafiri wa location na hata kwa wazazi wa Kajala, alikuwa anatuma fedha,” kilisema chanzo hicho.

Mwanahabari wetu alifanikiwa kuzinasa SMS hizo na kujionea zikiwa na majibizano ya muda mrefu huku zikitaja pia marafiki wa Kajala anaofanya nao kazi kwa muda mrefu.

Baada ya paparazi wetu kumwagiwa SMS hizo, alimvutia waya Kajala ambaye alizikana SMS hizo na kuomba atumiwe ndipo atoe jibu ambapo mwandishi wetu alifanya hivyo lakini hakujibu chochote na hata alipopigiwa tena, hakupokea.
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KHAA JAMANI UDAKU MBONA WACHONGANISHI SANA?? HUYU BWANA SI NI MUME WA MTU?? WEMA ATASEMAJE KAIBIWA BWANA?? NA MWENYE MUME ASEMEJE JAMANI???

    ReplyDelete
    Replies
    1. aaah wee nae kwendraa umeshikilia mume wa mtu mume wamtu huwelewi ni mjane ameachana na mke wake na mke wake anato*** kwengine mbona hamsemi mke wa mtu wee kama unamtaka ck na wee nenda tu ila ndio keshafulia tena oopps anakufaa mana wee wakuhogwa ela ya maarage tu mfyuu

      Delete
    2. ACHA UJINGA WEWE!!! NANI KAKUAMBIA KAACHANA NA MKEWE?? NDO MNAVYOJIRISHA?? MIYE NA KAZI YANGU KWA TAARIFA YAKO NA SITEGEMEI HELA ZA KUHONGWA KAMA WEWE !!!

      Delete
  2. Ukweli unabaki pale pale kajala is a nasty woman for me doesn't matter kwamba ck alikuwa boyfriend wa wema kajala ni mbaya sana sana ukizingatia kuwa hawa wawili walikuwa marafiki wa kufa na kuzikana

    ReplyDelete
    Replies
    1. WEWE UNAUJUA HUO URAFIKI WA KUFA NA KUZIKANA????????ACHA UJINGA. KAJALA HANA KOSA KABISA!!!

      Delete
  3. UWONGO MTUPU!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Tizama show yake ya in my shoe 14 analalamika mpaka anataka kuliya kajala kumchukuwa ck kutoka na kajala ck siyo mume wake yeye mwenyewe kamwiba bila ayibu nakutowa hadharani uyi ndiyo MISS taz anatowa kipindi kama icho anafundisha nini watoto kisha anasema niliachana na ck nikaenda kwa mwenye nilimpenda ndio diamond inamana ck hajampenda wala diamond hampendi yeye anataka wote wawe wake kweli ni KICHECHE

    ReplyDelete
  5. Haijalishi kuwa ni mume wa mtu au sio ukweli ni kwamba alikuwa bwana wa wema sasa kajala vipi asikumbuke fathila???

    ReplyDelete
    Replies
    1. NDO KAKUMBUKA FADHILA HELA ALIZITOA CK

      Delete
  6. Kajala wee piga kimya wazidi kuumia kichwa, raha sana pale mtu anapokuchokoza halafu ukaa kimya.

    ReplyDelete
  7. Ilo neno kajala kaa kimya.

    ReplyDelete
  8. Kajala piga kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  9. YES KAJALA KAA KIMYA!!!

    ReplyDelete
  10. Wape madonge yaovhao

    ReplyDelete

Top Post Ad