Maoni: Alikiba Atazidi Kupitwa kila Siku, Kama R Kelly Anakujua Why Dunia isikujue?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mi ni team Ali Kiba forever ila jamaa anazingua na sijui anajisikia au vipi maana kila siku anaambiwa hasikii kama atataka kushindana na Diamond naona kachelewa sana.

Katoa audio ya chekecha cheketua siku hizi video ndio inakutambulisha kimataifa kakaa kama mjinga fulani, Diamond katoa video ya nyimbo yake nyimbo ya kawaida sana Sema hafanyi kama Kiba kutanguliza audio. 

Dogo mjanja sana katoa video akijua itazidi kumtambulisha kimataifa. Naona Namibia, Ghana, Nigeria, Botswana wanacomment kuhusu video. Ali Kiba unalala tu.

Tuwe wawazi team Kiba Tunajua Diamond yupo juu Sema Diamond Hana kipaji kama Ali Kiba ila ukiendelea hivi utakimbiwa halafu dogo ana dharau ndo maana Hata instagram hajamfollow mtu yeyote.

Diamond big up ishu ni kujulikana kimataifa maana Tanzania umemaliza tayari Kiba ukitaka kuwa juu sikiliza mashabiki acha dharau na angalia soko linaendaje acha ujinga team Kiba tupo pamoja.

Ni ushauri maana tunataka ujulikane Dunia nzima kama R Kelly anakujua why Dunia isikujue? Jitambue.

By Vidodi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kiba naona sasa hivi hali mbaya, nilikwenda kwenye shoo yake moja alikuwa na mdogo wake London, shoo ilikuwa ni mbuzi sana na ilifanyika kwenye vijibaa vya waTanzinia London.sikutegemea yaani ni basi tu ni kama alikuja kutembea. si arena kama Diamond alikofanya shoo yake 02. Ali Kiba amekwisha hana tena story, anazidi kupoteza kipavi chacke pia ujivuni unamdondosha.. anaboa!!

    ReplyDelete

Top Post Ad