Q-Chillah,TID wataka kutwangana kisa,ngoma mpya ya Ali Kiba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mastaa wa Bongo Fleva,Q-Chillah na TID mwishoni mwa wiki hii walitaka kutwangana walipokutana katika Klabu moja usiku.
  
Kwa mujibu wa Q-Chillah akizungumza kwenye Uheard na Soudy Brown alisema kuwa alikwenda kwenye klabu hiyo kuangalia shoo iliyokuwa ikifanyika lakini baadaye aliamua kutoka nje kucheza ‘pool table’ ndipo alipomuona TID.

 

‘’Nilimuona jamaa(TID) akiniangalia na baadaye alinifuata akaniambia kuwa anataka kuongea na mimi nikamwambia ile siye sehemu yake atafute muda mwingine ndiyo tuongee,’’alisema Q-Chillah. 

 

Aidha Chillah aliongeza kuwa TID aliendea kumuongelesha ndipo alimwambia kuwa anachofanya kumuongelea yeye vibaya siyo vizuri na kile alichokipost hivi karibuni kuhusu kuuponda wimbo mpya wa msanii Ali Kiba uitwao ‘Cheketua’ aliouachia hivi karibuni kupitia account yake ya Instagram hakikuwa kitu cha busara ilitakiwa amsapoti kama msanii mkongwe kuliko kumponda hadharani kupitia mitandao.
‘’Kiukweli kitendo cha TID kuandika Instagram kuwa ngoma mpya ya Alikiba ni mbaya na baada ya miezi mitatu haitokuwepo siyo kizuri nilimwambia yeye ni msanii mkubwa inabidi kumsapoti Ali Kiba na kwamba nilitaka kumpiga kwa fimbo ya pool table siyo kweli nilikuwa nikimueleza tu,’’aliongeza Q-Chillah.

Kwa muda mrefu wasanii hao wawili ambao waliwahi kuwa pamoja kwenye bendi ya (Top Band) wamekuwa kwenye bifu zito wakitupiana maneno kwenye vyombo vya habari.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KWELI CHILA ULICHOSEMA NI SAHIHI KABISA

    ReplyDelete
  2. wote mateja wazee tuu walale mbele

    ReplyDelete
  3. BEAUTIFUL NA KIUNO"NGOMA IMELALA HAPO

    ReplyDelete
  4. NGOMA HAINA MPANGO

    ReplyDelete

Top Post Ad