Shirika la Tanesco Lakiri Kuwepo na Madudu Katika Mfumo wa LUKU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), limeshindwa kutoa huduma kwa wateja wake wanaotumia meta za LUKU kutokana na hitilafu iliyojitokeza katika mtambo wa kuuza vocha tangu Februari 27 mwaka huu. Anaandika Deusdedit Jovin

Tangu Ijumaa ya Februari 27, wateja wa TANESCO wamekuwa wakihaha kutafuta huduma ya LUKU bila mafanikio. Kuna matatizo ya aina tatu yameripotiwa na wateja wa TANESCO mpaka sasa.

Baadhi ya wateja waliojaribu kununua vocha kupitia kwa mawakala wa TANESCO walishindwa kupata huduma kwa kuwa mfumo ulikuwa hautoi majibu.

Wateja wengine walifanikiwa kununua vocha za LUKU kupitia simu zao za mikononi, lakini vocha hizo zikakataliwa na mita za TANESCO zilizosimikwa majumbani mwao.
Pia, kuna wateja waliojaribu kununua vocha za LUKU kupitia simu zao za mikononi lakini pesa ikakatwa bilakupatiwa vocha yoyote ya LUKU.
Kwa siku zote hizo hakuna taarifa iliyotolewa kwa umma kueleza tatizo lililopo,- hali ambayo iliwafanya baadhi ya viongozi wakiwemo mawaziri kulizana masawali yasiyo na majibu wakati wakiwa kwenye hafla ya kuaga mwili wa hayati Kapteni John Komba.
Msemaji wa TANESCO, Adrian Severin, alipoulizwa  kuhusu tatizo lililopo, alisema kuwa mfumo wao wa kompyuta unaotumika kuuza vocha za LUKU una matatizo tangu Ijumaa ya Februari 27.
“Ni kweli mfumo wetu wa kompyuta una matatizo. Tayari mafundi kutoka Afrika Kusini wako kazini kunusuru hali,” amesema.
Severin alieleza kwamba, mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wateja walifanya jitihada za kumtaarifu mtaalam aliyewauzia mfumo huu kwa ajili ya matengenezo. Mtaalam huyo alithibitisha kwamba mtambo ulikuwa na matatizo makubwa.
Alisema kwamba, mpaka Jumapili matengenezo hayo yalikuwa yanaendelea yakiwa yametatua nusu ya tatizo.
“Mafundi walifanikiwa kuuwezesha mtambo kuzalisha vocha kwa wateja wanaojaribu kununua kwa njia ya simu lakini vocha hizo zikakataliwa na mita za TANESCO,” alieleza.
Alipoulizwa kuhusu hatua walizochukua mafundi baada ya tatizo hilo jipya, alisema, “baada ya kupata taarifa hii mpya mafundi waliuzima kabisa mtambo ili kupata fursa ya kuuimarisha zaidi.

Alipoulizwa aseme kama TANESCO wanao mfumo kwa ajili ya matumizi ya dharula pale mfumo wa kawaida unapokuwa na hitilafu alisema, “security modules (program za kulinda usalama wa kompyuta) tulizo nazo hazina nakala ya dharula kwa hapa Tanzania”.
Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud, alipotafutwa ili aeleze ni kwa nini wizara iliiruhusu TANESCO kununua mtambo wa malipo ya LUKU nje ya nchi na kuacha usimikwe huko alikuwa mkali.

“Sisi wizarani tunatengeza sera tu. Mambo ya utendaji walize TANESCO,” alitamka kwa ukali.
Alipoambiwa kwamba uamuzi wa kutafuta huduma nje ya nchi na namna ya kuendesha huduma vinaongozwa na sera za wizara, alisema “hakuna mtambo uliosimikwa nje ya nchi. Nenda pale Ubungo Makao Makuu ya TANESCO utaukuta mtambo wa LUKU kwenye server room (chumba cha kompyuta kubwa).”
Hata hivyo, hapo awali, msemaji wa TANESCO Adrina Severin aliliambia gazeti hili kwamba sehemu ya mitambo ya LUKU iko Afrika Kusini na kwamba wataalam wanaoendelea kutatua tatizo hili wako kule kule sasa hivi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwa kweli hiki ni kimeo kingine kumbe kuna baadhi ya siku tautalalal giza wakati hela ya kununua umemem tunayo hii kali kuliko

    ReplyDelete
  2. kwa kweli hiki ni kimeo kingine kumbe kuna baadhi ya siku tautalalal giza wakati hela ya kununua umemem tunayo hii kali kuliko

    ReplyDelete
  3. Halafu utasikia oh bongo siku hizi kuna kila kitu namna hiyo umeme madawa na tiba hospitalini elimu mbovu kila siku ukisoma news za bongo ni kasheshe tu about this and that till when?

    ReplyDelete
  4. MAUOZO MENGINE YA SERIKALI

    ReplyDelete

Top Post Ad