CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mnamo tarehe 24/4/2015 huko maeneo ya Sogea Tunduma Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, METHEUS ANGANILE MWAFONGO, Mndali, 37yrs, Mkuu wa Ulinzi CDM Wilaya Momba, pamoja SALEHE TABLEI@SICHALWE, 22yrs, mkazi wa Majengo Tunduma walikamatwa kutokana na taarifa za kiintelijensia.
 
Watu  hawa walikamatwa wakiwa na buti pair 2 za kijeshi, kofia pair 2 za kijeshi, kamba kurukia ya mazoezi, vyuma kwa ajili ya mazoezi ya pushup, visu pair 2 kimoja spring knife na kingine kisu kikubwa, miwani ya FFU(ya kwenye misafara), manati pair 2 na mawe yake 40 pamoja na nati 4 zilizotarajiwa kutumiwa kama mawe, shenguard kwa ajili ya mikono na miguu pair 4, Bendera 2 za CDM, Tshirt 1 ya CDM, Kilemba 1, koti 1, Pamoja na barua 3 za CDM za kata ya MSANGANO, SHITETE, na KAMSAMBA (W) MOMBA zenye kichwa cha habari "UTOAJI WA VIONGOZI WA RED BRIGED KATIKA KATA YENU KWA MAFUNZO YA RED BRIGED".
 
Barua inasomeka hivi
Husika na kichwacha barua hapo juu chajifafanua vema.

Napenda kukujulisha kuwa kutakuwa na ziara ya kimafunzo ya RB (Red Briged) katika kata yenu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi wa kumi mwaka huu.

Na kwa barua hii naomba uwapokee na uwape ushilikiano wa kutosha kwa ajili ya maendeleo ya chama chetu.

Ni matumaini yangu kuwa utawapokea na kuwatunza pamoja na usalama wao.

Wako katibu wa chama Wilaya.
 
Katika mahojiano vijana hawa walikuwa wakienda kutoa mafunzo ya kijeshi katika kata tajwa na mpango wao ni kufundisha vijana 300 katika wilaya ya Momba na mpango huu ni wa mkoa na Nchi nzima chini ya Mkurugenzi wa Usalama Taifa CDM bwana LWAKATARE.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Intelligencia gani hiyo au aibu? kamba kurukia ya mazoezi, vyuma kwa ajili ya mazoezi ya pushup, visu pair 2 kimoja spring knife na kingine kisu kikubwa, miwani ya FFU(ya kwenye misafara), manati pair 2 na mawe yake 40 pamoja na nati 4 zilizotarajiwa kutumiwa kama mawe, shenguard kwa ajili ya mikono na miguu pair 4, Bendera 2 za CDM, Tshirt 1 ya CDM, Kilemba 1, koti 1 ni zana za kijeshi??? Duh...naona polisi bongo wako macho kufuatilia wapinzani lakini sio wezi wa EPA wala escrow

    ReplyDelete
  2. Sijawahi sikia polisi PUMBAFU kama wa bongo, ndiyo vifaa vya kijeshi hivyo? nyie ng’ombe kweli, mnaswagwa tu kama MAZUZU, mumejaza matumbo kichwani ZIRO.. mnaambiwa kamata pale, nenda kaseme hivi, hapa fumba macho …… kama mi-ng’ombe

    ReplyDelete

Top Post Ad