Wema Sepetu: Hata Aje na Bill Gates Kamwe Siwezi Mrudia Diamond, Kwanza Sitaki Kukumbuka Kabisa Kuhusu Huyu Mtu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KIAPO! Kuonesha kwamba hana mpango wa kurudi nyuma, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amefungukia msimamo wake juu ya mwandani wake wa zamani, Wema Sepetu ‘Madam’ kwa kusema kuwa kamwe hawezi kumrudia tena, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili

Licha ya Diamond kufunguka hayo, wawili hao wamekuwa na mapenzi ya vipindi, kuna wakati waliwahi kumwagana kisha kurudiana na hakuna aliyewahi kutoa tamko zito lakini safari hii Diamond amesema ndiyo basi tena!

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na staa huyo, mara kwa mara Diamond amekuwa akijiwekea nadhiri ndani ya moyo wake na kusisitiza kwamba pamoja na kuwa maisha ya sasa huendeshwa kwa msingi wa fedha lakini hata kama ‘atafulia’ kiasi gani, ni bora afe maskini kuliko kurudiana na Wema.

“Diamond amekuwa akisema kila wakati kwa msisitizo kuwa kutokana na matatizo aliyokumbana nayo katika uhusiano wake kwa Wema, ni vigumu sana kurudiana naye wala kuwaza kama ipo siku anaweza kuwa naye, maana hakuna tena jambo geni asilolijua kwake,” kilisema chanzo hicho na kufunguka zaidi:

Kama hiyo haitoshi, Diamond anasema anaposema haoni kitu kipya  kwa Wema anamaanisha ndiyo maana utaona leo hakuna hata siku moja ambayo amewahi kuwaza kurudiana naye hata kama atatumia ushawishi wa fedha kwa kumpelekea makontena ya fedha, hawezi kukubali anasema bora afe maskini kuliko kushea kitanda kimoja na Wema.

DIAMOND ATHIBITISHA
Baada ya madai hayo, Risasi Jumamosi lilifanya jitihada za kukutana na Diamond uso kwa uso ambaye alithibitisha taarifa ambazo zilielezwa na mtu wake wa karibu:

Umeambiwa na nani hayo? Sipendi kuongelea sana hivi vitu lakini huo uliousikia ndiyo ukweli. Kwa sasa nawaza maisha yangu na mpenzi wangu Zari baada ya kupitia majaribu mengi kimapenzi enzi hizo.
“Huenda wengi wasiamini ninayosema lakini nafsi yangu haijawahi kuniongoza kukumbuka ya nyuma tena kama ilivyowahi kutokea awali.

Wengi wamekuwa wakiniuliza swali kama hili lakini sikupenda kujibu kwa kuwa nilihisi litaleta tafrani kwa mashabiki wangu, sioni sababu ya kuendelea kuulizwa kwenye media hivyo ukweli ni kwamba siwezi kurudi nyuma tena,” alisema Diamond


ASISITIZA KWA KUREKODI WIMBO
Kuonesha kweli amedhamiria kutogeuka nyuma, Diamond alisema kwa sasa yuko bize studio kurekodi wimbo na Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki) ambao utakuwa umesheheni majibu ya maswali yote ya kila kitu ambacho kilimkera kwenye uhusiano wake na Wema.“Naomba mashabiki wangu wawe na subira kwa maswali hayo yote, majibu yake yatapatikana katika project yangu na Nay inayokuja muda si mrefu,” alisema Diamond.

WEMA AJIBU MASHAMBULIZI
Alipotafutwa Wema kuhusiana na kauli hiyo ya Diamond, naye alijibu mashambulizi kwa kusema kamwe hawezi kurudiana na Diamond, hamfai hata kidogo na hata akimshawishi na  fedha nyingi kiasi gani hawezi kurudi nyuma.

Hata aje na Bill Gates (tajiri mkubwa duniani), aje na matajiri wote anaowajua yeye duniani kamwe siwezi kulamba matapishi, kwanza sitaki kukumbuka kabisa kuhusu huyo mtu, please naomba nisimuongelee kabisa huyo mtu,” alibwatuka Wema.

WAMEFIKAJE HAPA?
Wawili hao ambao walidumu kwenye uhusiano na kupamba vyombo mbalimbali vya habari, kila mmoja amekuwa akimtuhumu mwenzake kuwa msaliti lakini sababu kubwa ambayo Diamond amekuwa akiisimamia juu ya kummwaga Wema ni baada ya mrembo huyo kuhongwa gari na mwanaume mwingine.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wote Malaya tuu

    ReplyDelete
  2. Si bora wema hajakupachikia Mimba endelea kumtungia nyimbo kuna Siku na saa utaumbuka wewe Malipo hapa hapa duni

    ReplyDelete
  3. Hivi the fact kwamba huyo ajuza alirecord ngono Daimond anajifanya kasahau?Zari is more of a bitch than Wema.Colour hiyo anaji modify kwa sindano,so sit down Dimond and enjoy with ur ajuza usituletee misifa ya kijinga.

    ReplyDelete
  4. Yes she is pregnant but are you sure the baby is yours?

    ReplyDelete
  5. HUYO DOMO ALIAMBIWA WEMA ANAMTAKA? AU ANAANZA KUTAMANI KAISHA YAKE ALIVYOKUWA NAE ALIMFUJA NA WEMA ALIKUWA HAFANYI CHOCHOTE ZAIDI YA KUMPANDISHA KWENYE STEGI. LEO KUMPATA ZEE LA UGANDA NA KUDANGANYWA MIMBA NIYAKE ANAONA WEMA MMBAYA, TUSUBIRI ATAKAPOACHWA NA ZARI NAE ASEMA MABAYA YAKE.

    ReplyDelete
  6. tushamzoea Diamind akiachwa na dame anajifanya hana kosa, inamaana kila demu kamkosea yeye? haache uongo Wema anamazuri yake tena alimtumia sana mpaka watu walipiga kelele,

    ReplyDelete
  7. kwakuwa kapata alichokipata leo anamuona Wema hafai? kweli mfadhili mbuzi. na cku akiachana na Zari nae atasemaje? au kaona hiyo mimba ndo kashafika kwa bi kizee hahaaaaaa, kaingia choo cha???

    ReplyDelete
  8. NASSIBU ASIJIONE KAFIKA KWA ZARI, AKAANZA KUMTUKANA WEMA, AU KAMUONA SWT WEMA YUKO JUUU, SASA ANAANZA KUROPOKA? ASITAFITE UMAARUFU KWA KUMTAJA WEMA. ATULIE NA ALEE MIMBA ZA WENGINE.

    ReplyDelete
  9. hana lolote anaona ameanza kwisha anatafuta wa kumpaisha, anafikiri Wema bado kalala pole yake arudi kwa mganga wake

    ReplyDelete
  10. mimba yenyewe si yakwake halafu analeta kashafya za kijinga, Wema anafanya yake, sasa kaona hamtaji anaanza kutafuta kiki, umedoda Domo usitafuteumaarufu kupitia kwa Wema huna jipya.

    ReplyDelete
  11. Kama hana habari naye anamtungia nyimbo za nini? Ukimuona mwanaume kutwa haishi kukutaja mdomoni mwake hata kama mmeachana ujue huyo mwanaume anakutaka bado na anaumia sana kukuona uko happy na maisha yako.

    Wee Diamond kama kweli humtaki Wema na wala huna haja nae acha kumuimba imba kwenye nyimbo zako na kumtaja taja Hovyooo mwanaume mzima usiejua kuna kupendana na kuachana. Sasa na wewe wanawake zako wakianza kukuimbia nyimbo utapona kweli?

    Halafu na huyo mwanamke aliyenae sasa ni zuzu kweli, mie siwezi kukubali bwana wangu kila siku akae anamuongelea X wake au anamuimba X wake najua tu moyo wake bado uko kule. Kama amemove on amuimbe sasa na kumsifia huyo Zari wake mbona anatosha sana kujaza mistari. Au anaogopa akimuimba Zari nyimbo zake hazitauzika?

    ReplyDelete
  12. DIAMOND ONYESHA UANAUME WAKO KWA KUACHA KUMFUATAFUATA WEMA KWA NYIMBO, MAFUMBO, MICHAMBO NA MANENO.

    AU BILA YA KUMUIMBA WEMA HUUZIKI? UNATAKA KUTWAMBIA KUWA THERE IS NO DIAMOND WITHOUT WEMA? HAHAHAHAAAA DOGO MUIMBE ZARI SASAYA WEMA YAMESHAPITA.

    Ukimuimba this time akikupeleka TCRA na ushahidi huo hapo wa interview yako anaweza kukufilisi mali zako zote, kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Muimbe Zari sasa ndio zamu yake na yeye ya kuuza, au hata umuimbe mama yako na baba yako mzazi mpumzishe mwana wa mwenzio hata hana habareeee na wewe hahahahahaaa

    UNATAFUTA KIKI KUPITIA JINA LA WEMA USHACHUNDA KWELI KWELI

    ReplyDelete
  13. Lea Mimba badaye uje upokonywe mototo rubbish na ujanja wote umenasa kwa Malaya wa UN. Kisa mtoto unafikiri wako subiri kuumbuka.
    Kazi kumchafua wema mbona yeye hakuchafui ?mtungie zari Wimbo si ndio unayempinda?bila kutunga Wimbo unaomuhusu wema unajua huwezi kutoka I hate u

    ReplyDelete
  14. Tuna subiri Wimbo ututungie Wimbo ulivyopachiwa Mimba. Tuna subiri kwa hamu!umeishiwa ujanja wote unalea Mimba sio yako?

    ReplyDelete
  15. kama kweli wewe una nyota mtungie Zari na mimba ya kusingiziwa uone kama utauza. muwache Wema kashakufanyia mengi mazuri mpaka ukapata vikombe 7 mwaka jana umesahau? au unaanza kushuka na mialiko ya uk na us nayo inayeyuka unaona uanze kumtaja Wema, wapiiiiiiiiiiiiiii.

    ReplyDelete
  16. Hii gemu uliyoingia na rich gang itakufundisha Adabu!,,, utakuja unaheshimu wan awake

    ReplyDelete
  17. thats true, gemu ya rich gang inamuangalia tuu domo iko cku mashauzi yoote atayasahau, anafikiri wamekaa kimya?

    ReplyDelete
  18. Hivi hawa ndugu zako wanaokupenda hawakushauri? Manake naona soon utakua history,asiyefunzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu

    ReplyDelete
  19. DIAMOND STOP USING WEMA AS YOUR LEDDER TO CLIMB TO YOUR DESTINATION TAFUTA NYIMBO ZAKO ZA MAISHA YAKO YA UMALAYA YA KUTEMBEA NA WASANII DUNIA NZIMA WEMA BORA UMEACHANA NA MTU HUYU ASIEJUA MAPENZI YA KWELI KWA ZARI AMEFATA PESA TU AKIENDA KUPIGA SHOW SEHEM YOYOTE ATAWACHUKUA TU KM KAWAIDA YAKE HANA LOLOTE NGOJA WAOANE UTAONA KAMA MUME ALIEZAA NAE WATTOTO WATATU KAPIGWA CHINI ITAKUWA WEWE MVUTO WENYEWE HUNA WEMA YANI DIAMOND KAMA DEREVA WAKO REALLLY HAMFANANI KABISA

    ReplyDelete

Top Post Ad