Habari zaidi Kuhusu Watu 9 Waliokamatwa Msikitini na Silaha, Milipuko, Majambia na Bendera ya Al Shaabab Morogoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limekamata watu 9 wakiwa na silaha za kulipua na nguo za jeshi la wananchi wakiwa wamejifungia katika msikiti wa Suni Kidatu wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema tukio la kukamatwa kwa watu hao limekuja kufuatia jeshi la polisi kupata taarifa za uhalifu ambapo jambazi mmoja aliruka katika bajaji na kisha kumjeruhi askari shingoni ambapo wananchi wenye hasira kali walioshuhudia tukio hilo walimkimbiza jambazi huyo akiwa na silaha na kisha kumchoma .

Kamanda Paul amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi liliongeza nguvu ya askari ambapo walifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine wakiwa katika msikiti wa Suni Kidatu na baada ya kupekuliwa wamekutwa na vifaa vya milipuko nguo za kijeshi la wananchi wanaendelea kuwashikilia watuhumiwa na kuna taarifa kuwa watuhumiwa hao walijiandaa kufanya tukio la uhalifu .

Aidha kamanda paul amewashukuru wananchi wa ruhembe kidatu wilayani kilomeroa mbao wametoa ushikiano kufanikisha kukamtw akwa watuhumiwa hao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya mambo mengine wala sio Dini, hasa mambo mabaya yanayokatzwa kila siku, ila wanapitishia kwa misahala ya dini, ili wawapate wengi, waharifu, dunia ya sasa inabidi mtu kuwa makini sana, la sivyo waweza dumbukia pabaya, baadhi ya watu hapa ulimwenguni wana dhiki zao na intrest zao, na njaa zao basi watatafuta la kutafuta waweze kutoka na kujimalisha kwa kujipatia wafuasi kwa kuwa uwelewo wao ni mdogo, lakini si maswala ya ya dini, ukiangalia Yemeni mbona wanamwagana damu wenyewe kwa wenyewe, na wote ni wafuasi wa dini mmja, sasa kwa nini? wanauwana wakiwa kwenye nyumba za Ibada misikitini? na wote ni wa dini mmja, sio maswala ya dini ni Intrest zao wenyewe. Ndio zinazotupeleka pabaya, ifike wakati tutumie Imani zetu za dini vizuri katika jamii zetu

    ReplyDelete
  2. Wasituharibie dini zetu.. tutafanya kila njia kuwatokomeza

    ReplyDelete

Top Post Ad