HAWA wa Nitarejea Afunguka "Wimbo wa Nitarejea wa DIAMOND Nauchukia Sana Umeniharibia Maisha Yangu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Unakumbuka Video ya Nitarejea ya Diamond? Basi yule msichana aliyeshirikiana naye katika huo wimbo hali yake si nzuri kisanii na kimaslahi pia kiasa cha kusema kuwa anauchukia huo wimbo kwani ndo umemuharibia Maisha
Hawa akihojiwa na Mlimani TV amefunguka na kusema kuwa Pamoja na Wimbo huo kuwa ndio uliomtoa Diamond Kimuziki lakini Diamond hakuwahi kumpa Hata Shiling 10 , Japo ameshawahi kumfuata na kumuomba msaada wakati tofauti tofauti lakini haikuwezekana kupata huo msaada ....Hawa amesema alitegemea nae angetoka lakini ameishia kuwa na maisha ya Dhiki huku mwenzake akitengeneza Hela za Maana ..

Alipoulizwa Kuhusu tuhuma za kutumia Madawa ya Kulevya baada ya kuona mambo hayaendi vizuri  Hawa amesema hakuwahi kutumia Madawa ya Kulevya bali alijiingiza katika unywaji wa pombe sana baada ya Mwanaume aliyempa Mimba Kumkimbia hivyo alianza matumizi ya pombe kupunguza Mawazo ..

Hawa anasema Hamchukii Diamond ila Anapenda kumwambia akumbuke alipotoka na Arejee Nyumbani....
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAWA ULUKUWA HUMJUI DIAMOND, MWANAMKE AKIMSAIDIA NA AKIPATA ANACHOKITAKA ANAMTOSA NA KUANZA KUMZUSHIA KILA BAYA. DUNIA NDO HII IKO CKU.

    ReplyDelete
  2. Aisee, nasib si vizuri ulivyofanya kumbuka kua mtu mwema

    ReplyDelete
  3. Hawa mi naujua vizuri sana uwezo wako katika uimbaji! We unaweza kufanya kitu ktk muziki na watu wakakuelewa, achana na mtu ambae alitumia kila njia kufikia alipofikia na we wajua fika Kuwa Huyo kwako harudi tena, Jipange Fanya Kazi na utafanikiwa

    ReplyDelete
  4. Haya na huyu nae tusemeje? Diamond ni mdhalilishaji na mharibifu, amlipe tu dada wa watu haki yake.

    ReplyDelete
  5. Hiv huyo mwanamke ushapata shavu lakushirikishwa na nyimbo ime tamba na bado iko vizur unadhindwaje kuji saidia mwenyewe kwakutoa nyimbo kali booster usha pata unataka msaada upi tena

    ReplyDelete
  6. Kwanza niiweke wazi Diamond ni bahili sana nakumbuka dada yake Esma alipoolewa aliandika kwenye insta Kuwa hongera dada angu nikirudi toka safari tegemea booonge la zawadi mbona hakumpa.Nina hakika angempa kwa alivyo mpenda sifa kila mtu angeiona magazetini

    ReplyDelete
  7. kweli kabisaaa, Diamond akitaka kitu kwa wanawake atatumia nguvu nyingi kumsifia akisha kipata sasa ni ubaya kwa kwenda mbele, hasa asante hakuna.

    ReplyDelete
  8. KWANI MTU UKIMPALIFT YA GARI BASI AKAKUSAIDIA NJIANI ULIVYOKWAMA,LABDA PENGINE TRAFIKI ALIEKUKAMATA ANAMFAHAMU. BASI WEWE SASA UTAKUWA HUTOKI BILA YEYE NA HUWEZI KUNUNUA GARI NYINGINE LAZIMA UMKUMBUKE KILA UNAVYOZIDI KUNUNUA MAGARI NAE UMNUNULIE, AKUMBUKE NYUMBANI WAPI ? MBONA MNAPENDA KUMCHAFUA SANA DOMO MNATAFUTA SABABU KILA SIKU !!!! HAYA BASI HATA MTU AKICHEKA NAYE UTASKIA MIMI NDO MWANZO WA FURAHA YAKE BILA MIMI ASINGEKUWA NA FURAHA MWEH MWEH JAMANI ACHENI HAYO YAANI NAKERWA UTASIKIA NILISOMA NAE AMEPATA HATUANGALII WENZAKE . KUSOMA WOTE NDO NIWE NAKUPA MAHITAJI YAKO YOTE CHANGAMKA JITUME KAMA UNAUWEZO WA KUIMBA IMBA

    ReplyDelete
  9. Sasa waungwana kwan hakukuwa na business terms kabla ya project? maana ni kama huyu dada aliokotwa na kupelekwa location bila kujielewa. Ilibid lazima ajue atalipwaje na kwa utaratibu upi. kwani ikiwa hivyo kila atakaeshiriki kwenye kazi ya msanii akataka aendelee kubebwa msururu utaanzia jangwani mpk kimara..this is bull shit tumia kipaji chako utafika mbali

    ReplyDelete
  10. ADMINI UKIONA WATU WANAMPONDA HAWA HUTOI KOMENTI ZAO. AHHAAAAAA NIMEKUELEWA. HUZIRUSHI BASI NIWEWE UNAMPONDA KWANI NILISHANGAA KUONA HIZO JUMBE ZINALALIA UPANDE MMOJA

    ReplyDelete
  11. Daima diamondd atakuwa juu hata mumchafue vipi,kwani anaejua anajua tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad