google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Jeshi la Kenya Lafanya Shambulio Somalia Kulipiza Kisasi Baada ya Al Shabaab Kuuwa Wanafuzi 148 Kenya | UDAKU SPECIAL

Jeshi la Kenya Lafanya Shambulio Somalia Kulipiza Kisasi Baada ya Al Shabaab Kuuwa Wanafuzi 148 Kenya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab katika taifa jirani la Somalia ,msemaji wa jeshi ameiambia BBC.

Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza.

Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo.

Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki iliopita

.Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.
Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya jumapili usiku katika eneo hilo.
Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani wanagombania kitu gani

    ReplyDelete
  2. Uuuwiii!! Mauaji kila siku...
    Sasa tusubirie na al-shababu kujibu mashambulizi..
    tafuteni njia nyingine ya kusuluhisha hayo mambo la sivyo Kenya itageuka nchi ya wakimbizi.

    ReplyDelete

Top Post Ad