Kundi lingine la watoto limekutwa kwenye misikiti ya mji wa Dodoma

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kuna tetesi kuwa kuna kundi la watoto zaidi ya mia, wengine wakiwa na miaka mitatu tu,wamekutwa kwenye misikiti mbali mbali ya mji wa dodoma. Wengi wakitokea mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Betty Mkwasa alisema jana kuwa aliyoyaona katika kituo hicho hayakubaliki.

“Kwanza watoto wanalala wengi, hakuna hewa ya kutosha, wanajipikia wenyewe chakula na hawana uangalizi wa watu wazima,” alisema Mkwasa.

Alisema serikali haikatai dini yoyote kufundishwa kwa watoto bali taratibu, kanuni, sheria pamoja na haki za mtoto lazima zifuatwe.

“Siwezi kujua walikuwa wanafundishwa nini lakini baada ya upembuzi yakinifu utakaofanywa na wataalam ambao nimekuja nao, tutaweza kuzungumza kama walifuata kanuni na utaratibu,” alisema.

Mwananchi ilipofika katika moja ya kituo hicho, jana asubuhi lilikuta watoto hao wakicheza kwenye eneo hilo lililokuwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa na silaha za moto.

Watoto wengi walikuwa hawajavaa viatu na baadhi yao walisema kuwa viatu walivyokuja navyo kutoka makwao vimeshakwisha.

Bakwata

Sheikh mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaaban Rajabu alisema wanakitambua kituo hicho kama ilivyo kwa vituo vingine vinavyofundisha dini ya Kiislamu.

Sheikh huyo alipinga suala la watoto kukosa elimu, akisema wazazi wao wamehiyari vijana wao kusoma dini tu.

“Naomba ifahamike kuwa, wapo wazazi ambao wanapenda watoto wao wasome dini tu na hata mimi nilisoma hivyo kabla ya kwenda nje kwa masomo zaidi na kurudi,” alisema.

Alipinga suala la kusajiliwa kwa kituo akisema viko vituo vingi havijasajiliwa hata katika dini nyingine, lakini havisumbuliwi na kushangazwa kuona utaratibu wao unakuwa na shida.

Kwa upande mwingine alishauri Bunge kutunga sheria kali kwa ajili ya kuvilazimisha vituo vyote kuwa na usajili ili viweze kufuatiliwa kulingana na matakwa ya serikali.

Kwa upande wake, katibu wa Bakwata mkoani hapa, Hassan Kuzungu, aliyeongozana na kamati hiyo, alieleza kusikitishwa na kitendo cha mazingira waliyokuwapo watoto hao.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nkhungu, Kasian Mponela alisema kuwa amekuwa akiwaona watoto hao, lakini hajui wanachojifunza hapo.

Alisema suala la kuangalia kama wanajifunza dini au mambo mengine sio jukumu lake, kwani yeye anajua kila mtu anapanga mwenyewe matumizi ya nyumba yake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ama kweli CHUKi Za MAKAFIRI zimedhihiri.

    ReplyDelete
  2. Hii ni nchi huru, uhuru wa kuabudu lazima uheshimiwe na kusoma dini ni sehemu ya ibada hiyo, mbona mnawafuata fuata sana waislam? au ndiyo ile falsafa ya ukitaka "kumuua mbwa" anza na kumpa jina "baya" la mbwa mwizi ili ukianza kumpiga watu washangilie???

    ReplyDelete
  3. Imeshathibitika chuki na bughdha..."Na yaliofichikana katika nafsi zao ni makubwa zaidi".......

    ReplyDelete
  4. hivi hii serikali dini gani au mfumo kristo ndiyo huo kuna makanisa mangapi hapa nchini yanalea watoto wadogo wenye mwezi mmoja na kuendelea

    ReplyDelete
  5. Mini nadhani ni busura kwa watoto kufundishwa elimu ya dini na elimu dunia kwa wakati mmoja kama ilivyo kwa makanisa mengine. Faida ya kufanya hivi ni kwamba baada ya watoto hao kukua wataamua njia iwapasayo ama kuendelea na majukwaa ya kidini au kusaka maisha kupitia elimu dunia.

    ReplyDelete

Top Post Ad