Lulu: Sina cha Kusema Wala Tamko Kuhusu Kifo cha Seki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kufuatia kuhusishwa na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu Bilionea Lusekelo Samson Mwandenga ‘Seki’ aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita, Staa wa Bongo Movies Elizaberth Michael ‘Lulu’ amesema hana la kusema na hana tamko lolote fufuatia kifo cha Seki.

Akiongea na gazeti la Ijumaa Wikienda Juzi, lililotaka kujua taarifa za yeye kuhusishwa na bilionea huyo pamoja na mambo mengine, Lulu alijibu kwa kifupi;

Mwandishi: “Lulu kwanza tumesikia unaumwa na umelazwa, ni kweli?”

Lulu: “Siyo kweli, mimi mbona nipo tu hapa nyumbani.”

Mwandishi: “Kuna manenomaneno kuhusu kifo cha Seki, watu wanakusema vibaya mitandaoni. Je, unatoa tamko gani?”

Lulu: “Sina tamko lolote.”

Mwandishi: “Lakini ni mtu uliyekuwa unamfahamu au alikuwa mpenzi wako?”

Lulu: “Sina cha kusema mimi na sina tamko lolote.

Gazeti hilo lilipojaribu kumbana kwa maswali zaidi kuhusiana kuwa na uhusiano na bilionea huyo, kutofanyika kwa bethidei yake na kufuta akaunti ya Instagram, Lulu hakuwa tayari kujibu lolote.

Marehemu Seki ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa madini, Arusha na Dar ameacha mke na watoto wawili.

Mwili wake ulitarajiwa kuagwa jana katika Kanisa la KKT, Wazo-Hill jijini Dar na kusafirishwa mjini Dodoma kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika leo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JAMANI HEBU MWACHENI MTOTO WA WATU MBONA MNAMSAKAMA SANA ?? KHA ONENI AIBU BASI.

    ReplyDelete
  2. Nayeye haone AIBU kubeba waume za watu mchana kweupeee

    ReplyDelete
  3. Aibu yy ndio maisha aliyochagua kuishi je afanye je? hapa Lulu umepata fundisho la ukubwani kabisaa u mzuri lakini wewe hapana aisee duu nadhani hata kidume kilichowahi kukulamba hakika kinaanza kujiuliza who next!

    Sasa la Segerea lilikuwa dogo kubwa lao ndio hili na ukicheza cheza utaibua la karne tulia ukae chini mama uu mzuri ila sasa sidhani kama huo uzuri wako utakusaidia kamwe

    ReplyDelete
  4. mwanamke mchafu kazi kutembea na waume za watu, hujui mali zao wamezihangaikiaje wewe unaingilia tuu, kilichobaki kufanyiwa maombi Mwenyezi Mungu akuadhibu tena akupe pigo la aina yake uteseke kwelikweli

    ReplyDelete
  5. MHUKUMU NI MUNGU TU.

    ReplyDelete

Top Post Ad