Majibu ya DNA Test Aliyoifanya NAY WA MITEGO Kubaini Kama Mtoto Aliyezaa na SIWEMA ni Wake Ama Laa Yametoka..Majibu Haya Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya utata mzito kutawala kwenye vyombo vya habari juu ya uhalali wa mtoto wa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mzazi mwenzake Siwema Edson, hatimaye kipimo cha vinasaba (DNA) kimetoka na kumaliza ubishi kwamba mtoto huyo aitwaye Curtis ni damu halisi ya msanii huyo.

Hivi karibuni, Nay na Siwema ambao walikuwa wapenzi kisha kumwagana, waligombana na kila mmoja kuzungumza lake juu ya mtoto wao huyo ambapo Siwema alidai si damu ya Nay wakati msanii huyo alisema ni damu yake.

Licha ya kupokea majibu hayo mazuri kwake, Nay aliyachukua majibu hayo kwa kuangua kilio cha furaha huku akieleza ya moyoni kuhusiana na sakata hilo.

“Hili ni swala ambalo lilikuwa linaniumiza kichwa kila kukicha. Unajua kama mwanaume, mtu akwambie mtoto si wako unadhani ni maumivu kiasi gani utayapata? Inauma sana, mtu umelea kuanzia mimba hadi mtoto amezaliwa, si kitu kidogo.

“Namshukuru Mungu kwa majibu kwamba ni damu yangu. Mashabiki wangu watambue tu kwamba, Curtis ni mwanangu asilimia mia hivyo hakuna ubishi tena.

“Ujue nampenda sana mwanangu na kwa bahati nzuri huyo ndiye mwanangu wa kiume pekee, hivyo sikutaka kuruhusu wazo lolote kutoka kwa mtu mwingine maana hata kama majibu yasingesema kama ni wangu nilikuwa radhi kuishi naye na kumlea bila kujali hilo kwa sababu tu niliamini siku zote ni mali yangu,” alisema Nay.

Nay aliingia kwenye utata huo takriban mwezi mmoja uliopita baada ya kupishana kauli na Siwema ambaye alimfumania akiwa na mwanaume mwingine nyumbani kwake, jijini Mwanza na kuamua kumchukua mtoto kisha kuishi naye jijini Dar kwa msaada wa mama yake mzazi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hongera sana kwa uwamuzi uliofikia mpaka umepata ukweli mtoto wetu. sasa lete mambo mengine ili siwema ajue kama mtoto ni wa ney na yeye nafasi hakuna tena kwako

    ReplyDelete
  2. Ungemlea Terry!!
    mnafki mkubwa

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  4. huyu mama mjinga, siye tumeolewa na watoto, lakini waliotuoa wanajua baba wa watoto tulionao. usithubut kumpa mtoto baba asiye wake. mwambie mtoto baba yako yupo huyu ni baba wa kukulea, hata kama baba yake hakutoa sapoti katika makuzi na malezi.

    ReplyDelete
  5. Bila shak kwanza mmefanana, sema kwa kuwa binadamu wanamidomo mirefu ni heri kuyamaliza kuwafumba hiyo midomo yao, sasa uwe baba bora kwa watoto wako wote bila ubaguzi, wa kuchagua huyu wa kiume dume langu na hawa ni wa kike sio midume yangu huo ni ukosefu wa kujua binadam tumeumbwaje kibaology, wote ni sawa, upatikanaji wa mwanamke au mwanaume ni ule ule, sasa uwapende watoto wako wote na kuwaeshimu na malezi bora kwa wote, watakuwa watu wazuri, bila kusahau elimu bora

    ReplyDelete
  6. jaman zamani watu walikuwa wanasema kuwa mama wa mtoto ndiyo anamjuwa babake ila science imeprove watu wrong kuna kundi kubwa la akina mama ambao mababa wanaowajuwa ndio baba za watoto wao sio!

    ReplyDelete
  7. KWELI KABISA MTOTO KAFANANA JAMANI TULIOGOPA KUSEMA MWANZO TUSIJE HARIBU MAMBO. LAKINI DNA YA MACHO NAYO INASEMA MTOTO NI WAKOO.

    ReplyDelete
  8. WAZALISHE KAKA USISIKILIZE HAO WASENGE SI WENYEWE WANACHANUA MIGUUU, WAPACHIKE

    ReplyDelete

Top Post Ad