google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Makanisa Mengi ya 'KIROHO', ni Biashara Isiyo na Hasara | UDAKU SPECIAL

Makanisa Mengi ya 'KIROHO', ni Biashara Isiyo na Hasara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni uwekezaji kama ilivyo biashara nyingine yoyote yenye wamiliki kisheria na wanahisa pia
Kinachofanyika ni rahisi sana una karama ya kuhubiri na kukariri vifungu vya Biblia takatifu, muongeaji mzuri unakaa chini na wadau mnatengeneza plan ya gharama za uanzishwaji na uendeshaji! Mnagawana majukumu , washika dau wanatoa mtaji wa kianzio na kanisa linaaza

Sasa kwakuwa lengo kubwa ni kutengeneza pesa/faida basi mahubiri yote msisitizo unakuwa kwenye kutoa. Na mara nyingi watu maarufu wenye nyadhfa na madaraka kwenye kada mbalimbali wakiwemo matajiri na wasanii hutumika kama chambo cha hadaa na kuwavuta wengine 

Ni nadra saana kukuta mtu wa kawaida asiye na kitu amekaa mstari wa mbele, nafasi katika haya makanisa hutegemea wewe ni nani na una bei gani

Miaka ya nyuma wakati ule taasisi za kidini zikiwa na misamaha ya kodi, makanisa haya yalitumika sana kufanya biashara. Zinaingizwa mali bila kodi kisha zinauzwa kwa bei ambayo imelipiwa kodi! Ndio kipindi kile ambapo viongozi na matajiri wengi walikuwa wakionekana kwenye ibada za haya makanisa

Makusanyo ya sadaka kwa kanisa moja tu kwa ibada moja si chini ya milioni tano ukitaja kwa kiwango cha chini kabisa kwahiyo kwa mwezi mmoja tu ana uhakika wa kutengeneza milioni 20 kwa uchache kabisa

Sasa ili kuendelea kupata waumini wengi zaidi na kuwa na mvuto wengi wao huingia mpaka kufanya mambo ya ki shetani ulozi na uganga! Mambo yafanyikayo huko yanatisha lakini kwao si tatizo 

Kwenye haya makanisa hakuna huduma ya bure hata moja na wengine wamechapisha kabisa mchanganuo na gharama kwa kila huduma

Makanisa yetu haya mengine tunaona yanavyoisadia jamii kuanzia afya mpaka elimu na huduma nyinginezo lakini si makanisa haya ya mitume na manabii

Imani ni kitu kizuri sana lakini imani bila fikra ni mzigo na upofu mkuu, watu wanatajirika kwa kupitia vichwa vya wapumbavu ni wakati wa kubadili ka sasa na kuona mambo katika uhalisia wake
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu umechambua vilivyo kabisa maana hawa jamaa wanapiga pesa ndefu na hata kutoa dharau kwa maaskofu wenzao wasio na tabia hizo mfano ni hapo juzi tuliona jamaa mmoja akitoa lugha kali kwa baba askofu mzoefu na mwenye heshima kubwa Tanzania.
    Yaani ukitaka pesa wewe anzisha kanisa la kiroho utakuwa tajiri mara moja kwani principle yake ni kuwa 'wajinga ndio waliwao'.
    Huku Dodoma kuna mwarabu mmoja anaitwa Abdallah Saleh yeye ameanzisha kanisa maeneo ya maili mbili na watu wanafurika hapana mchezo,jamaa alikuwa hoehae sasa anatembelea Rangelover Sports.Wanatumia mahubiri ya uongo kwamba wanaponyesha wagonjwa wakati kila kukicha vifo vinatokea kutokana na wagonjwa kuwa wengi yaani hata huyu jamaa anayehojiwa na polisi anaumwa kisukali na presha na sasa hivi anatembelea ktk kiti cha wagonjwa wakati yeye anadai kuwaponesha wenzie magonjwa,aibu kubwa sana.
    Nawasihi sana acheni kutapeliwa wakati uchumi wenu ni mdogo huku mkiwaneemesha wenzenu wakanunua madege,magari ya kifahari nk.Kama kweli wanafufua wafu basi kwanini hawakumfufua Moses Kulola aliyekuwa mstari wa mbele kufufua wenzie?
    Jitambueni sio kila goti litapigwa kwa bwana mengine yatatupwa nyuma ya shetani!

    ReplyDelete
  2. HATA YESU ALIKEMEA BIASHARA KWENYE NYUMBA ZA MUNGU,,LAKINI DUNIA TUNAYOISHI SASA IMEKWISHA MANAKE WAJINGA TUKO WENGI

    ReplyDelete
  3. Hahaaa amkeni badilisheni dini hiyo siyo mnatumiliwa tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad