MALI ZA GWAJIMA ZAANIKWA: Akisiwa Kuwa Mchungaji Tajiri Afrika!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sakata la Gwajima limechukua sura mpya baada ya mchungaji huyo kutakiwa na jeshi la polisi kupeleka nyaraka mbalimbali zinazohusu umiliki wa mali zake!

Mchungaji Gwajima katika kupingana na amri hiyo halali ya jeshi la polisi, amekimbilia kwa mawakili, ili tu kuweka pingamizi la yeye kuthibitisha umiliki wake wa mali alizonazo na namna alivyozipata.

Itakumbukwa kuwa jeshi la polisi lilimtaka Gwajima apeleke nyaraka zifuatazo: Hati ya usajili wa kanisa lake, namba ya usajili wa kanisa lake, hati ya umiliki wa helikopta, hati za nyumba anazomiliki, idadi ya makanisa yaliyopo chini yake na taarifa za mapato na matumizi ya makanisa yake.

Nyaraka zingine ni: majina ya bodi ya udhamini wa kanisa na waraka wa maaskofu uliosomwa makanisani ambao Kardinali Pengo aliupinga!

Taarifa kuhusu mali za Gwajima ni hii hapa:

...Gwajima ana miliki nyumba nne za ghorofa Mbezi beach na kwa mujibu wa ripoti ya uthamini wa nyumba hizo jumla zina thamani ya bilioni 11 na milioni 400 (11.4 bilioni) pesa za Kitanzania.

...Pia ana nyumba nyingine kadhaa kwenye maeneo mbalimbali nchini ila hadi hivi sasa taarifa za uhakika za thamani ya nyumba hizo bado hazipo wazi.

...Gwajima ana miliki helikopta moja na magari ya kifahari kama vile Hammer, Range rover. Magari mengine ni Nissani Murano, Land Rover 4 na Land Cruiser V8.

...Gwajima pia amenunua magari mengine 40 yenye thamani kati ya Tshs 10 milioni na Tshs 20 milioni na kuwapatia wachungaji wake kote nchini kwa ajili ya shughuli zao binafsi na magari yote hayo yapo chini ya umiliki wake.

...Inakadiliwa kuwa akaunti binafsi za Gwajima zilizopo hapa nchini zina zaidi ya Tshs 20 bilioni ikiwa ni fedha zilizopo nje ya fedha za akaunti ya kanisa.

Aidha, pamoja na yeye mwenyewe kutaarifu juu ya mali zake kama ambavyo zimeorodheshwa hapo juu, lakini siku ya jana akiwa anahubiri kanisani kwake alikana kuwa yeye sio tajiri! 

Gwajima alikaririwa akisema kwamba mali zote anazomiliki ni baraka tu za Mungu na sio kwamba yeye ni tajiri. Gwajima alisisitiza kuwa yeye ni maskini kama walivyo maskini wengine wakiwemo wahumini wake, na wanaosema yeye ni tajiri wanawivu na wanamuonea. 

Source: HabariLeo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao ndio manabii wetu

    ReplyDelete
  2. Mwiteni kwanza Chenge na Rizi1 waeleze mali zao. Ndio wengine wafate. Acheni ukuda bongo kila mtu ni mwizi tu. Wenye wivu ni wale wasiokuwa na pesa lakini hata wao wakipata mwanya ni wezi tu.

    ReplyDelete
  3. kweli kabisa hao ndio manabii wetu.

    ReplyDelete
  4. wezi tu hawana unabii wowote

    ReplyDelete
  5. Kweli sio mbaya kutaka kujua mchungaji anapata wapi umiliki wa mali zote hizo,ukizingatia kumekuwa na uhusishwaji wa viongozi wa dini na madawa ya kulevya,Lakini ingekuwa bora na kuonyesha picha nzuri kwa Wa-Tanzania kama mngeanza kwa viongozi wa serikali kwanza ndipo muende kwa hawa viongozi wa dini na bila kusahau wasanii wote,vinginevyo ni uonevu tu.

    ReplyDelete
  6. Hiyo nikuwaibia waumini vihela vyao walivyo dunduliza na kujirundika yeye na familia yake what evil people!!!!! umeona wapi mtu anatangazi neno la mungu halafu anaishi kama celebrate, kama si wizi nini mnaibia masika halafu mnadai utauona utukufu wa mbiguni. Please give me a break !!!

    ReplyDelete
  7. wewe unaongea nini??? kiongozi wa dini na mamali yote hiyo unapeleka wapi??? sio hela za sandaka hizo????

    ReplyDelete
    Replies
    1. SADAKA TU?MBONA KKT,RC,ANGLICAN NA WENGINE WENGI WANATEGEMEA SADAKA LAKINI HAWANA UTAJIRI WA HIVYO INGAWA WAKO KWENYE HUDUMA MIAKA MINGI?

      Delete
  8. mmmmmmm jamani mali zimekuwa nyingi mno nadhani inabidi achunguzwe vizuri maana mwanainchi wa kawaida tu kumiliki mali zote hizo na zaidi ya bilioni 20 kwenye acc binafsi mmmhh

    ReplyDelete
  9. TAJIRI SANA,KWA KAZI YA UCHUNGAJI TU HAIWEZEKANI.

    ReplyDelete

Top Post Ad