Mama Ajifungua Mtoto na Kisha Kumtupa Katika Shimo la Takataka ( Jalala) jijini Mwanza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mama mmoja mkazi wa kata ya Mkuyuni-Sokoni wilayani Nyamagana jijini Mwanza (jina lake halikufahamika mara moja) amejifungua mtoto wa kiume na kisha kumtupa kwenye shimo la kutupa taka (jalala) eneo a Mkuyuni jijini hapa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa watoa taarifa kwa viongozi wa serikali aliyetoa sharti la kutotajwa jina lake amesema:
 
“Mimi ni mfanya usafi hapa Mkuyuni, wakati ninaenda kumwaga uchafu pale dampo nikakuta kitoto kichanga kimetupwa maeneo hayo ndipo nilipoenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkuyuni-Sokoni ili wafanye utaratibu wa kukitoa hapo:”
 
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Mkuyuni, Godwin Peter  Kyangara,  amesema: “Mimi nimeletewa hizi taarifa za mtoto huyu aliyetupwa maeneo haya mida ya saa 2:30  asubuhi, baada ya kupokea taarifa hizo ikabidi nikatoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ndipo walipokuja kuuchukua mwili wa mtoto huyo.”
 
Inasemekana kwamba mtoto huyo alikuwa tayari ana umri wa miezi tisa hivyo mzazi wake alikuwa tayari amejifungua ndipo alipoamua kumtelekeza kwenye shimo hilo la kutupa takataka.
 
Kwa upande wake, diwani wa kata ya Mkuyuni, Charles Fashion, ameeleza kuwa ameshangazwa na kitendo hicho cha mwanamke kujifungua mtoto na kumtupa jalalani ambapo alisema inabidi atafutwe na apewe adhabu iwe fundisho kwa akina mama wengine wenye tabia kama hizo katika jamii.
 
Aidha, Jeshi la Polisi jijini Mwanza limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa bado juhudi za kumtafuta mwanamke huyo aliyetenda unyama huo zinaendelea ili afikishwe mahakamani  kujibu mashtaka yanayomkabili.




Mpekuzi blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yote haya ni mitihani yake mola mana wengine anajua hawa hawahitaji watoto na anawapa na kuna wale wanakesha kuomba watoto na pengine hawapi kabisa yote mitihani tu! mi nashauri elimu itolewe kwenye mashule, mihadhara ya dini, vitongojini , mitaani na mote kama mtu haitaji mtoto aliyembeba akijifungua kuna sehemu anaweza mpeleka na hatashitakiwa kwa kufanya hivyo kuna watu wanawahitaji awo watoto wataasiliwa, mana binadamu wengine hawana utu kabisa awo wagojwa wa akili hawatupi watoto wanapojifungua! nimesimuliwa story na mama wa kituo cha kulea watoto aliingia mwanamke aliyeathirika na madawa ya kulevya na kumuacha mtoto wake akatimuka na hakurudi kamwe sasa itakua mtu wa kawaida kweli jamani!! !

    ReplyDelete
  2. eeeeee jamani why?????? si urge muweka mlangoni kwa mtu akapatikana akiwa mzima??? mbona wanawake mnakuwa na roho za kikatili hivyo.

    ReplyDelete
  3. UBAYA NA UKATIRI ANAANZA MWANAUME, MWANAMKE ANAMALIZIA TU.CHECK SOURCE

    ReplyDelete
  4. Anonymous 10:38 am hata mimi ni mwanamke ubaya unaanza kwa mwanamke, kwanini uli do bila kinga?

    ReplyDelete

Top Post Ad