Mbona Jitihada Anazotifanya Sasa Kiongozi Mkuu Zitto, Hatukuziona Wakati Akiwa CHADEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Just thinking loud! 

Sasa anafanya safari juu ya safari, mikutano juu ya mikutano, facebook, twitter, kukutana na waandishi wa habari usiku wa manane, nk. Kiongozi huyu mkuu kwa sasa halali, hatulii, wala hasikii la mkuu. 

Najaribu kuvuta taswira nyuma kidogo, wakati akiwa chama kilichomlea, chama kilichomfikisha hapo alipo sikuziona jitihada hizi. Wakati huo, wenzake wakifanya mkutano Arumeru, yeye alikwenda kula bata Germany. Wakati wakiendelea na M4C, yeye alikuwa Uswizi akisaka kwa udi na uvumba majina ya waliohifadhi fedha huko. Sababu hazikuisha ilimradi tu jina na sura yake isionekane katika timu ya ukombozi.

Ninachojiuliza, kazipata wapinguvu hizi za ziada, ambazo siku chache zilizopita hakuwa nazo. Ukisoma alama za nyakati, low profile ya wakati huo na high profile ya wakati huu utajiuliza maswali na utapata hisia, hisia za usaliti. Deal lilipangwa kitambo kwa siri likabumburuka, akaenda mahakamani. Kwa sasa ni utekelezaji wa deal hilo kwa hisani ya watu wa Marekani, naamini nalo litabumburuka. 

Kama Taifa hili lingekuwa la uwazi na ukweli, na kama ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali angeweza kutupia jicho, tungetaka kufahamu juu ya mapato na matumizi ya chama hiki kwa miezi mitatu tu iliyopita. Term of reference zingekuwa nini vyanzo vya mapato ya Matangazo ya moja kwa moja, safari ya kusini, na kama mapato haya yanaripiwa kodi *income tax* 

Mtu aweza kujiuliza, pamoja na madeni kwenye asasi za fedha, je ni kweli Milioni 5 zilizotangazwa kama salio la account ndizo zinagharamia mikutano na safari hizi kibao.

Democrasia inapokwa kwa watu kukubali kutumika kwa masilahi yao binafsi!

By Rpg-JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wajinga ndio watakao amini Kua zito Kabwe ni mpinzani lakini Kama Mungu kakifikisha japo darasa la 7 zito ni CCM damu na hicho Chama anachokiongoza ni cha wanaCCM wachache na wasaliti pia toka ndani ya CCM

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wajinga kama nyinyi ndo wenye mawazo mgando, mnafikiria mtu kutoka CHADEMA ndo wasaliti but, akina mabele, slaa, na wote waliotoka CCM kuingia chadema hawakuwa wasaliti bali ni mashujaa siyo? JITAMBUE WEWE

      Delete
    2. Mnajisumbua na chama chenu cha wachaga!!! Na bado Zito atakipukutisha chote hicho halafu mjute

      Delete
  2. Zito katumwa kuanzisha Chama wenye Chama wako ndani ya CCM kwa sasa wataungana nae mwezi wa 10 Chama hiki kimeanzishwa na serikali kwa ajili yakuua chadema

    ReplyDelete
  3. Zito umetusaliti kwasababu ya pesa

    ReplyDelete
  4. Zito umetusaliti kwasababu ya pesa

    ReplyDelete
  5. Wewe upeo wakomdogo sn umeandika bila kufikiria huyu sasa hivi nimwenyekiti wa hichi chama lazima awetofauti nakipindi alichokuwepo chadema kumbuka yy hakua mwenyekiti wachadema.kuhusu fedha hilo sio jambo lakushangaza kwani hata wewe kama unauwezo unaweza toa pesa zakusaidia chama chako hilo sio kosa kisheria kunawachama hawapendi kujitangaza kwamba wao ndio wazamini which is fine so fikiria kabla hujaleta hoja za kitoto.

    ReplyDelete
  6. Sawa kabisa mfikirie kabla yakuropoka

    ReplyDelete
  7. chama hiki kinafadhiliwa na wananchi wenyewe

    ReplyDelete
  8. anakampeni mwenyewe wakiwepo wengine waoneshe mapungufu yake atabuma ameanza mapema wakati wa kampeni atakosa ya kuzunguza

    ReplyDelete
  9. Mmeanza unafiki wenu.kwani juhudi alizofanya chadema hamkuziona

    ReplyDelete
  10. ukiwa muongo uwe Na kumbukumbu kaka,a cha kupotosha kwa siasa uchwara uliyonayo,kama huna data bora ukakaa kimya,unaleta una I.leta hoja yenye mashiko.ACT siyo chama cha mtu.

    ReplyDelete
  11. Wewe na udaku yako yote hamna nyimbo zito ni mwenyekiti na anasafiri bila ya kusubiri kupangiwa na freeman mbowe, wassira au kibaka yyte wa chadema sasa wewe kawaambie chadema wamzuie kutangaza Chama chake kwa nguvu zake zote lol

    ReplyDelete
  12. Fimbo ya chadema hiyo.....najua admn unaumia sana tuu...

    ReplyDelete
  13. Acheni ujinga, mnaropoka ropoka tu. Mwandish kama huna cha kuandika utulie

    ReplyDelete
  14. ZITTO JUHUDI HIZI HATUKUZIONA CHADEMA!!???

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nguvu mnayotumia kujadili,kukosoa nakuchukia ACT mngetumia kukiimarisha chadema.hamkumtaka zito, ameondoka sasa inawauma nini,mwache ajenge chama chake.zito kichwa hawezi kutumia hela bila kujustify source of income

      Delete

Top Post Ad