Mimba ya Zari, Familia ya Diamond Wadai Wanashaka na Ujauzito Huo, Kauli ya Penny na Mume wa Zari Ndio Chanzo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SHAKA! Familia ya ‘President’ wa Kruu ya Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ imeamua kuweka kikao kummbana staa huyo aweke wazi kama ni kweli ana uhakika mimba aliyonayo mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari’ ni ya kwake au magumashi, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia ya staa huyo, ndugu wa karibu akiwemo mama, binamu yake Romy Jons, wajomba zake, mameneja na marafiki wa karibu wa familia, waliamua kuweka kikao hicho usiku  hivi karibuni ili Diamond athibitishe kama kweli kiumbe kinachoripotiwa kuwa ni cha kwake magazetini ni chake kweli.
“Ndugu walichachamaa, walitaka kujua kama kweli mimba inamhusu Diamond au ni magumashi ya kiki za vyombo vya habari.

“Kwenye hicho kikao walimualika na Diamond mwenyewe ili aweze kufunguka kama ana uhakika kweli mimba ni yake,” kilisema chanzo hicho

 WALITAKA ATOE MSIMAMO

“Mbali na kutaka kujua kama mimba ni yake, walitaka pia kujua ana msimamo gani na Zari maana kila kukicha wanasikia mambo tofauti katika mitandao na vyombo vya habari,’’ kilisema chanzo hicho.

SABABU ZAZIDI KUANIKWA

Chanzo hicho kilipobanwa na mwanahabari wetu kuhusiana na sababu zilizowafanya ndugu wa Diamond watilie shaka mimba hiyo, kilisema ni kauli ambazo ziliwahi kusemwa na aliyekuwa mpenzi wake Penniel Mungilwa ‘Penny’ na aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga.

“Walishitushwa na kauli ambayo aliwahi kuitoa Penny kwamba Diamond hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini kama hiyo haitoshi, waliitafakari kauli ya mume wa Zari ambaye alidai Zari hawezi kumzalia Diamond ndiyo maana wakataka wapate uhakika,” kilisema chanzo hicho.

 MUAFAKA WA KIKAO

Chanzo hicho kikizidi kumwaga ubuyu mbele ya kinasa sauti cha Risasi Mchanganyiko kwamba, baada ya Diamond kubanwa na nduguze, alithibitisha kuwa Zari ndiyo kila kitu kwake kwa sasa, hivyo wasiwe na shaka yoyote juu ya kiumbe kinachotarajiwa kuzaliwa.

“Diamond aliwahakikishia kwamba mzigo ni wake, na msimamo wake ni kufika katika hatua ya ndoa Mungu akijalia.

 KUMVISHA PETE

“Kuonesha yupo serious baada ya Diamond kuwatoa hofu ndugu zake, alisema atafanya sapraiz siku ya Mei Mosi katika shoo ya mrembo huyo, All White Party itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar,” kilisema chanzo hicho na kudokeza kuwa Diamond atamvisha pete mrembo huyo.

DIAMOND AFUNGUKA

Ili kuweza kupata ukweli, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond ili aweze kuweka wazi juu ya kikao hicho na kama ni kweli anatarajia kumvisha pete Zari. Diamond alifunguka:

“Yeah ni kweli ndugu zangu walikuwa na shaka lakini nimewahakikishia kwamba kiumbe kilichomo tumboni mwa Zari ni mali yangu, kuhusu kumvisha pete ni mapema kidogo kulizungumzia lakini watu wahudhurie kwa wingi katika shoo ya Zari White Party Ijumaa hii pale Mlimani City kwani nimeandaa sapraizi nyingi sana.

“Mei Mosi itakuwa ni siku ya kihistoria sana kwake kwani kuna mambo muhimu mengi natarajia kumfanyia mpenzi wangu Zari, watu watajua rasmi nia yangu kwa Zari maana ni mwanamke ambaye ameamua kujitoa kwa ajili yangu, hivyo sina budi kumuonesha upendo stahiki, nitafanya kila linalowezekana kumuonyesha namna gani nampenda.”

 SHOO YA KIHISTORIA

Kwenye shoo hiyo ya Zari, watu mbalimbali mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo dairekta mkubwa Afrika, Godfather wa Afrika Kusini na Top Ten ya Washiriki wa Shindano la Big Brother ‘Hot Shot’ 2014.
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

34 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hatuwezi kuhudhuria Party za kijingajinga, akafanyie huko huko Uganda kwao, mngetwambia hiyo party inahusu may be kuchangia kukomesha mauaji ya albino au kusaidia watoto yatima tungekuja, lakini kwa upuuzi huu muende na familia zetu tu. wajinga nyieee

    ReplyDelete
    Replies
    1. SEMA HUNA HELA!!! WABONGO BANA!!!!!!

      Delete
    2. Acha wasakatonge wa bongo wana shida sana

      Delete
  2. MIBONGO MUPOO

    ReplyDelete
  3. wanapenda sifa za kijinga tuu, sasa hiyo pati matangazo kila cku kwani nabii atashuka au, alafu bi kizee anatamba et anavunja magazet kila cku. mbona kwao wanamponda sana? domo anataka kumpaisha na wajinga wasojielewa wako nyuma ya matako yao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kazi kwako mwenzio mbunifu anaingiza hela tu

      Delete
  4. WABONGO WAMELALA USINGIZI MZITO, YAANI KIKI ZAO ZA KUZINI NA KUTAFUTA PESA WANATAKA WATU WAWASHOBOKEE, KAMA WAO MALAIKA. WAKATI NI WAZINIFU NA HUYO BI MATENDE KASAHAU WATOTO WAKE KWA KUJIFANYA ANAMPENDA SANA ALMASI. DU! MJINI SIHAMI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwani wewe ni bikira??? he he he he kweli we ni nyani usiyejione kundu lako

      Delete
  5. hawawezi kuishi bila matangazo na uongo,Zari anaakili yake kashamaliza ug.sasa anamzubaisha Domo amle kistaarabu. si tuliambiwa bi kizee ni tajiri na anakazi nyingi, mbona kafika bongo

    ReplyDelete
  6. tumewachoka wahana jipya, tunajua analipa magazeti ili waandikwe waonekane wako juu. pole yao

    ReplyDelete
    Replies
    1. and your point is??? maana ujumbe sent mpaka misuli yote ya kichawi imekutoka pima!

      Delete
    2. and your point is??? maana ujumbe sent mpaka misuli yote ya kichawi imekutoka pima!

      Delete
  7. SIPATI PICHA YULE HAYAWANI SINTA ATAKAVYORUSHA MAPISHA. NAONA WASHAMPA KAZI YA KUMNYOA ZARI KILA WIKI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thank you sana. Hata mm nilihisi ni Sinta ndio sapota wa Zari ktk zile team zao...now confirmed.

      Delete
  8. Ukisikia kichwa maji ndio diamond, kuparamia mimba za watu na kulea mimba za wenzake, sari is in the business, get that domo, open your eyes fool! You rip way you saw. Get DNA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao wamekutana wachaga wawili Mkibosho na Mrombo...kila mmoja anamtumia mwenzake kujinufaisha. Tutafika tu!!!

      Delete
  9. Hahahaaaa. ukistaajabu ya musa utaona ya firauni, kumbe hata family wanawasiwasi na mimba? sasa zaituni hajipendekezi kwa wakwe au hawamtaki jitu zima lishaingia leba x3

    ReplyDelete
    Replies
    1. we unaye jipendekeza kwa hao wakwe zako umepata nini cha ziada kwani? au ndio unafikishwa kileleni kabisa na huyo mchepuko wako halooooo team michirizi mnaonekana mna gubuuuuuuuuu la kuachwaaaaaa

      Delete
    2. Wanaongeaaa sanaaa wenzao wanaingiza pesa koo linauma usiku dagaaa wa maji alooooooooooooooo baaafhi ya watanzania akili amna

      Delete
  10. ulimbukeni ulokosa elimu, hiyo pesa wanaoingiza si ya maana, hata muuza unga anapesa, kazi kwako wewe limbukeni wa pesa za kiki.

    ReplyDelete
  11. ANAEKANDIA UJUE HANA UWEZO WA PESA KULIPIA TIKETI, TUACHIENI SISI WATU NA PESA ZETU HAPA MJINI TUKAINGIE, NYIE MULIOFULIA KALAGENI BAO

    ReplyDelete
  12. ni shidaaaa tu!toka lini mimba iiatangazwa kama biashara?

    ReplyDelete
  13. Party hamna hela za ticket ujinga mtabaki nao nyiye tajiri hatafuti hela kwao tuu popete anajuwa hapa nanjiya ya kupata basi atakwenda kwani ao warabu na wahindi wameja huko hawana kwao pumbavu nyiye kaeni chini nanyiye mfikiriye vipi kupata hela mnakaliya upumbavu wakutukana watu wasiyo wajuwa leo mmeshindwa kulipiya elf 50000 wenye akili ya kutafuta hela wana panda ndege kuja kufurahi weye usinunuee muhogo wakunyweya chai asubuhi weka MB ulale unachezeya interney unatukan
    Kama hawo wenye kusema ana zini 95% apo nyiye wote wana ume kwa wanawake nyote mnazini

    Wanakaye sema katupa watoto wake nyiye hapo mmelelewa na baba zenu 70% hamuwajuwi hata baba zenu ni nani

    Na aliye sema kaingiya labour mara 3 sasa akazaliye chooni kama weye uliza ukadumbukiza chooni yeye kazaa akaleya

    Kuhusu chibu kuleya mimba si yakwakwe kwani yeye ni mjinga kiyasi hicho
    Anauhakika 100 % kama mtoto ni wake

    WATANZANIA NENDENI KWA LE MUTUIUUZ AKAWAPENI LECTURE KWA SABABU NAONA WENGI WALI ISHIYA DARASA LA PILI

    ReplyDelete
    Replies
    1. neno LECTURE umeandika vizuri, basi nakushauri kama unaweza kurudia ulichoandika kwa kingereza itakua vizuri labda tutakuelewa, una point nzuri ila ulichoandika unajua mwenyewe, au tumia kiswahili ata kile cha la nne tu pia tutakuelewa vizuri!au mpe mtu yyte pembeni yako aliyesoma kidogo points zako akuandikie ata akitaka pesa mpe tu ili ueleweke nawewe khaa..!!una haki ya kuchangia jamani bac ebu fanya kati ya hayo niliyokushauri plzz..

      Delete
    2. We wa ajabu kweli mwenzio kaandika point unadai kusoma ajui ....wenzio wanakula bata ata ukiwapondea z not a big deal kwao.......weak up kijana wewe badala muongeee ya maaana mjue na nyie karanga utauzaje utoke bt kelele tu na pesa huna........kisimu icho cha itel na tecno ulopata unaona maisha mtelezo....pesa tafuta zako nawe uongelewe

      Delete
  14. Watu wanatunga uongo kùuza magazeti

    ReplyDelete
  15. Tusimlaumu Almasi manake kipenda roho hula nyama mbichi,,isitoshe Almasi nae ana akili timamu kujua kitugaani anafanya

    ReplyDelete
  16. zari mtu mzima sana na anajua anachofanya,,anachofanya hapo ashafanyaga sana!na kwao alishawamaliza kaamia huku kakutana na dogo ambae ni mshamba hajielewi ndokwanza anaanza so kakurupukia,,hataka kama hujasoma sometymz unaeza ukawa na akili za ziada za kujua upepo unapoelekea. anyway hii muvi inaitwaje kwani!?

    ReplyDelete
  17. PESA TUNAZO LAKINI SI ZAKUTOA KWA AJILI BI KIZEE NA DOMA WANAPATI. MJINGA NA HAYAWANI NA LIMBUKENI NI WEWE ANONY 6.29.UNAEJIBU KILA MTU. TUNAJUA UNALIPWA VIJISENT UWAPE KIKI, KIVYAKO VYAKO MWENYEPESA HUWA HAWAJITANGAZI. LABDA UWE NA VIJISENT NDO UTATAKA DUNIA NZIMA IJUE. OPS! MAMA YAKO ALIWATUMBUKIZA CHOONI NDUGU ZAKO WANGAPI VILE--- MWANAHARAMU USOJIJUA.

    ReplyDelete
  18. Huu uwongo mwingine hauna kichwa wala miguu. Sasa hiyo management ya Diamond na marafiki zake inawahusu nini hiyo mimba? Kwani na wao wana share kwenye familia? Au family matters inawahusu nini? Pelekea Chekechea huu uwongo sio watu wazima na akili zao.

    ReplyDelete

Top Post Ad